📘 Access 10,000+ CBC Exams With Marking Schemes

Prepare your learners for success! Get CBC-aligned exams for Grades 1–9, PP1–PP2, Playgroup and High School - all with marking schemes.

Browse Exams

Instant download • Trusted by 100,000+ teachers • Updated weekly

Mbinu Za Lugha Na Fasihi  Question Paper

Mbinu Za Lugha Na Fasihi  

Course:Bachelor Of Education

Institution: Kenyatta University question papers

Exam Year:2008



KENYATTA UNIVERSITY
UNIVERSITY EXAMINATIONS 2007/2008
INSTITUTIONAL BASED PROGRAM - APRIL 2008 SESSION
EXAMINATION FOR THE DEGREE OF BACHELOR OF EDUCATION

ECT 313: MBINU ZA LUGHA NA FASIHI

DATE: _Wednesday 27th August 2008_________________TIME: 8.00am – 10.00am
MAAGIZO: Jibu swali la kwanza, na mengine yoyote mawili.

1.
(a)
(i)
Fafanua maana ya kauli isemayo kwamba “lugha ni mfumonasibu”. [ 2]
(ii)
Toa mifano mitatu kuthibitisha ukweli wa kauli hii. [ 3 ]
(iii)
Wewe kama mwalimu unaweza kujifunza kanuni gani za kukuongoza kufundisha kiswahili kutokana na ukweli wa kauli hii? [ 4 ]
(b)
Kama kawaida, wanafunzi wanachukia somo la mashairi.
(i)
Hali hii husababishwa na nini? [ 4 ]
(ii)
Unaweza kuchukua hadua gani wewe kama mwalimu kuwezesha wanafunzi kubadili mwelekeo wao? [ 4 ]
(c)
“Mbinu ya kimapokeo ina walakini na haina nafasi yo yote katika utaratibu wa kufundisha Kiswahili”. Jadili. [ 5 ]
(d)
Mwanafunzi ametamka kama ifuatavyo:
(i)
“ugubwa” badala ya “ukubwa”
“ugimwi” badala ya “ukimwi”
“kubanda” badala ya “kupanda”
“kubima” badala ya “kupima”
(ii)
“ngari” badala ya “gari”
“ndawa” badala ya “dawa”

1
Baada ya kuainisha makosa ya kimatamshi yanayohusika katika makundi mawili, eleza asili/sababu ya makosa haya; na kasha eleza hatua utakazochukua kusaidia mwanafunzi husika kurekebisha makosa yake. [ 8 ]

2.
Mwalimu anawajibika kutilia maanani sera ya elimu nchini pamoja na madhumuni ya ujumla ya somo husika katika utekelezi wa majukumu yake ya kufundisha.
(a)
Taja mambo yo yote manne yanayotiliwa mkazo na sera ya elimu humu nchini. [4]
(b)
(i)
Taja madhumuni yo yote sita ya ujumla ya somo la kiswahili katika shule za sekondari yaliyomo katika silabasi ya kiswahili. [ 6 ]
(ii)
Ukirejelea matatu kati ya madhumuni hayo, eleza jinsi madhumuni hayo yanavyoweza kutekelezwa kutokana na ufundishaji wa kiswahili. [ 10 ]

3.
(a)
Eleza uzuri wa kufundisha msamiati na sarufi kwa njia ya kutumia muktadha na vifaa vya maono. [ 5 ]
(b)
Tuseme unatarajia kufundisha jinsi ya kutendea pamoja na matumizi ya kabla na kama.
(i)
Andika lengo la kipindi linalofaa.
(ii)
Onyesha jinsi utakavyoshughulikia ufundishaji wa mambo haya kwa kutumia muktadha na vifaa vya maono na kuhakikisha kwamba wanafunzi wanadhibiti vilivyo matumizi yake. [ 15 ]

4.
(a)
Kwa kutoa mifano, eleza uhusiano pamoja na tofauti kati ya dhana zifuatazo:
(i)
Lugha
(ii)
Lahaja
(iii)
Sajili
[ 8 ]
(b)
Ukitoa mifano ya kutilia nguvu jibu lako eleza jinsi ufahamu wa Isimu, na hasa zaidi ufahamu wa Isimu jamii unavyoweza kuwa wa manufaa kwako katika kazi yako ya kufundisha kiswahili. [ 12 ]

5.
(a)
Toa hoja za kutetea au kupinga masharti ya kuunganisha lugha na fasihi na kuvifundisha kama somo moja. [ 10 ]
(b)
“Fasihi simulizi imepitwa na wakati na haistahili kufundishwa katika shule”. Jadili.[10]






More Question Papers


Exams With Marking Schemes

End Term 3 Exams

Mid Term Exams

End Term 1 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers