Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Form 4 Kiswahili Kartasi La Tatu Question Paper

Form 4 Kiswahili Kartasi La Tatu 

Course:Kiswahili

Institution: Form 4 question papers

Exam Year:2017



KISWAHILI
Karatasi 3
Muda: Saa 2½
FASIHI
Karatasi 3
Maagizo
Jibu maswali MANNE pekee.
Swali la kwanza ni la LAZIMA. Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu NNE zilizosalia yaani, TAMTHILIA, HADITHI FUPI, USHAIRI na FASIHI SIMULIZI.
Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
Kila swali lijibiwe katika karatasi tofauti.


SEHEMU A:HADITHI FUPI
DAMU NYEUSI NA HADITHI NYINGINE


1. Kwa kurejelea hadithi mbalimbali katika Diwani ya Damu Nyeusi, fafanua matatizo KUMI yanayozikumba nchi za bara la Afrika. {alama 20}

Kanda la usufi
2 “..naomba msaada wako… kichwa kinaniwanga na sijui kama shule yenu ina kliniki ambapo naweza kusaidiwa..”
a) Eleza mkutadha wa dondoo hili. {alama 4}
b) Eleza sifa nne za mzungumzaji. {alama 8}
c) “Mzigo wa mwenzio ni kanda la usufi” Fafanua kauli hii ukirejelea hadithi nzima. {alama 12}



SEHEMU B: TAMTHILIA
MSTAHIKI MEYA – Timothy M. Arege

2. Huku ukirejelea mifano mwafaka fafanua mbinu zozote kumi zilizotumiwa na utawala wa Meya Sosi kuendeleza utawala wake dhalimu katika mji wa Cheneo. {alama 20}

3. ‘Wafanyikazi katika bohari ya mafuta wamegoma kwa muda sasa.’
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. {alama 4}
b) Toa sababu kwa nini wafanyikazi wanagoma kulingana na muktadha huu. {alama 4}
c) Wafanyikazi walifanya kazi kwa masaibu mengi kule Cheneo. Fafanua. {alama 12}






SEHEMU C: HADITHI FUPI
DAMU NYEUSI NA HADITHI NYINGINE

: RIWAYA
KIDAGAA KIMEMWOZEA – Ken Walibora
5. “Wema wako umeniua kabisa.kuna mahakama ndani ya moyo wangu ninakojishtaki mwenyewe kila siku kwa miaka na mikaka.Imenikatia hukumu ya kifo sasa”
a) Eleza muktadha wa dondoo hii. {alama 4}
b) mnenaji ana maana gani katika tamthilia hii. {alama 6}
c) Jadili makosa yoyote matano ambayo mnenaji anajishtaki nayo. {alama 10}

.

SEHEMU D: USHAIRI

6. Soma shairi hili kisha ujibu maswali.

Wenye vyao Watubana
1. Wenye vyao watubana, twaumia maskini,
La kufanyiza hatuna, hali zetu taabani,
Kwa sasa kilo ya dona, bei mia ishirini,
Wakubwa tuteteeni, wenye vyao watubana.

2. Washindana matajiri, kwa bei siyo utani,
Na pigo kwa mafakiri, tunao hali ya chini,
Wazeni kutafakari, wanyonge tu madhilani,
Wakubwa tuteteeni, wenye vyao watubana.

3. Limekuwa kubwa zogo, hakwendeki madukani,
Fungu moja la muhogo, sasa shilingi miteni,
Huo mkubwa mzigo, waelemea vichwani,
Wakubwa tuteteeni, wenye vyao watubana.

4. Si hichi wala si kile, hakuna cha afueni,
Bei imekuwa ndwele, wenye macho lioneni,
Ukiutaka mchele, pesa jaza mfukoni,
Wakubwa tuteteeni, wenye vyao watubana.

5. Waliko hao samaki, huko ndiko uchawini,
Wachuuzi hawacheki, zimewatoka huzuni,
Vibuwa havishikiki, kimoja kwa hamsini,
Wakubwa tuteteeni, wenye vyao watubana.

6. Maisha yetu viumbe, yamekuwa hilakini,
Wenye vyao kila pembe, wametukaa shingoni,
Nyama ya mbuzi na ng’ombe, sasa hali maskini,
Wakubwa tuteteeni, wenye vyao watubana.

7. Maji yamezidi unga, kwa lodi wa darajani,
Kajitolea muhanga, kwa bei hawezekani,
Mvao wake wa kanga, ni shilingi elifeni,
Wakubwa tuteteeni, wenye vyao watubana.

Maswali

a) Fafanua toni ya shairi hili. {alama 2}
b) Kwa kutoa mfano mmoja, bainisha matumizi ya TASWIRA katika shairi hili. {alama 2}
c) Andika ubeti wa SITA kwa lugha nathari. {alama 4}
d) Fafanua kwa kutoa mfano, mbinu MOJA aliyotumia mshairi kutosheleza mahitaji ya kiarudhi katika shairi hili. {alama 2}
e) Taja na ueleze bahari mbili za shairi hili ukizingatia:
i) Ubeti
ii) Vina {alama 4}
f) Ujumbe unaowasilishwa katika shairi hili una hadhira lengwa tatu. Zitaje na utoe mifano.
{alama 6}

7. Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata.

Mwepesi wa Kusahau
1. Alikuwa mtu duni, alizongwa na shakawa,
Hana alichoauni, wala alichoambuwa,
Walikimwita mhuni, na thamani kumtowa,
Utamwonea imani, jinsi alivyokuwa
Mwepesi wa kusahau

2. Alipita mitaani, kuomba kusaidiwa,
Mtoto wa kimasikini, riziki haizumbuwa,
Alizubaa mjini, lake jua na mvuwa,
Apate walau nini, japo kipande cha muwa
Mwepesi wa kusahau

3. ‘Ekosa kwenda chuoni, kwani alibaguliwa,
Daima kawa mbioni, kulima au kuvuwa,
Kijembe ki mkononi, aitafuta afuwa,
‘Chumia chungu mekoni, furaha yake haiwa
Mwepesi wa kusahau

4. Wakati ukabaini, mjinga akatambuwa,
‘Katoka usingizini, napo kweupe kukawa,
Watu wakamuamini, kuwa mtu wa muruwa,
Kumbe vile atahini, na jeuri kuingiwa
Mwepesi wa kusahau

5. Leo kawa sultani, mwingine katu hajawa
Hatamani na haoni, nyuma aliyochukuwa,
Anga kwake limeguni, gubi amegubiliwa,
Mwanadamu maluuni, hakika ukichunguwa
Mwepesi wa kusahau

Maswali

a) Eleza dhamira ya shairi hili. {alama 2}
b) Bainisha toni ya shairi hili. {alama 2}
c) Taja na utoe mifano ya aina mbili za tamathali za usemi zilizotumika katika shairi hili.
{alama 4}
d) Eleza umbo la shairi hili. {alama 5}
e) Andika ubeti wa PILI kwa lugha nathari. {alama 5}
f) Eleza umuhimu wa kibwagizo kilichotumiwa katika shairi hili. {alama 2}


SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI

8(a) Eleza dhima ya semi kwa kutoa hoja sita. {alama 12}
1 b) Taja na kufafanua aina nne tofauti za hadithi.


HERI NJEMA






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers