📘 Access 10,000+ CBC Exams With Marking Schemes

Prepare your learners for success! Get CBC-aligned exams for Grades 1–9, PP1–PP2, Playgroup and High School - all with marking schemes.

Browse Exams

Instant download • Trusted by 100,000+ teachers • Updated weekly

Kiswahili Form Four  Question Paper

Kiswahili Form Four  

Course:Kiswahili

Institution: Form 3 question papers

Exam Year:2006



FRIENDS SCHOOL KAMUSINGA
KIMILILI
TAMRINI YA PILI
KIDATO CHA TATU
MUHULA WA KWANZA, 2007
MUDA: MASAA MAWILI
MAAGIZO: Jibu maswali yote kwenye karatasi za majibu ulizotengewa


MATUMIZI YA MTAHINI PEKEE
SWALI 1 2 3 4 JUMLA
ALAMA 20 20 20 20 80
TUZO

1. FASIHI SIMILIZI (ALAMA 20)

a. Taja aina nne za ngano katika fasihi simulizi. (alama 4)
b. Andika sifa mbili za kila aina za ngano ulizotaja. (alama 8)
c. Eleza umuhimu wa hadithi katika jamii. (alama 8)

2. USHAIRI (ALAMA 20)

FUNZA
Funza hao wana funza, mafunza ‘sije wafuza,
Mafunzo ‘ sipowafunza, uwele utawafunza,
‘Siache bila kufunza, ulimwengu kuwafunza.
Wana tusipowafunza, mafunza yatawafunza.

Mwaiona haya gani? Wana hao kuwafunza,
Mwapata aibu gani? Maadili kuwafunza,
Pamoja nao kaeni, funza wasije wafunza,
Wana tusipowafunza, mafunza yatawafunza.

Ushauri wapeeni, msiwaache gizani,
Ni wachanga eleweni, mkono muwashikeni,
Hao wana wafunzeni, ngononi waepukeni,
Wana tusipowafunza, mafunza yatawafunza.

Kuanza tunda kumea, sio kwamba wamefika,
Kuanza ua kuelea, linaweza kunyauka,
Ukiwona waelea, ndo’ kwanza kuharibika,
Wana tusipowafunza, mafunza yatawafunza.

Bongo zao zageuka, mambo hayo wafunzeni,
Hisia zabadilika, wafundishe watunzeni,
Ndipo sasa waumbika, msiwaache nyikani,
Wana tusipowafunza, mafunza yatawafunza.

‘Siwawache baharini, mwelekio wapeeni,
Maisha yao lindeni, mafundisho wapeeni,
Enyi nyote eleweni, si wangali ujingani?
Wana tusipowafunza, mafunza yatawafunza.

Gizani wanajikwaa, vijana wanaduwaa,
Wajiona ni masaa, mahewani wanapaa,
Mapenzi yawahadaa, mtegoni wajikwaa,
Wana tusipowafunza, mafunza yatawafunza.

Wanasiasa funzeni, mapadiri wafunzeni,
Waalimu fundisheni, wazazi semezeneni,
Vijana ‘sipoteeni, kwa kukosa mafunzoni,
Sisi sote tuungane, wana wetu tuwafunze.

Maswali

a. Kulingana na shairi hili neno ‘FUNZA’ lina maana mbili. Zieleze. (alama 2)
b. Licha ya shairi hili kuwa tarbia, linaweza pia kuitwa ukaraguni. Eleza. (alama 2)
c. Eleza muundo wa shairi hili. (alama 4)
d. Eleza matumizi ya jazanda jinsi yanavyojitokeza katika shairi hili. (alama 5)
e. Uhuru wa mshairi unajitokezaje katika shairi hili? (alama 3)
f. Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari. (alama 4)

HADITHI FUPI- MAYAI WAZIRI WA MARADHI NA HADITHI NYINGINE- K.W. WAMITILA

3. KACHUKUA HATUA NYINGINE – K.W. WAMITILA

“Kachukua Hatua Nyingine” ni hadithi inayokejeli wingi wa hatua anazoweza kuchukua mtu pasi kutathmini athari za halafu.” Fafanua kwa kurejelea hadithi hii. (alama 20)

4. SIKU YA MGANGA – CHESI MPILIPILI

a. Kwa nini hadithi hii ikaitwa “ Siku ya Mganga”. (alama 6)
b. Eleza tamathali/mbinu tatu za usemi/lugha zilizotumiwa katika hadithi hii. (alama 6)
c. Wahusika wa hadithi hii wanasheheni sifa sawa. Eleza kwa kurejelea, Mwaibale, Asteria Mlekani na Msomi. (alama 6)
d. Taja njia mbili zinazoeneza ukimwi katika hadithi hii. (alama 2)

“mgaagaa na upwa hali wali mkavu”
heri njema!
Kutoka idara ya Kiswahili na lugha zingine.






More Question Papers


Exams With Marking Schemes

End Term 3 Exams

Mid Term Exams

End Term 1 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers