šŸ“˜ Access 10,000+ CBC Exams With Marking Schemes

Prepare your learners for success! Get CBC-aligned exams for Grades 1–9, PP1–PP2, Playgroup and High School - all with marking schemes.

Browse Exams

Instant download • Trusted by 100,000+ teachers • Updated weekly

Mbinu Za Lugha Na Fasihi  Question Paper

Mbinu Za Lugha Na Fasihi  

Course:Bachelor Of Education

Institution: Kenyatta University question papers

Exam Year:2008



KENYATTA UNIVERSITY
UNIVERSITY EXAMINATIONS 2007/2008
INSTITUTE OF OPEN LEARNING
SUPPLEMENTARY/SPECIAL EXAMINATION FOR THE DEGREE OF
BACHELOR OF EDUCATION

ECT 313: MBINU ZA LUGHA NA FASIHI

DATE: Wednesday 8th October 2008 ____________TIME: 3.00pm – 5.00pm
MAAGIZO: Jibu maswali matatu, likiwamo swali la kwanza ambalo ni la lazima.

1.
(a)
Eleza masharti manne ambayo mwalimu anawajibika kuzingatia anapoandika lengo la kipindi. [ 5 ]
(b)
Andika lengo bora la kipindi ambalo limejikita katika ufundishaji wa fasihi. [ 4 ]
(c)
(i)
Fafanua maana ya kauli kwamba lugha hufungamana na utamaduni wa jamii. Toa mifano kuthibitisha ukweli wa kauli hii. [ 6 ]
(ii)
Je, wewe kama mwalimu unapata maarifa gani kuhusu mkabala wa kufundisha Kiswahili kutokana na ukweli wa kauli hii? [ 3 ]
(d)
Jadili kufaa na upungufu wa mbinu ya kimapokeo kama njia ya kufundishia Kiswahili humu nchini. [ 8 ]
(e)
Ukitoa mifano ya kutilia maki jibu lako, jadili kauli isemayo kwamba ā€œmsamiati na sarufi ni kama pande mbili za sarafu mojaā€. [ 6 ]

2.
(a)
Kwa kutoa mifano mahsusi eleza umuhimu wa kufungamanisha ufundishaji wa msamiati na utumiaji wa muktadha pamoja na vifaa vya maono. [10]

(b)
Eleza umuhimu wa vyombo vifuatavyo katika harakati za kufundisha
lugha:
(i)
Ubao
(ii)
Kamusi
[ 10 ]

3.
(a)
Eleza uhusiano kati ya kusikiliza na kuongea pamoja na umuhimu wa kila moja wapo ya mambo haya katika mchakato wa kujifunza lugha. [ 6 ]
(b)
(i)
Ni mambo gani ambayo yanaweza kufanya mwanafunzi ashindwe kusikiliza kwa njia ya ufahamu? [ 6 ]
(ii)
Unaweza kuchukua hatua gani kama mwalimu kusaidia mwanafunzi kuepukana na mambo hayo uliyotaja? [ 8 ]

4.
(a)
Tofautisha baina ya dhana ya uchambuzi na ufafanuzi ukirejelea ufundishaji wa mashairi. [ 6 ]
(b)
Ni mambo gani ambayo hufanya wanafunzi kuwa na mwelekeo hasi juu ya ushairi? [6]
(c)
Eleza hatua ambazo wewe kama mwalimu unaweza kuchukua ili wanafunzi wawe na mwelekeo chanya kuhusu ushairi. [ 8 ]

5.
ā€œFasihi simulizi imepitwa na wakati. Haina nafasi tena katika mfumo wa elimu humu nchiniā€. Jadili kauli hii kwa kurejelea ufundishaji wa methali na nyimbo za kimapokeo. [20]






More Question Papers


Exams With Marking Schemes

End Term 3 Exams

Mid Term Exams

End Term 1 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers