Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Got a question or eager to learn? Discover limitless learning on WhatsApp now - Start Now!

Kiswahili Paper 3 (Fasihi) Question Paper

Kiswahili Paper 3 (Fasihi) 

Course:Kiswahili

Institution: Kcse question papers

Exam Year:2006



Karatasi 3
FASIHI
Saa 2 ½
Jibu maswali manne pekee.
Swali la kwanza ni la lazima.
Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki yaani:
Tamthlia,Riwaya,Hadithi Fupi na Ushairi.Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
FASIHI SIMULIZI
1.(a) Fasihi Simulizi ni nini?(alama 2)
(b) Eleza tofauti nne baina ya Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi.(alama 12)
(c) Nini umuhimu wa Fasihi Simulizi?(alama 6)

TAMTHILIA
Kithaka wa Mberia:Kifo Kisimani
2. "Utani? Haukuwa utani! Mtemi amesikia sifa za uzalendo wako...Mipango yote imepangwa na kupangika..Unajua,bwana,hiari ya binadamu ni kifaa cha mtu mwenyewe.Anaweza kukitumia vizuri au vibaya.Anaweza kukitumia kujinufaisha maishani au kujikwamisha njiani.Inategemea mtu mwenyewe"
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.(alama 2)
(b) Ni mipango gani inayozungumziwa?(alama 4)
(c) Fafanua jinsi baadhi ya wanajamii wa Kifo Kisimani wanavyoitumia hiari yao vibaya.(alama 14)

RIWAYA
Z.Burhani:Mwisho wa Kosa
3.Linganisha wasifu wa wahusika wafuatao na uonyeshe umuhimu wao katika riwaya ya Mwisho wa Kosa:
(a) Monika
(b) Muna (alama 20)

HADITHI FUPI
K.W.Wamitila:Mayai Waziri wa Maradhi
Jibu swali la 4 au la 5.
Siku ya Mganga
4. "Lakini kulikuwa na tatizo gani iwapo..mganga alikuwa hajui chochote kuhusu ugonjwa?"
(a) Fafanua muktadha wa maneno haya.(alama 2)
(b) Eleza sifa za mganga anayerejelewa katika hadithi hii.(alama 10)
(c) Taja na ufafanue madhara aliyosababisha mganga kwa jamii.(alama 8)

7.Soma shairi hili kasha ujibu maswali yanayofuata.
MKULIMA
Mtazameni..nguzo ya Afrika
Mtumwa wa watumwa waloridhiya!
Amekita jembe lake akilisujudia
Kwa tambo liloumbuka na kuselehea
Uso ukifuka ukata ulojifanya tabia
Na machungu ya maonevu alovumilia.

Moyo wake mzito ulokokomaa kama kuni
Haujui tena kutarajia wala kutamani
Umekufa ganzi,kutohisi raha wala huzuni

Basi iteni fikira mambo mukiyafikiri
Siku hamaki yake itapochafuka kama bahari
Siku ukweli wa hali yake utapodhihiri
Umejiandalia vipi...
Huo mkono ulomuumba na kumkausha
Hizo pumzi zilomzimia taa ya maisha
Kumfunga kizuizi,gizani kumtowesha?

Ni jawabu gani alowekewa na wakati
Kipoza ghadhabu ya kiu ingawa katiti
Kuiliwaza hamaki ya njaa hii ya dhati
Njaa ya maisha itakayo kushibishwa.
(a) Eleza mambo muhimu yanayojitokeza katika shairi hili.(alama 4)
(b) Taja na utoe mifano ya aina zozote mbili za usemi zilizotumika katika shairi hili.(alama 4)
(c) Eleza umbo la shairi hili.(alama 3)
(d) Onyesha umuhimu wa matumizi ya kihisishi katika shairi.(alama 2)
(e) Fafanua maana ya:
(i)Siku hamaki yake itapochafuka kama bahari.(alama 2)
(ii) kuipoza ghadhabu ya kiu ingawa katiti.(alama 2)
(f) Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika shairi:
(i)tambo
(ii) ulokokomaa
(iii) kumtowesha(alama 3)






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers