Trusted since 2008
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Questions and answers: Kiswahili Fasihi

Ask, answer and revise exam-style questions across Kenyan subjects and professional courses.

Q&A Categories

Exams With Marking Schemes

102 Questions    View: All Solved Unsolved

Search Results...
  • Eleza namna mwandishi wa kidagaa Kimemwozea alivyofaulu kutumia fani ya barua kwa kutolea mifano mitano.

    Date posted: October 3, 2019
  • Timothy Arege, Mstahiki Meya "...Sote ni wafanyikazi wa baraza. Kile linachochuma Baraza tunagawana sote." (a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (b) Fafanua sifa tano za msemaji (c) Tunagawana sote ni kinyume ejia hali halisi. Thibitisha.

    Date posted: October 3, 2019
  • SIPENDI KUCHEKA Pana jambo ninatukiya, kwangu hilo ni muhali, Kitenda naona haya, kujishusha yangu hali Sipendi unipe hidaya, sipendi kutenda hili Sipendi mimi kucheka Sipendi mimi kucheka, kuchekea mawi Sipendi na ya dhihaka, kwangu nyemi hiwi Sipendi kwa hakika, mwovu kistawika Halafuye nikacheka! Masikini akiteswa Yatima akinyanyaswa Mnyonge naye akinyonywa Sipendi hata ikiwa Unazo nguvu najuwa Ni hili sitatekezwa Mbona lakini nicheke, kwayo furaha? Na wewe ukajiweke, uli na siha? Na yatima ali pwek.e, wa anahaha? Amenyimwa haki yake, hanayo raha! Na moyo wangu ucheke, kwa ha ha, ha! Kucheka kwa kucheka Mimi katu sitacheka. MASWALI a) Shairi hili ni la aina gani? Thibitisha. b) Taj a sababu zinazomfanya mshairi asitake kucheka. c) Chambua umbo la shairi hili kwa kuzingatia ubeti wa mwisho. d) Tambua nafsineni na nafsinenewa katika shairi hili. e) Tambua toni ya shairi hili. f) Fafanua uhuru wa mshairi katika shairi hili. g) Andika ubeti wa pili kwa lugha tutumbi. h) Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika shairi i) Mawi ii) Nyemi

    Date posted: October 3, 2019
  • “Shaka ya Mambo” (Farouk Topan) Eleza hali ya shaka ya mambo inavyojitokeza katika hadithi ya shaka ya mambo.

    Date posted: October 3, 2019
  • Mstahiki Meya Eleza jinsi wanacheneo walivyotatua shida zinazowakumba.

    Date posted: October 3, 2019
  • Mstahiki Meya "Mtu huvuna alichopanda, ukipanda pojo huwezi kuvuna kunazi." a) Eleza muktadha wa dondoo hili. b) Anayeambiwa alisema nini baada ya kuambiwa haya? c) Thibitisha kuwa wanacheneo walipanda pojo.

    Date posted: October 3, 2019
  • Taja aina nne za hadithi.

    Date posted: October 3, 2019
  • Kidagaa kimemwozea Mtemi Nasaba Bora ni kielelezo cha viongozi wa kiafrika wanaondeleza uongozi mbaya. Jadili kauli hii.

    Date posted: October 3, 2019
  • Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika Diwani Damu Nyeusi, jadili namna ambavyo wahusika wa kike wamesawiriwa.

    Date posted: October 2, 2019
  • Riwaya ya Kidaa Kimemwozea. "Hizi kurani zako ndizo zifanyazo nisije huku …" a) Eleza muktadha wa maneno haya. b) Eleza umuhimu wa mrejelewa katika dondoo hili kwenye riwaya. c) Eleza maisha ya msemaji yalivyokuwa kwa mujibu wa Riwaya ya Kidaa Kimemwozea.

    Date posted: October 2, 2019
  • Damu nyeusi na hadithi zingine "Leo ni siku, siku ya nyani kufa ambapo miti yote huteleza" a) Eleza muktadha wa dondoo hili. b) Bainisha tamathali mbili za usemi zinazojitokeza katika dondoo hili. c) Huku ukitoa mifano, thibitisha maudhui sita ambayo yamejitokeza katika hadithi ya Damu Nyeusi na wanayoyaendeleza.

    Date posted: October 2, 2019
  • Kidagaa kimemwozea "Umenena ndipo ndugu yangu. Hiyo ndiyo tanzia ya Afrika huru." a) Eleza muktadha wa dondoo hili. b) Ni nini sifa za mvuto zinazowaleta pamoja mzungumzaji na mzungumziwa. c) Tambua na ufafanue mbinu inayotumika katika dondoo. d) Kwa mifano mwafaka fafanua tanzia hiyo inayorejelewa katika dondoo.

    Date posted: October 2, 2019
  • Jadili mbinu zifuatazo kama zilivyotumika katika Mstahiki Meya. (a) Jazanda (b) Uzungumzi nafsia (c) Majazi (d) Methali (e) Taharuki

    Date posted: October 2, 2019
  • Eleza dhima ya lakabu kwa kurejelea hoja tano.

    Date posted: October 2, 2019
  • Eleza maudhui ya ukengeushi ukirejea hadithi zifuatazo katika diwani ya Damu nyeusi na hadithi nyingine (i) Mke wangu (ii) Damu Nyeusi (iii) Tazamana na Mauti (iv) Mizizi na matawi

    Date posted: October 2, 2019
  • "Wanyonge ndio wanyongwao" ni kauli inayodhihirika vyema kupitia wahusika tofauti katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea. Jadili.

    Date posted: October 2, 2019
  • Soma mashairi yafuatayo kisha ujibu maswali. SIKUJUA! 1. Kama ningefuga ng‘ombe, mafahali na vindama, Zisingenidhuru pembe, ngeu kuniandama, Samli ni lembelembe, na minofu ya minyama. 2. Kama ningefuga mbuzi, na kondoo kundi zima, Ningewajengea zizi, na maziwa nikakama, Ningewachuna na ngozi, kutengenezea ngoma. 3. Kama ningefuga bata, nao kuku kwa ujima, Chakula siyo matata, ni machicha na mtama, Mayai ningeyapata, na kitoweo kizima. 4. Kumbe nimefuga punda, mashuzi ndio heshima, Ni ukaidi na inda, mateke kurusha nyuma, Nyama limekuwa nunda, mfugaji humuuma. Kiitikio Sikujua wa kufuga, mnyama mwenye faida SHAIRI B Afrika na Watu Wake Mimi ninaona mgonjwa Bado amelala kitandani. Kama hatutamtoa miiba iliyobaki Mgonjwa hataweka miguu yake chini Ili kutembea bila ya kujiegemeza. Miiba iliyomo ndani mwetu lazima Pia iondolewe upesi kabla haijaingia Kati ya mfupa na kufa pamoja nasi. Baada ya kuitoa tuvae viatu vya chuma Halafu tucheze nao mchezo wa siasa na uchumi. Lakini kuitoa miiba hii Tunahitaji macho makali Mikono isiyotetemeka Moyo usio na huruma Na kuona miiba ilipoingilia. MASWALI (a) Onyesha jinsi ujumbe unaopatikana katika ubeti wa nne wa Shairi A na Shairi la B unavyokatisha tamaa. (b) Eleza maana ya mshororo huu kama unavyojitokeza kwenye ubeti wa pili wa shairi B. Baada ya kuitoa tuvae viatu vya chuma. (c) Linganua sifa za kimuundo ukizingatia ubeti wa pili wa Shairi A na Shairi B. (d) Ukizingatia Mshororo wa kwanza kwenye ubeti wa pili wa Shairi A, onyesha jinsi Mshairi alivyotumia kibali chake. (e) Onyesha sifa moja ambayo inadhihirika kwenye shairi la B na ambayo hutawala tungo za aina hii. (f) Nafsi neni amedhihirisha toni gani kwenye shairi A? (g) Taja nafsi mbili nenwa kwenye shairi la B. (h) Andika ubeti wa mwisho wa shairi B kwa lugha ya nadhari.

    Date posted: October 2, 2019
  • SABUNI YA ROHO Ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia? Ndiwe suluhu za zama, waja wakukimbilia, Waja wanakutazama, madeni wakalipia, Ndiwa sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima. Ndiwe mafuta ya roho, walisema wa zamani, Utanunua majoho, majumba na nyumbani, Umezitakasa roho, umekuwa mhisani, Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvinja mlima. Matajiri wanakujua, wema wako wameonja, Nguo zao umefua, wakupata kwa ujanja, Sura zao ‗mefufua, wanazuru kila njanja, Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima. Ndiwe mvunja mlima, onana na maskini, Watazame mayatima, kwao kumekua duni, Webebe waliokuwa, wainue walio chini, Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima. Ndiwe mvunja mlima, wapi kapata uwezo, Umezua uhasama, waja kupata mizozo, Ndiwe chanzo cha zahama, umewatia vikwazo, Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima. Umevunja usuhuba, familia zazozana, Waliokuwa mahabuba, kila mara wagombana, Roho zao umekaba, majumbani wachinjana, Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima. Nakutafuta kwa hamu, sabuni unirehemu, Sinilipue ja bomu, sije kawa marehemu, Niondoe jahanamu, ya ufukara wa simu, Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima. Naondoka wangu moyo, nikuitapo itika, Fulusi wacha uchoyo, tatua yalonifika, Nichekeshe kibogoyo, nami nipate kuwika, Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

    Date posted: October 1, 2019
  • Mstahiki Meya Jadili matumizi ya mbinu ya ishara katika tamthilia hii.

    Date posted: October 1, 2019
  • Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea imesheheni hali zinazotukia bila kutarajiwa. Fafanua.

    Date posted: October 1, 2019
  • Damu Nveusi na Hadithi nyingine "………Alimaliza kwa kuandika, "yajayo yapokee" (a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (b) Thibitisha ufaafu wa anwani ya hadithi hii.

    Date posted: October 1, 2019
  • Kidagaa kimemwozea "Alikuwa na kiu lakini si ya maji, kadhalika alikuwa na njaa lakini si ya chakula Habebeki mwanamume habebeki……." (a) Weka dondoo hili katika muktadha wake . (b) Eleza tamathali mbili zilizotumika katika dondoo hili. (c) Eleza aina za kiu na njaa zilizomkumba mrejelewa wa kwanza. (d) Mrejelewa wa pili alishindwa mtihani wa maisha. Jadili.

    Date posted: October 1, 2019
  • Tamthilia nzima ya Mstahiki Meya. "Duniani kuna watu na viatu" (a) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (b) Thibitisha ukweli wa kauli hii ukirejelea tamthilia nzima ya Mstahiki Meya.

    Date posted: October 1, 2019
  • Mwandishi wa tamthilia ya Mstahiki Meya ametumia wahusika kukuza kazi yake, Thibitisha kauii hili kwa kuwarejelea wahusika wafuatao. (i) Diwani wa tatu (ii) Bili (iii) Mhubiri (iv) Diwani I na II

    Date posted: October 1, 2019
  • Kila nikaapo hushika tama Na kuwazia hali inayonizunguka. Huyawazia madhila Huziwazia shida Huiwazia dhiki Dhiki ya ulezi Shida ya kudhalilishwa kazini. Madhila ya kufanyiwa dharau Kwa sababu ya jinsia ya kike. Hukaa na kujidadisi Hujidadisi kujua kwa nini Jamii haikisikii kilio changu Wenzangu hawanishiki mikono Bali wananidharau kwa kuukosoa utamaduni Hukaa na kujiuliza I wapi raha yangu uiimwengu huu? I wapi jamaa nzima ya wanawake? MASWALI (a) Shairi hili ni la aina. gani? Eleza (b) Eleza dhamira ya mtunzi wa shairi hili. (c) Kwa kutolea mifano eleza maana ya mistari mishata. (d) Taja na ueleze tamathali mbili zilizotumika katika shairi hili. (e) Tambulisha nafsi-neni katika shairi hili. (f) Fafanua toni ya shairi hili. (g) Fafanua maudhui mawili ya shairi hili. (h) Onyesha namna nafasi neni anavyosalitiwa. (i) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika shairi. (i) Madhila (ii) Kudhalilishwa.

    Date posted: October 1, 2019
  • Soma ushairi ufuatao kisha ujibu maswali. 1. Wasiwasi n‘ondokeya, ondoka enenda zako, Ondoka andama ndiya, nondosheya uso wako, Ondoka wanisikiya, ziwate jeuri zako, Jishughulishe na yako, yangu wayatakiyani? 2. Wasiwasi siitaki, suhuba yako si nzuri, Haistahamilikii, uovu umekithiri, Inganyoshwa hainyoki, ikukutene kikiri, Sikati yako shari, enda zako wasiwasi. 3. Huna kazi ufanyayo, ela kuwafitinisha, Viumbe na zao nyoyo, vitina kuwagotanisha, Hiino ndio kaziyo, yenye kukufurahisha, Ni kazi isiyokuchosha, mno umeizoeya. 4. Mara waja na habari, mambo yalivyo nyumbani, Ati mambo si mazuri, mambo yote tatashani, Wanitaka nifikiri, usemayo ni yakini, Nisononeke moyoni, upate kufurahika. 5. Au mara hunijiya, na kingine kisahani, Kuhusu zao afiya, hao waliyo nyumbani, Huwa husishi nambiya, hali zao taabani, Zingawa wakati gani? Ni zako au ni zao? 6. Na mara kuja mambiya, nitakapotoka humu, Na kwamba yaningojea, nde maisha magumu, Uliloni kusudiya, ni kunitiya wazimu, Kama ndiyo yako hamu, basi unshatahayari. (a) Eleza ujumbe uliojitokeza katika shairi hili. (b) Fafanua muundo wa ubeti wa tatu. (c) Eleza aina ya shairi hili. (d) Fafanua arudhi za utunzi alizozingatia mshairi. (e) Eleza toni ya mshairi. (f) Andika ubeti wa tano katika lugha ya kinathari. (g) Eleza mifano mitatu ya uhuru wa mshairi. (h) Eleza maana ya misamiati ifuatayokama ilivyotumika katika shairi. (i) ndiya (ii) kisahani (iii) nde

    Date posted: October 1, 2019
  • Soma ushairi ufuatao kisha ujibu maswali. 1. Ajaye kisimani mbele hunywa maji maenge, Asinywe yalo na vunju, Yakampa kigegezi, Yakamkibua roho akaona na kinyaa, Awali ndio awali, awali mbovu hamna. 2. Kiwa utalimatia. Utayaramba makombo, Utadata vitu cheche, Kisomo chenye dhamana kikakupa kisogo, Inajuzu ujihimu Mwanafuu darasani, Urauka po mapema, Katu hutayaramba makombo, Hutakosa kisebeho. 3. Dereva hata utingo, Natija ni asubuhi, Wateja utawawahi, Wasaa kuzingatia, Uwafikishe kazini, Kwa wasaa ufaao, Wasije wakateteshwa, Na bosi wao kazini, Nao wakakuapiza. 4. Na ewe mwanazaraa, Mpini uukamate, Kabla jua kuwaka sana, Majasho kutiririsha mwilini, Yang‘oe yote magugu, Kutoka kwa lako konde. 5. Mhadimu mwenye ajizi, Yakujuza ujihimu, Ununue na maziwa, Majogoo uyawahi mapema, Usije ukayadata, Chai mkandaa ukaandaa, Wateja wakuambae mithili ya ibilisi. Maswali (a) Eleza nasaha yoyote inayotolewa kwa wafanyakazi wowote watatu kwenye shairi. (b) Taja sifa zozote za kimuundo zilizotumiwa na mtunzi. (c) Eleza toni ya mshairi. (d) Nafsi nenewa anahimizwa kufanya nini. (e) Andika ubeti wa tatu kwa lugha tutumbi. (f) Toa mifano miwili ya uhuru wa mshairi. (g) Eleza maana ya misamiati ifuatayo kama ilivyotumiwa kwenye shairi. (i) Maji maenge (ii) Natija (iii) Majogoo

    Date posted: October 1, 2019
  • Kufariki kwa kitoto Uhuru ni jazanda inayoashiria hali halisi ya mambo riwayani "kidagaa kimemwozea". Jadili.

    Date posted: October 1, 2019
  • Onyesha jinsi ukatili unavyojitokeza kwa kurejelea hadithi zifuatazo. (i) Kanda la usufi (ii) Shaka ya mambo (iii) Mwana wa darubini (iv) Ndoa ya Samani.

    Date posted: October 1, 2019
  • Thibitisha jinsi anwani "Damu Nyeusi" inaafiki yaliyomo katika hadithi.

    Date posted: October 1, 2019