Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Kiswahili Ufahamu Question Paper

Kiswahili Ufahamu 

Course:Secondary Level

Institution: Kcse question papers

Exam Year:2012



UFAHAMU;
Soma makala yafuatatayo kasha ujibu maswali.
Je,unajua kuwa ukandaji wa mwili umetumika kama njia mojawapo ya matibabu toka dahari? Watu wanaofahamika kutumia ukandaji kimatibabu toka jadi ni Wahindi, Wachina,Wagiriki, Warumi na Waafrika.
Ukandaji unajulikana kuwa na manufaa makubwa kimatibabu. Mathalani, ukandaji hufungua vitundu vya ngozi. Ufunguzi huu huondoa sumu mwilini kupitia kwa utoaji jasho. Pili, ukandaji hupunguza mkazo wa misuli. Misuli ikiwa na mkazo zaidi kwa muda mrefu huleta urundikaji wa asidi. Ukandaji huondoa asidi hii, huufanya mwili kuwa miegevu, humletea mtu uchangamfu na kuondoa uchovu.
Hali kadhalika, ukandaji huimarisha mzunguko wa damu mwilini kwa wepesi. Hali hii huhakikisha kuwa virutubishi vya mwili huweza kufikia viungo vyote vya mwili. Hili nalo huchangia kuzidisha uwezo wa mwili kujikinga na maradhi. Hewa safi ya oksijeni .huweza pia kusambaa kote mwilini kupitia kwa uimarishaji wa mzunguko wa damu. Aidha, ukandaji wa taratibu na polepole hupunguza mkazo wa neva na kuziliwaza. Ukandaji wa kasi huchangamsha neva na kuimarisha utendaji kazi wake.
Ukandaji unaweza kufanyiwa kiungo chochote mwilini. Ukandaji huu huweza kuwa na matokeo mbalimbali mwilini.
Mathalani, ukandaji wa njia ya chakula mwilini, hasa tumbo na utumbo, huimarisha usagaji wa chakula na kuchangia uondoaji wa uchafu na sumu mwilini. Nao ukandaji wa njia ya mkojo hustawisha uondoaji wa chembechembe za sumu mwilini.
Kwa kawaida, viganja vya mikono hutumika katika ukandaji. Viungo hivi vinapaswa kuwa na wororo. Wororo huu hupatikana kwa kutumia mafuta. Mafuta ambayo ni bora zaidi kwa shughuli za ukandaji ni ya ufuta au simsim. Matumizi ya kitu chochote kama ungaunga kinachoweza kuziba vitundu vya ngozi hayapendekezwi.
Ukandaji wapaswa kutekelezwa kwa njia ifuatayo. Mtu aanzie mikono na miguu. Kisha aingie kukanda kifua, tumbo, mgongo na makalio. Hatimaye, akande uso na kumalizia na kichwa. Mtu anaweza kutumia kitambaa kukandia mgongo. Ni bora kutumia viganja vya mikono kukandia, Kwa njia hii, manufaa huwa maradufu. Kwanza, tutanufaika na ukandaji na wakati huo huo tutakuwa tukifanya mazoezi ya viungo. Wasioweza kujikanda, wanaweza kuomba msaada. Ni muhimu ukandaji ufuatiwe na kuoga kwa maji vuguvugu.
Kwa walio na tatizo la shinikizo au mpumuko wa damu, wanaweza kubadilisha utaratibu wa ukandaji. Waanzie kichwani, kisha waelekee usoni, kifuani, tumboni, mgongoni, makalioni, miguuni na kuhitimisha mikononi,
Hata hivyo, ukandaji haupaswi kufanywa wakati mtu anaugua maradhi yoyote. Wanawake wajawazito nao wanatakiwa kuepuka ukandaji wa tumbo. Hali kadhalika , ukandaji wa tumbo hauruhusiwi wakati mtu anaendsha ana vidonda vya tumbo au uvimbe tumboni . Hatimaye, ukandaji haupendekezwi iwapo mtu ana maradhi ya ngozi.


MASWALI
a). Ukandaji ni nini ? ( Alama 1)



b). Taja manufaa matatu ya ukandaji. ( Alama 3 )





c)Ukandaji unatakiwa kutekelezwa kwa njia gani ( Alama 2 )



d) Ukandaji unatakiwa kutekelezwa na nani na kwa nini ? (Alama 2)




e) Onyesha ni lini ukandaji haupendekezwi( Aama 2)



f) Eleza maneno yafuatayo kama yalivyotumika kwenye kifungu;
i) Ufunguzi,

ii) auni,

iii) maji vuguvugu.

iv) shinikizo la damu.















More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers