Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Form 4 Kiswahili Kajiado County Joint Evaluation Question Paper

Form 4 Kiswahili Kajiado County Joint Evaluation 

Course:Kiswahili

Institution: Form 4 question papers

Exam Year:2016



SEHEMU A:HADITHI FUPI
1.LAZIMA
K.Walibora na S.A Mohamed(Wah):damu nyeusi na hadithi nyingine
shaka ya mambo
a)"Ndiyo nimeharibika, lakini...................
1)Eleza muktadha wa dondoo hili.(alama 4)
11)Kwa nini msemaji anaonyesha kuwa na dukuduku kuhusu kubahatika kwake?(alama 6)
b)thibitisha jinsi suala la taasubi ya kiume linavyojitokeza katika hadithi za samaki wa nchi za joto ns kanda la usufi(alama 10)
SEHEMU B:RIWAYA
K.Walibora: Kidagaa kimemwozea
Jibu swali la 2 au 3
2.Eleza jinsi mwandishi alivyotumia mbinu ya tashtiti katika Riwaya ya Kidagaa Kidagaa Kimemwozea.(alama 20)
3."Miaka Fulani iliyopita, wakati baadhi yenu mlikua bsdo hamjaona mwanga wa jua.........Mwafrika alionwa kama matapishi na kutumiwa kama kopo la msalani..."
a)eleza muktadha wa dondoo hili.(alama 4)
b)kwa kutoa mifano taja mbinu mbili za lugha zliizotumika katika dondoo hili
c)Eleza sifa za mnenaji(alama 4)
d)thibitisha madai kwamba Mwafrika alionwa kama matapishi na kutumiwa kama kopo la msalani(alama 8)
SEHEMU C:TAMTHILIA
T.Arege :Mstahiki Meya
jibu swali la 4 ama 5
4.a)Meya hastahiki.Thibitisha kwa kutoa mifano kumi(alama 10)
b)Pengo baina ya maskini na matajiri katika tamthilia ya Mstahiki Meya lazidi kuongezeka.Fafanua (alama 10)
5."....Sisi tunatumaini kabisa tunachokitaka ni haki yetu na ya vizazi vingine."
a)Fafanua muktadha wa dondoo hili.(alama 4)
b)Thibitisha kuwa haki hizi zilikiukwa (alama10)
c)Eleza wasifu wa msemaji(alama 6)
SEHEMU YA D:USHAIRI
Jibu swali la 6 au 7
6)Soma shairi lifuatalo kasha ujibu maswali.
1.Fahali la dunia, 2.Fahali la dunia 3)Fahali la dunia,
Ndani ya zizi lake,linanitesa, Latumia mabavu,laoneya, Lisilo na huruma,
linaminya
Linaninyonya, Lasakama linapiga vindama,
Kwa kinyama, Laandama Na wengine wanyama
Linaoneya. Kina mama, Tena bila huruma
Linatesa Laonewa,
4)Fahali la dunia, 5.Fahali la dunia 6)Fahali la dunia,
Limeota pembe,laoneya Kwa kiburi,linatesa, Lidhibitiwe,lisitese
Limehama zizi, Linajigamba, Dunia unganeni,
Laranda duniani, Linatamba, Pamoja shikaneni,
Mashariki na Kusini, Kuwa mwamba, Unyonge kataeni
Linatesa Linaoneya. semeni basi.
(Kutoka :Dunia ya WasakTONG,mUHAMMED Seif Khatib,OUP,Dar es Salaam,uk,45
a)Taja mhusika anayerejelewa kama fahali.Thibitisha.(alama 2)
b)Ni maovu gani yanaoendelezwa na anayerejelewa?(alama 4)
c)Huku ukitoa mifano,onyesha aina mbili za uhuru wa kishairi uliotumiwa katika shairi(alama 2)
d)Changanua muundo wa shairi hili(alama 2)
e)Thibitisha kuwa mishata Imetumika katika shairi hili(alama 3)
f)Mshairi anatoa ushauri gani katika shairi?(alama 2)
g)Bainisha vipengele vifuatavyo vya kimtindo katika shairi hili(alama 2)
1.jazanda 2.Takriri
h)Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika shairi.
1.Lasakama 2.limeota pembe
7.Soma swali lifuatalo kisha ujibu maswali
Ewe tunu ya mtima,kwa nini wanikimbia?
Ndiwe suluhu za zama,waja wakukimbilia,
Waja wanakutazama, madeni wakalipia,
Ndiwe sabuni ya roho,ndiwe mvunja mlima.

Ndiwe mafuta ya roho, walisema wa zamani,
Utanunua majoho,majumba na nyumbani,
Umezitakasa roho,umekua mhisani,
Ndiwe sabuni ya roho,ndiwe mvunja mlima.

Matajiri wanakujua,wema wako wameonja,
Nguo zao umefua,weakupata kwa ujanja,
Sura zao mefufua, wanazuru kila njanja,
Ndiwe sabuniya roho,ndiwe mvunja mlima.

Ndiwe mvunja mlima,onana na maskini,
Watazame mayatima,kwao kumekua duni,
Webebe waliokua, wainue walio chini,
Ndiwe sabuni ya roho,ndiwe mvunja mlima

Ndiwe mvunja mlima, wapi kapata uwezo,
Umezua uhasama,waja kupata mizozo,
Ndiwe chanzo cha zahama,umewatia vikwazo,
Ndiwe sabuni ya roho,ndiwe mvunja mlima.

Umevunja usuhuba,familia zazozana,
Waliokuwa mahabuba,kila mara wagombana,
Roho zao umekaba majumbani wachinjana
Ndiwe sabuni ya roho,ndiwe mvunja mlima

Nakutafuta kwa hamu,sabuni unirehemu,
Sinilipueja bomu,sije kawa marehemu,
Niondoe jahahanamu,ya ufukara wa simu,
Ndiwe sabuni ya roho,ndiwe mvunja mlima.

Naondoka wangu moyo,nikuitapo itika,
Fulusi wacha uchoyo,tatua yalonifikia,
Nichekeshe kibogoyo, name nipate kuwika,
Ndiwe sabuni ya roho,ndiwe mvunja mlima

Maswali
a)Taja nafsi nenewa.Thibitisha(alama 2)
b)Eleza toni ya nafsi neni (alama 1)
c)Eleza arudhi zozote nne zilizingatiwa katika utunzi wa shairi hili.(alama4)
d)Mshairi anawasimulia ujumbe gani katika mleo wa ubeti wa sita?(alama1)
e)Ukitoa mfano eleza mbinu zozote tatu za lugha alizotumia mshairi(alama 3)
f)Andika ubeti wa nne katika lugha nathari(alama4)
g)Jadili jinsi mshairi anatumia ruhusa ya mshairi(alama 2)
h)Kwa kurejelea mpangilio wa vina eleza bahari ambamo shairi linaweza kuainishwa(alama 1)
I)Fafanua maana ya ;
I)ndiwe sabuni ya roho,ndiwe mvunja mlima
II)jehanamu
SEHEMU YA E:FASIHI SIMULIZI
8. a)Kwa kutoa mifano,eleza mbinu tatu ambazo hutumiwa kuzua misimu.(alama 6)
b)Fafanua dhima ya ngomezi katika jamii(alama 4)
c)Eleza sifa nne za mlumbi (alama 4)
D)Ni juhudi zipi ambazo jamii inafanya kudumish a fasihi simulizi(alama 6)






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers