Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

1.Taja aina nne za ngomezi za kisasa. 2. Eleza sifa nne za maapizo. 3. Eleza kikwazo vitatu vinavyokumba Fasihi simulizi.

      

1.Taja aina nne za ngomezi za kisasa.
2. Eleza sifa nne za maapizo.
3. Eleza kikwazo vitatu vinavyokumba Fasihi simulizi.

  

Answers


ESTHER
(1) Aina za ngomezi za kisasa.
- Rununu.
- Kengele.
- King’ora.
- Mlio wa ambulensi.
- Kipenga.
- Filimbi.
(2) Sifa za maapizo.
1. Maapizo yalitolewa na watu walioenda kinyume na matarajio ya jamii zao mifano ya watu hawa ni wabakaji, wezi, wauaji na waliowatusi wazazi, wazee au ukoo.Wazazi pia huweza kutoa maapizo kwa wana wao ili kuwaonya dhidi ya hulka mbaya kama vile utumiaji wa vileo.
2. Katika baadhi ya jamii za kiafrika, maapizo yalitolewa kabla ya ulaji viapo.mlaji kiapo anaweza kusema ambaye amefanya tendo hili chuma hiki kimwingie kwenye mboni ya jicho,asiuone mwangaza wa jua tena
3. Maapizo yanaweza kutolewa moja kwa moja na yule aliyeathirika, mtu anapopoteza kitu chake anaweza kuapiza ili kumtisha aliyeiba k.m aliyeiba mbuzi wangu apepenuke na huo mchanga, zizi lake asiweze kulala mbuzi hata mmoja
4. Kidini, Mungu, miungu au mizimu huweza kutoa maapizo kuhusu mustakabali wa mhusika fulani aidha maapizo ya kidini yanaweza kutolewa kama laana baada ya mhusika kukaidi amri za Mungu au miungu, maapizo ya aina hii huathiri mhusika na jamii yake.
5. Maapizo huaminika kuwa yataleta maangamizi kwa jamii, hivyo wanajamii hushauriwa kuyaepuka kwa kutenda mema.
6. Maapizo hutumia fasaha k.m ulumbi watoaji maapizo katika ulaji wa aghalabu huwa walumbi.
7. Maapizo hutumia lugha kali inayonuiwa kujaza woga ili kuonya dhidi ya uovu.

(3)
- Uvumbuzi wa vyombo vya mawasiliano kama tarakilishi.
- Mitambo ya kuchapisha na kuhifadhi maandishi.
- Dini ya Kikristo ambayo inapuuza baadhi ya vitendo au miviga ya F.S.
- Elimu ya kisasa haitambui wala kuthamini F.S.
- Waandishi wengi wa Kiafrika hawashughuliki F.S.
- Vifo vya fanani.
- Ushindani wa F.S. na burundani ya kisasa.
ESTHER STEVE answered the question on May 4, 2018 at 20:05


Next: Give some of the reasons for opposing innovation
Previous: What methods can be put in place to check the network security problems in an IT department?

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions