Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Ujenzi wa jamii mpya ni wajibu wa vijana. Thibitisha ukweli wa kauli hii ukirejelea riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.

      

Ujenzi wa jamii mpya ni wajibu wa vijana. Thibitisha ukweli wa kauli hii ukirejelea riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.

  

Answers


ESTHER
(i) Amani na Imani wanakutana na kuamua kushirikiana licha ya kuwa tofauti.
(ii) Madhubuti kuungana na tabaka la chini kuleta madbadiliko. Anakangamana na wote na kuhamia kibandani mwa Amani.
(iii) Amani na madhubuti ambao ni vijana wanahimiza usawa na hivyo kugawia maskini ardhi.
(iv) Amani na Imani kubadili Imani na mtazamo wa Wanasokomoko kuhusu walemavu/watu wenye mahitaji maalum na kumfanya Majisifu kuenzi wanawe kama binadamu kamili.
(v) Amani na Madhubuti kusaka haki ya Yusuf na kumtoa gerezani.
(vi) Amani kukataa kuishi katika nyumba ya Mtemi na kuamua kujenga yake mwenyewe.
Haja ya bidii.
(vii) Amani anaamini maridhiano katika jamii baada ya chuki. Anamshawishi Oscar
Kambona alilipize kisasi kwa kumuua Mtemi. Pia alimsamehe majisifu kwa kumwibia mswada wake.
(viii) Madhubuti anapendekeza jamii inayo dumisha maadili. Anakataa kazi anayotafutiwa kifisadi na babake.
(ix) Imani anabadili taasubi ya kiume kwa kusema kuwa wanawake wasiwekwe pembeni katika kitabu atakachoandika.
(x) Vijana (Amani) kupinga wizi wa miswada.
(xi) Amani analeta mfumo mpya wa kuendesha serikali na kuhimiza wananchi wawachunguze viongozi vizuri, wawapige msasa.
(xii) Amani na Imani wanataka jamii inayomlinda mtoto wanamlea mtoto japo si mtoto wao.
(xiii) Amani anahimiza uongozi usiwe unafumbiwa macho hata unapokuwa dhalimu.
(xiv) Amani na Imani kupiga vita Imani potovu ambazo zimepitiwa na wakati mf. Kutokunywa maji ya mto Kiberenge. Zozote 10 x 2 = 20

ESTHER STEVE answered the question on April 30, 2018 at 20:44


Next: Onyesha jinsi mbinu ya Taharuki imetumiwa katika Tamthilia ya kigogo
Previous: “Lowela tunapendana mno na ni msiri wangu wala hakuogopa kuniambia yaliyojiri.(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (b) Fafanua ‘yaliyojiri’ kwa mujibu wa msemaji. (c)Lowela ni kielelezo kibaya cha msichana wa kisasa. Thibitisha.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions