Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Jadili sifa za malumbano ya utani

Jadili sifa za malumbano ya utani.

Answers


KELVIN
Malumbano ya utani hufanywa na watu wawili au makundi mawili ya watu wanapokutana hata hivyo, kila utani una msingi na mpaka wake.
Watu wenye uhusiano mzuri ndio hutaniana, watani hufanya mizaha ambayo inadhibitishwa na masharti yanayotawala uhusiano wao. Baadhi ya makabila hutaniana mazishini.
Malumbano ya utani inaweza kuwa kati ya makabila, marafiki, wajukuu na mababu, wajukuuu na mabibi, bwana na bi harusi. Katika malumbano ya utani, mbinu ya chuku hutumiwa kwa kiasi kikubwa, mbinu hii hunuiwa kusisitiza sifa fulani au kukejeli sifa fulani wazi. Malumbano ya utani yanaweza kuwa hata na masimango.
Huchukua njia ya ushindani, kila mmoja akijaribu kumpiku mwenzake.Wakati mwingine watu hutania wasiokuweko, utani wa aina hii huandamana na uigizaji wa kuchekesha.
kalvinspartan answered the question on July 24, 2018 at 11:25

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions