Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Got a question or eager to learn? Discover limitless learning on WhatsApp now - Start Now!

Kcse Kiswahili Karatasi Ya 3 Fasihi 2015 Question Paper

Kcse Kiswahili Karatasi Ya 3 Fasihi 2015 

Course:Kiswahili

Institution: Kcse question papers

Exam Year:2015



Kiswahili Karatasi 3 Fasihi 2015

SEHEMU A: FASIHI SIMULIZI
1 Lazima
(a) Soma utungo ufuatao kisha ujibu maswali .

Hadithi ya Jabari inasimuliwa na jamii nyingi. Jabari alizaliwa kashika mkuki mkononi.
Mawio ambayo kilio chake, ambacho kwa kweli kilikuwa mngurumo, kilipopasua anga, nyota
kubwa ilianguka kutoka mbinguni. Ulimwengu mzima ulitetemeka na kutwaa giza.
Hata kabla mama mtu hajampa ziwa, Jabari alikuwa amevuvumuka na kuwa ghularnu wa
miraba minne. Haikuchukua muda, hata vita kati ya jamii ya Sule na Suna vikaanza; kikosi
cha Sule cha wapiganaji mia moja kikawajia vijana wa Suna kwa sime na nyuta. Jabari
aliwakabili kwa konde moja pekee, akakirambisha dongo kita kizima.
(i) Bainisha kipera cha utungo huu. (alama 1)
(ii) Toa sababu mbili kuthibitisha jibu lako la (i) hapa juu. (alama 1) .
(iii) Eleza manufaa sita ambayo jamii itapata kwa kukirithisha kipera hiki kwa
vizazi vijavyo. (alama 6)
(b) Soma utungo ufuatao kisha ujibu maswali.
Ndimi Mwimo mdumishaji ukoo
Ndimi ndovu mtetemesha ardhi
Aliyepigana vita, ukoo kuauni
Ziliporindima zangu nyayo
adui alinywea, mafahali na mitamba akatukabidhi
Kwen ye misitu sikuwa na kifani
Paa na hat a visungura
vilijikabidhi kwangu
kwa kuinusa tu mata
Nani aliyewahi
ngomani kunipiku?
Makoo hawakunisifu, wakalilia nikaha?
Kwenye nyanja za michuano
nani angethubutu, ndaro kunipigia?
Sikuwabwaga chini, kwa yangu maozi, hata kabla hatujavaana?

(i) Andika aina ya sifo hii. (alama 1)
(ii) Bainisha shughuli mbili za kiuchumi na mbili za kijamii zinazoendelezwa na
jamii inayosawiriwa na utungo huu. (alama 2)
(iii) Eleza mambo matano ambayo yanaweza kuzingatiwa ili kufanikisha
uwasilishaji wa utungo huu. (alama 5)
(c) Eleza faida nne za matumizi ya nyimbo katika uwasilishaji wa ngano. (alama 4)
SEHEMU B: RIWAYA

K. Walibora:
Kidagaa Kimemwozea

Jibu swali la 2 au la 3.
(alama 4)
"Moyo ulimpapa na kijasho chembamba kumtekenya juu ya mwanzi wa pua. Akahisi uchungu
wa mwiba wa kujidunga."
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
(b) Huku ukirejelea riwaya hii, fafanua kwa kutoa hoja nane, namna anayelengwa na kauli
hii alivyojidunga miiba. (alama 16)
(a) "lmani ni kielelezo cha vijana waliowajibika." Thibitisha kauli hii kwa kurejelea
mifano kumi kutoka Kidagaa Kimemwozea. (alama 10)
(b) "Nadhani Mzungu pale alipo hana budi kutambua ukomavu wa Mwafrika katika
kila sekta ya maisha
."
Onyesha kinyume katika kauli iliyopigiwa mstari kwa kurejelea uongozi wa T moko.
(alama 10)

SEHEMU C: TAMTHILIA

T. Arege:
Mstahiki Meya

Jibu swali la 4 au la 5.

"Kushindana naye ni kama kushindana na ndovu. Utapasuka."
(a) (i) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(alama 4)
(ii) Bainisha tamathali moja ya usemi inayojitokeza katika dondoo hili.
(alama 2)
(b) Kwa kurejelea hoja saba, thibitisha kwamba kushindana na anayerejelewa na
kauli hii ni saw a na kushindana na ndovu. (alama 14)
"Wahenga wanasema dawa ya adui ni kummegea unachokula."
(a) (i)
Andika suala linalodokezwa na kauli iliyopigiwa mstari.
(alama 2)
(ii) Jadili hoja nane zinazoonyesha narnna suala hili linavyozorotesha hali ya
maisha Cheneo. (alama 8)
(b) Jadili jinsi vyombo vya usalama vilivyotumiwa kuuendeleza uongozi wa Cheneo. (alama 10)

SEHEMU D: USHAIRI

Jibu swali la 6 au la 7

6 Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Daima alfajiri na mapema
Hunipitia na jembe na kotama
Katika njia iendayo kondeni
Kama walivyofanya babuze zamani;
Nimuonapo huwa anatabasamu
Kama mtu aliye na kubwa hamu
Kushika mpini na kutokwa jasho
IIi kujikimu kupata malisho.

Anapotembea anasikiliza
Videge vya anga vinavyotumbuiza
Utadhani huwa vimemngojea
Kwa usiku kucha kuja kumwimbia;
Pia pepo baridi kumpepea
Rihi ya maua zikimletea
Nao umande kumbusu miguu;
Na miti yote hujipinda migongo
kumpapasa, kumtoa matongo;
Na yeye kuendelea kwa furaha
kuliko yeyote ninayemjua
Akichekelea ha ha ha ha ha ha ...

Na mimi kubaki kujiuliza
Kuna siri gani inayomliwaza?
Au ni kujua au kutojua?
Furaha ya mtu ni furaha gani
katika dunia inayomhini?
Ukali wa j ua wamnyima zao
Soko la dunia lamkaba koo;
Dini za kudhani zamsonga roho
Ayalimia matumbo ya waroho;
Kuna jambo gani linamridhisha?
Kama si kujua ni kutokujua
Laiti angalijua, laiti angalijua!

(T. Arege)

(a) Eleza hali ya mzungumziwa katika shairi hili.
(b) Huku ukitoa mifano, onyesha aina mbili za uhuru wa kishairi uliotumiwa katika shairi
hili. (alama 2)
(c) Fafanua aina tatu za taswira ukirejelea ubeti wa pili. (alama 3)
(d) Eleza umuhimu wa maswali ya balagha katika shairi hili. (alama 2)
(e) Bainisha vipengele vifuatavyo vya kimtindo katika shairi hili: (alama 3)
(i) tashhisi
(ii) kinaya
(iii) tashbihi
(t) Eleza toni ya shairi hili. (alama 2)
(g) Bainisha nafsineni katika shairi hili. (alama 1)
(h) Changanua muundo wa shairi hili. (alama 3)

7 Soma Shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

T. Arege: Mwili
Leo kitaka nifike, natamani, ila wauma mwili
Kwa kazi nihusike, samahani, unahiliki mwili
Napenda nihesabike, rnakundini, ila huwezi mwili.

Vitisho pamwe kelele, ninavicha, kwa nafsi na mwili
Ila ugonjwa utirnile, umechacha, na kuudhili mwili
Msikose simile, magalacha, si gurudumu mwili.

Vingekuwepo viraka, kuutia, ngeushuruti mwili
Kifundi kivipachika, kuingia, hata kuridhi mwili
Upya ukaungilika, kuvutia, roho na wake mwili.

Lakini kamwe haiwi, kuvipata, vipande vyake mwili
Sihofu kupata mawi, sitajuta, kupigania mwili
Hata kufutwa sikawi, nitakita, kidete nao mwili.

Kazi ninaithamini, ni hakika, akilini na mwili
Ila kamwe siamini, kusagika, damu, jasho na mwili
Uwele hususani, kioneka, nguvu hitishi mwili.

(a) Eleza dhamira ya mtunzi wa shairi hiIi. (alama 4)
(b) Fafanua mbinu nne za lugha zilizotumiwa katika shairi hili. (alama 8)
(c) Eleza toni ya shairi hili. (alama 2)
(d) Ni nani anayezungumziwa na nafsineni katika shairi hili? (alama 1).
(e) Eleza bahari ya shairi hili kwa kurejelea vipande. (alama 2)
(t) Andika ubeti wa mwisho kwa lugha ya nathari. (alama 3)

SEHEMU E: HADITHI FUPI
K. Walibora na S. A. Mohamed (Wah):
Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine
"Mizizi na Matawi" (A. Abdulla Ali)
8 (a) "Mwisho, naomba sote tusameheane kwa dhati."
(i) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
(ii) Jadili umuhimu wa hotuba ya mzungumzaji katika hadithi hii. (alama 8)
(b) Onyesha jinsi hadithi, "Mke wangu" ilivyotumia kinaya kufanikisha ujumbe wake.
(alama 8)






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers