Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Kiswahili Karatasi 3 Fasihi Form 4 Term 2 Question Paper

Kiswahili Karatasi 3 Fasihi Form 4 Term 2 

Course:Kiswahili

Institution: Form 4 question papers

Exam Year:2016



102/3
KISWAHILI
Karatasi 3
Juni 2016
Muda: Saa 21/( 2)

MTIHANI WA MWIGO 2016
FASIHI
Karatasi 3

Jibu maswali MANNE pekee.
Swali la kwanza ni lazima. Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu Nne zilizosalia yaani, TAMTHILIA, HADITHI FUPI, USHAIRI na FASIHI SIMULIZI.
Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja
Kila swali lijibiwe katika karatasi tofauti.

SEHEMU A HADITHI FUPI
DAMU NYEUSI NA HADITHI NYINGINE


1. Kwa kurejelea hadith zifuatazo katika diwani ya Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine, jadili changamoto zinazowakumba wanawake. (alama 20)
i) Mke wangu
ii) Samaki wa nchi za joto
iii) Tazamana na mauti
iv) Mwana wa Darubini
v) Mzizi na Matawi


SEHEMU B: RIWAYA
KIDAGAA KIMEMWOZEA – Ken Walibora
2. Kwa kuzingatia mifano katika riwaya yote, eleza vile masuala ya mabadiliko na utengano yameasawiriwa. (alama 20)

3. "Moyo wako umeniua kabisa. Kuna mahakama ndani ya moyo wangu ninakojishtaki mwenyewe kila siku, kwa miaka na mikaka. Imenikatia hukumu ya kifo sasa.”

a) Eleza muktadha wa maneno haya. (alama 4)
b) Onyesha tamathali mbili zinazojitokeza katika dondoo hili. (alama 4)
c) Ukirejelea riwaya fafanua wema wa mnenewa katika dondoo hili. (alama 6)
d) Jadili makosa ambayo mnenaji wa maneno haya anajishtaki nayo (alama 6)


SEHEMU C: TAMTHILIA
MSTAHIKI MEYA – Timothy M. Arege
4.Fafanua namna wananchi na wafanyikazi walipigania haki zao kule Cheneo. (20 marks)

5) ‘Naam Baraza la mji wa cheneo kupita kwa Mstahiki Meya, limewapa nafasi hii kujieleza kuhusiana na mgomo wa wafanyikazi uliopo. (Kwa kiburi) haya, uwanja ni wenu ......’
a) Eleza muktadha wa dondoo hii. (alama 4)
b) Fafanua tetesi za wale ambao wamepewa uwanja kujitetea. (alama 16)


SEHEMU D: FASIHI SIMULIZI
6. a) Fafanua hatua za utafiti na ukusanyaji data katika fasihi simulizi (alama 10)
b) Eleza dhima ya lakabu katika Fasihi simulizi. (alama 10)

7. a) Eleza sifa za rara. (alama 5)
b) Eleza umuhimu wa hodiya. (alama 5)
c) Fafanua umuhimu wa miviga katika jamii. (alama 10)


SEHEMU E: USHAIRI
8. Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata.
1. Unanidharau bure Dunia
Na fahamu hunazo
Kunihusu mimi
Ila kwa mavazi ya nje
Yasong’ara pengine.

2. Unanizungusha kokote niendako
Kujitafutia zangu afueni
Nizisetirie zako hasira
Angalau maadili niyanuse
Yaani riziki, mema mavazi na mengine.

3. Nitokapo kutafuta kazi
Kazi tu ya kijungujiko
Memo yako makali yaniuma
Hata ingawa mimi yatima
Japo kifunguamimba.

4. Dada na ndugu zangu
Waniona ndiye mwenye uwezo wa kifedha
Ijapokuwa pia
Nisiye udole mie
Nalilia umaskini.

5. Zao karo zanisubiri
Kila mmoja anining’inia
Kichozi kikimdondokka
Akiona msaada na usaidizi zote kwangu
Kweli mimi tajiri wa kwetu.

Maswali
a) Lipe shairi hili kichwa mwafaka. (alama 1)
b) Tambua sifa NNE bainifu za utungo huu. (alama 4)
c) Eleza maudhui makuu yanayojitokeza katika shairi. (alama 2)
d) Dondoa mbinu mbili za kimtindo alizozitumia mshairi. (alama 4)
e) Ni kwa nini mshairi anajiita wa kwao? (alama 2)
f) Tambua mifano miwili ya mishata katika shairi. (alama 2)
g) Eleza toni ya mshairi. (alama 2)
h) Onyesha mbinu mbili zinazothibitisha kuwa mshairi ametumia idhini ya utunzi. (alama 2)
i) Eleza maana ya msamiati ufuatao kulingana na matumizi katika shairi. (alama 1)
udole


9 B. USHAIRI
1. Kwa neema za Rabuka, daima tumsifu
Hebu sema ‘mekatika, langu guu abadani
Vigumu kushughulika, kweli najaa huzuni
Naam, Hakuna tunda, lisilokuwa na mti.

2. Kwa neema haya yake, isitoshe nyingi sana
Kandanda boli ‘ pigike, jukumule guu tena
Mguu mpenzi wake, kweli hawa wapendana
Waama hakuna tunda, lisilokuwa na mti.

3. Kwa neema na ujazi, musukumo utazidi
Maadamu waziwazi, ja gari lenye sipidi
Pasipo bora mzizi, mapenzi yatafisidi
Mana hakuna bahari, iso mawimbi.

4. Kwa neema zako Mungu, utulinde maishani
Uikarabati yangu, mienendo Duniani
Umkarabati wangu, laazizi maishani
Ewaa! Hakuna kapa, isokuwa na usubi.

5. Kwa neema haya kweli, nitakusifu milele
Ncha nafika kamili, heri nifike kilele
Yakini yote dalili, si ndwele wala upele
Kwani dalili ya ushehe ni kilemba.

Maswali
a) Toa kichwa kifaacho kwa shairi hili. (alama 1)
b) Pambanua mbinu mbili za kimtindo alizotumia mshairi. (alama 2)
c) Eleza muundo wa shairi hili. (alama 6)
d) Tambua mbinu zozote za uhuru wa mshairi na uzitolee mifano. (alama 4)
e) Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari. (alama 4)
f) Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika ushairi. (alama 3)

i) Yatafisidi
ii) ujazi
iii) Hakuna bahari iso mawimbi






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers