Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.
Ask, answer and revise exam-style questions across Kenyan subjects and professional courses.
172 Questions View: All Solved Unsolved
‘’ Hakikubakia hata chakula kidogo cha sadaka ya mwenye njaa… ‘’ Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa hoja kumi ukirejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba
Sekta ya elimu ina changamoto nyingi.Thibitisha kwa kurejelea hadithi zifuatazo : a) Mapenzi ya Kifaurongo b) Shogake dada ana Ndevu c) Mwalimu Mstaafu d) Mtihani wa maisha
Alfa Chokocho : Tulipokutana tena “ Mamangu siku ile aliniamsha mapema.” i) Eleza muktadha wa dondoo hili. ii) Tathmini umuhimu wa usimulizi wa mzungumzaji katika kuendeleza dhamira ya hadithi hii. iii) Onyesha jinsi mashaka linavyomwafiki mhusika mwenyewe katika hadithi ya “Ndoto ya Mashaka”
“…..ilmuradi mawazo yanamwadhibu sasa” a. Eleza muktadha wa dondoo hili. b. Fafanua sifa za anayerejelewa katika dondoo hili. c. Onyesha mawazo yanayomwadhibu anayerejelewa na dondoo hili.
Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika diwani ya, ‘Tumbo lisiloshiba na hadithi nyingine.’ Jadili maudhui ya nafasi ya wazazi katika malezi.
“... maendeleo yanadai mchango wa kila mtu, maskini na tajiri” a) Eleza muktadha wa dondoo hili. b) Taja na ueleze sifa nne za msemaji katika dondoo hili. c) Mambo yepi mengine ambayo msemaji huhojiana na wenzake wanapokutana ? d) Taja na ueleze maudhui matatu yanayojitokeza katika dondoo hili.
Jadili maudhui ya elimu katika Diwani ya Tumbo lisiloshima ukizingatia hadithi zifuatazo: a) Mapenzi ya kifaurongo b) Shagake dada ana ndevu. c) Mamake Bakari . d) Mwalimu mstaafu. e) Mtihani wa maisha.
“Hapana cha ala, bwana. Liswmwalo lipo,kama halipo linakuja. Kumbuka msemo mabrafu wa siri ya kata iulize mtungu . Mtungi wenyewe ni mimi ……” a) Eleza muktadha wa dondoo hili. b) Bainisha tamathali mbili za lugha zilitotumiwa katika dondoo hili c) Fafanua sifa moja ya msemaji inayodokezwa na dondoo hili d) Msemaji wa mabo haya baadaye anageuka kata na kupiga mbizi mtungini. Eleza ukitoa mfano kutoka hadithi. e) Eleza maudhui ya malezi kama yanavyojotokeza katika hadithi ya shogaka Dada ana Ndevu .
“Hatuwezi kumaliza kula, kila leo tunakula” (a) Eleza mukadha wa dondoo hili. (b) Fafanua tamathali ya usemi iliyotumika. (c) Eleza umuhimu wa mnenaji. (d) “Lakini nakwambia tena, kula kunatumaliza” Kwa kudokeza hoja kumi, jadili ukweli wa kauli hii.
“Hebu sikiza jo! Pana hasara gani nzi kufia kidondani?” a) Eleza muktadha wa dondoo hili. b) Taja na utoe mifano ya mbinu nne za lugha zilizotumika katika dondoo c) Onyesha ukweli wa kauli “ nzi kufia kidondani” unavyodhihirishwa na wahusika katika hadithi.
“ Wahusika katika hadithi shibe inatumaliza wanatumia uhuru wao vibaya.” Onyesha ukweli wa kauli hii kwa kutoa mifano.
“… Ningeondoka shuleni mapema niende niibe au niue ili niwe mtu wa maana.” a) Eleza muktadha wa maneno haya b) Onyesha vile kinaya kinavyojitokeza c) “ Kinaya kimetumika kwingine kwingi katika hadithi ya Mwalimu Mstaafu.” Thibitisha
“ Mwandishi wa haditi ya Tumbo lisiloshiba ametumia mbinu ya Jazanda kwa ufanisi mkubwa.” Thibitisha
Ilikuwa kama vile katia saini ya kutiwa kitanzi bila ya kutambua vipengele vya sheria za utiaji huo wa kitanzi. a) Fafanua tamathali mbili zilizotumika katika dondoo. b) Jadili vipengele vitano vya sheria zinazorejelewa katika hadithi nzima. c) Onyesha dhiki iliyompata mrejelewa kwa kukosa kuvitambua vipengele hivyo.
"Penzi lenu na nani? . . . . Mgomba changaraweni haupandwi ukamea. Potelea mbali mkate wee!" a) Eleza muktadha wa dondoo hii. b) Taja na ufafanue mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili. c) Onyesha vile maudhui ya utabaka yanavyo jitokeza katika hadithi nzima. d) Eleza sifa sita za mzugumzaji kwenye dondoo.
Jadili mashaka ya Mashaka katika hadithi ya “Ndoto ya Mashaka”
“Rasta twambie bwana!” a) Weka dondo katika muktadha b) Taja mbinu zilizotumiwa na mwandishi katika dondoo hili c) Ni kwa vipi mzungumziwa anamchukulia mwalimu mkuu kama hambe? d) Je, mtihani wa maisha ni amwani faafu ya hadithi hii.
Bara la Afrika limekumbwa na umaskini mkubwa. Fafanua dhana ukirejelea hadithi ya Tumbo lisiloshiba na Mapenzi ya Kifaurongo
“..Wanafunzi wa chuo kikuu si kama watoto vikembe wa shule ya chekechea…..” a) Weka dondoo hili katika muktadha wake. b) Taja na ufafanue tamathali ya usemi uliyotumiwa katika dondoo hili c) Hadithi hii inadhihirisha utegemezi wa binadamu. Fafanua.
Onyesha jinsi maudhui ya utabaka na mapenzi ,yanavyojitokeza katika hadithi ya mapenzi ya kifaurongo.
Huku ukirejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba na Shibe Inatumaliza, fafanua maudhui ya ukiukaji wa haki.