Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Kiswahili Lugha Form 4 Term 2 2016 Question Paper

Kiswahili Lugha Form 4 Term 2 2016 

Course:Kiswahili

Institution: Form 4 question papers

Exam Year:2016



102/2
KISWAHILI LUGHA
KIDATO CHA NNE
MUHULA WA PILI 2016
SAA 2.3O

CHETI CHA KUHITIMU ELIMU YA SECONDARI NCHINI KENYA
KISWAHILI PP 102/2
KIDATO CHA NNE MUHULA WA PILI 2016

MAAGIZO
Jibu maswali yote

Maswali:
a) Taja sababu za Makali kwenda nyumbani.
(alama.2)
b) Kuna sababu gani kati ya mlahaka wa Makali na msimulizi?
(alama.2)
c) Msimulizi na makali wana tofauti gani kwa mujibu wa taarifa?
(alama.2)
d) Fafanua mtazamo wa Makali kuhusu ndoa.
(alama.2)
e) Kwa kurejea kifungu fafanua hulka ya wazazi wa Makali kumhusu Imani.
(alama.2)
f) Fafanua msimamo wa Makali kumhusu Imani
(alama.2)
g) Eleza maana ya maneno haya:
i) Kilichokuwa nyuma ya pazia
ii) utashi
iii) Kupasua mitaro ya uchochole

sehemu II: Ufupisho (alama 15)
soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
Mitihani imetumiwa siku nyingi kama kigezo cha kupimia werevu wa mwanafunzi katika kutekeleza majikumu ya kiakili yenye kuhitaji ustadi mbalimbali. Hii ni njia ya kuaminika na rahisi ambayo imetumiwa kwa miaka mingi na watahini kukadiria uwezo wa mtu. Lakini wale wanaopinga mitihani wasema kuwa mitihani haipimi kwa njia inayoaminika, uwezo wa mwanafunzi ila tu uwezo wa kukariri mambo kama kasuku kwa muda mfupi uliojaa vitisho na shinikizo.

Wasiodhamini mitihani pia wanadai kuwa mitihani humpa mtahiniwa wasiwasi mwingi. Hi ni kwa sababu umuhimu na hadhi ya mitihani imekuzwa sana miongoni mwa watahiniwa wa jamii nzima kwa jumla. Mtihani ndicho kigezo pekee kinachokadiria kufaulu au kutofaulu kwa mwanafunzi.
Watahini hawajali sana masuala mengine ambayo yanaweza kuathiri jinsi mwanafunzi anavyowenza kuufanya mtihani. Kwa, mfano mtahiniwa anaweza kuwa mgonjwa siku ya mtihani au penginemzazi wake mmoja anaweza kuwa mgonjwa au pengine hakulala vizuri siku iliyotangulia mtihani. Haya yote ni masuala yanayoweza kumfanya mtahiniwa kutofanya vizuri katika mtihani. Elimu nzuri humfundisha mwanafunzi kutumia akili yake. Lakini mfumo wa elimu unaipendelea mitihani haufanyi hivyo. Mfumo wa aina hii husisitiza kufundisha yale yanayopatikana katika mwongozo uliotolewa tu. Mwanafunzi hapewi motisha ili kusoma kwa mapana na marefu ili kupanua akili yake. Badala yake mwanafunzi hufungiwa kwenye uwanja finyu ambamo haruhusiwi kutoka. Mwalimu naye kadhalika hana uhuru wa kumfundisha mwanafunzi kile anachofikiria kuwa muhimu katika maisha. Badala yake jukumu kubwa analoachiwa mwalimu huwa ni kumpa mwanafunzi mbinu za kujibu maswali nakupita mitihani.

Ingawa wanaotetea mitihani hudai kuwa matokeo ya mitihani ni ya kuaminika kwa sababu husahihishwa na watu wasiowajua watahiniwa. Lakini ni vizuri pia kukumbuka kuwa watahiniwa ni binadamu tu. Binadamu huchoka, huhisi njaa na zaidi ya yote anaweza kufanya makosa. Licha ya haya yote. Watahini hutakiwa kusahihisha rundo kubwa la karatasi kwa muda mfupi.

Mjadala uliopo kati ya wanaopendelea mitihani na wale wasiopendelea watukumbusha kuwa kuna haja kubwa ya kuendelea kuboresha mfumo wa mitihani ili uweze kukadiria kwa yakini uwezo wa kiakili wa mtahiniwa.

Maswali
a) Kwa maneno 70, eleza ujumbe unojitokeza katika aya tatu za kwanza (alama 9)
matayarisho
jibu a) Hoja


b) Wanaopendelea mitihani wanatetea vipi msimamo wao? Eleza kwa maneno 50 (alama. 6)
mayarisho
jibu






d) Badilisha maneno yafuatayo yawenomino za dhahania *(alama. 2)
i) Mchezo
ii) Kupanda

e) Tumia neno wote kama (alama. 2)
i) Kiwakilishi

ii) Kivumishi

f) Andika upya sentensi uliyopewa huku ukibadilisha maneno yaliyopigiwa mstari kuwa nomino (alama. 2)
chakula hicho kilipikwa vizuri kikawavutia wageni.

g) Huku ukitoa mifano, fafanua miundo mitatu ya silabi za kiswahali (alama. 3)


h) Andika upya kwa kufuata maagizo.
Mashaka alipowehuka, Bi Zuhura alijawa na majonzi. (alama. 2)
i) Bainisha yambwa katika sentensi ifuatayo
Hamisi amemvunjia kairu miwa

j) Tambua aina ya virai vilivyopigiwa mstari
Mfanyikazi yule mzembe ameifanya hiyo kazi kwa muda mrefu sana.


k) Andika kwa usemi wa taarifa
“safari yenu itakamilika kesho.” Dereva aliwaambia abiria. (alama. 2)



Sehemu III : Matumizi ya lugha (alama 40)
a) sauti zifuatazo hutumika wapi? (alama .2)
i) /ch/
ii)/h/

b) Mbali na ving’ong’o onyesha matumizi mengine mawili ya kibainishi (alama. 2)

c) Yakinisha

Asingalinipiga asingaliadhibiwa. (alama. 2)


l) Tunga sentensi yenye kishazi huru na tegemezi (alama. 2)
m) Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia mishale.
Kijiji chetu kinahitaji barabara nyingine ya lami. (alama. 5 )



n) Tambua aina za vitenzi katika sentensi ifuatayo (alama. 4)
Nimekuwa nikitaka kumwambia aninunulie kitabu kingine.


o) Tunga sentensi ili kutofautisha maana ya vitate vifuatavyo (alama. 2)
i) ziwa

ii) Siwa

p) Andika kwa ukubwa
kizee kinajikongoja kijiani. (alama. 2)


q) Andika kwa wingi
pahali pa kuchimba bwawa pamenyakuliwa na kiongozi mlafi,

Sehemu IV: Isimujamii (alama 10)
Huku ukitoa mifano fafanua sifa zozote tano za sajili ya dini. (alama. 10)






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers