-
Tumia kiwakifishi kifuatacho kubainisha matumizi yake katika sentensi ili kutoa maana mbili tofauti.
Ritifaa
Date posted:
November 24, 2022
-
Tunga sentensi ukitumia viwakilishi vifuatavyo.
(i) Nafsi viambata
(II) Visisitizi
Date posted:
November 24, 2022
-
Geuza neno lililopigwa mstari kuwa kiwakilishi
Mtoto mbaya aliadhibiwa
Date posted:
November 24, 2022
-
Tunga sentensi mbili kuonyesha tofauti kati ya maneno haya.
(i) shuka
(ii) suka
Date posted:
November 24, 2022
-
Eleza maana ya misemo ifuatayo.
(i) kupiga domo
(ii) kupiga kijembe
Date posted:
November 24, 2022
-
Bainisha vitenzi halisi katika sentensi zifuatazo.
(i) Nyanchama hakufika mkutanoni
(ii) Horukut amerudi kutoka masoni
Date posted:
November 24, 2022
-
Onyesha nomino za jamii katika sentensi zifuatazo
(i) Chuki baina ya jamii lazima ikomeshwe barani Afrika.
(ii) Wageni watatumbuizwa na bengi ya kayamba Afrika.
Date posted:
November 24, 2022
-
Onyesha kundi nomino na kundi tenzi katika sentensi hii.
Nyayo za wanyama hao zimeonekana hapa.
Date posted:
November 24, 2022
-
Eleza tofauti kati ya:
(i) Mofimu huru
(ii) Mofimu tegemezi
Date posted:
November 24, 2022
-
Eleza tofauti kati ya sauti /z/ na /f/
Date posted:
November 24, 2022
-
Soma taarifa hii kisha ujibu maswali ifuatayo.
UKANDAJI
Je,unajua kuwa ukandaji wa mwili umetumika kama njia mojawapo ya matibabu toka jadi? Watu
wanaofahamika kutumia ukandaji kimatibabu toka jadi ni Wahindi,Wachina,Wagiriki,Warumi na Waafrika.
Ukandaji unajulikana kuwa na manufaa makubwa kimatibabu. Mathalani,ukandaji hufungua vitundu
vya ngozi. Ufunguzi huu huondoa sumu mwilini kupitia kwa utoaji jasho. Pili,ukandaji hupunguza mkazo wa
misuli. Misuli ikiwa na mkazo zaidi kwa muda mrefu huleta urundikaji wa asidi. Ukandaji huondoa asidi
hii,huufanya mwili kuwa mlegevu,humletea mtu uchangamfu na kuondoa uchovu.
Halikadhalika,ukandaji huimarisha mzunguko wa damu mwilini kwa wepesi. Hali hii huhakikisha kuwa
virutubishi vya mwili huweza kufikia viungo vyote vya mwili. Hili nalo huchangia kuzidisha uwezo wa mwili
kujikinga na maradhi. Hewa safi ya oksijeni huweza pia kusambaa kote mwilini kupitia kwa uimarishaji wa
mzunguko wa damu. Aidha,ukandaji wa taratibu na polepole hupunguza mkazo wa neva na kuziliwaza
ukandaji wa kasi huchangamsha neva na kuimarisha utendaji kazi wake.
Ukandaji unaweza kufanyiwa kiungo chochote mwili ni. Ukandaji huu huweza kuwa na matokeo
mbalimbali mwilini.
Mathalani,ukandaji wa njia ya chakula mwilini,hasa tumbo na utumbo,huimarisha usagaji wa chakula na
kuchangia uondoaji wa uchafu na sumu mwilini. Nao ukandaji wa njia ya mkonjo hustawisha uondoaji wa
chembechembe za sumu mwilini.
Kwa kawaida,viganja vya mikono hutumika katika ukandaji. Viungo hivi vinapaswa kuwa na wororo.
Wororo huu hupatikana kwa kutumia mafuta. Mafuta ambayo ni bora zaidi kwa shughuli za ukandaji ni ya
ufuta au simsim. Matumizi ya kitu chochote kama ungaunga kinachoweza kuziba vitundu vya ngozi
hayapendekezwi.
Ukandaji wapaswa kutekelezwa kwa njia ifuatayo. Mtu aanzie mikono na miguu. Kisha aingie kukanda
kifua,tumbo,mgongo na makalio. Hatimaye,akande uso na kichwa. Mtu anaweza kutumia kitambaa kukandia
mgongo. Ni bora kutumia viganja vya mikono kukandia. Kwa njia hii,manufaa huwa maradufu.
Kwanza,tutanufaika na ukandaji na wakati huo huo tutakuwa tukifanya mazoezi ya viungo. Wasioweza
kujikanda,wanaweza kuomba msaada. Ni muhimu ukandaji ufuatiwe na kuoga kwa maji vuguvugu.
Kwa walio na tatizo la shinikizo au mpumuko wa damu wanaweza kubadilisha utaratibu wa ukandaji.
Waanzie kichwani,kisha waelekee usoni,kifuani,tumboni,mgongoni,makalioni,miguuni na kuhitimisha
mikononi.
Hata hivyo,ukandaji haupaswi kufanywa wakati mtu anaugua maradhi yoyote. Wanawake wajawazito
nao wanatakiwa kuepuka ukandaji wa tumbo. Halikadhalika,ukandaji wa tumbo hauruhusiwi wakati mtu
anaendesha,ana vidonda vya tumbo au uvimbe tumboni. Hatimaye,ukandaji haupendekezwi iwapo mtu ana
maradhi ya ngozi.
MASWALI
(a) Ukandaji ni nini?
(b) Eleza manufaa matatu ya ukandaji.
(c) Ukandaji unatakiwa kutekelezwa kwa njia gani?
(d) Ukandaji unatakiwa kutekelezwa na nani na kwa nini?
(e) Onyesha ni lini ukandaji haupendekezwi.
(f) Eleza maneno yafuatayo kama yalivyotumika:
(i) ufunguzi
(ii) auni
(iii) maradufu
(iv) maji vuguvugu
(v) shinikizo la damu
Date posted:
November 23, 2022
-
Nani kuku....? Sosi poa leo .... Mate ndo! ndo! ndo!. Ukimanga hii hutaona daktari kwa miaka
kumi..... Ng’ombe je? nani? ......nani!... Ni wewe.... poa basi naja......
a. Je, sajili hii inapatikana wapi?
b. Huku ukitoa mifano mwafaka, eleza sifa nne za sajili hii.
Date posted:
November 22, 2022
-
Tunga sentensi moja kubainisha tofauti kati ya maneno haya:
Paka na baka
Date posted:
November 22, 2022
-
Akifisha sentensi ifuatayo:
mwalimu kazungu alimuuliza mwanafunzi je unataka kunidanganya kuwa ulifika shuleni mapema
Date posted:
November 22, 2022
-
Andika kinyume cha sentensi hii: Alipoinama nilifurahi.
Date posted:
November 22, 2022
-
Tia shadda ili kutoa maana mbili tofauti ya neno ‘katakata’.
Date posted:
November 22, 2022
-
Huku ukitoa mifano mwafaka, eleza maana ya aina zifuatazo za silabi:
Silabi funge
Silabi wazi
Silabi mwambatano
Date posted:
November 22, 2022
-
Neno ‘chungu’ lina maana –enye kutokuwa na tamu. Eleza maana zake zingine mbili.
Date posted:
November 22, 2022
-
Andika matumizi mawili ya mshazari.
Date posted:
November 22, 2022
-
Andika katika ukubwa.
Mwanamwali huyu alijinunulia viatu vya ngozi.
Date posted:
November 22, 2022
-
Weka Nomino hizi katika ngeli zake.
Raha
Kumbikumbi
Date posted:
November 22, 2022
-
Akifisha sentensi hii:
alikufa siku ya jumapili tarehe 20 mwezi wa januari mwaka wa 2011.
Date posted:
November 22, 2022
-
Kwa kutoa mifano mwafaka, onyesha mianzo tofauti katika ngeli ya U-ZI.
Date posted:
November 22, 2022
-
Andika vigezo vitatu vinavyotumiwa kuainisha irabu.
Date posted:
November 22, 2022
-
Soma makala yafuatayo kasha ujibu maswali
Ajali haina kinga. Watu wengi wanapotajiwa neno ajali, fikira zao hukimbilia moja kwa moja hadi
barabarani. Mara chachemawazo yao huenda viwandani, mashambani au kwenye viwanja vya
michezo. Ni nadra sana watu kufikiraia kuwa nyumbani ndiko ajali nyingi zinztokea.
Idadi kubwa ya ajali nyumbani hutokea kimchezo tu. Watu wengi wameteleza msalani na wanapata
majeraha mabaya. Wengine wameteleza walipokanyaga vitu vyenye unyevu sakafuni, kama vile
mafuta, mabaki ya chakula au hata maganda ya ndizi. Ulemavu walio nao watoto na hata watu
wazima hutokana na ajali kama hizi wasizofikiria wtu wengi.
Ajali vilevile hutokea watu wanapozama katika shughuli au kupata jazba kuu ya kutenda. Katika hali
hii, huweza kujiumiza au kuwaumiza wengine bila kujua.
Hapa tunazungumzia watu ambao hujaribu kubebe mizigo yenye uzani wasiokadiria. Madhara huwa
kuteguka viungo na kuchanika misuli. Aghalabu hulemewa na kubanwa. Mwandishi wa makala haya
siku moja alipanda kibao kuangika picha ukutani. Ingawa alikuwa mfupi, ari ilimsukuma
kuchuchumia. Matokeo ni kibao kilijisukuma nyuma. Mhusika alianguka akajigonga kidevu. Kitendo
hiki kilisababisha yeye kujiuma ulimi vibaya. Kuvunjika jino na hata kuzirai. Bahati ni kuwa alikuwepo
mtu aliyempa huduma ya kwanza na kumkimbiza hospitalini.
Hat hivyo ajali nyingi hutokana na vifaa vya nyumbani. Zana hizi ni pamoja na visu, meko ya gesi,
mashine zinazotumia umeme na kadhalika na huwa hatari sana, hasa kwa watoto. Kitu kidogo hata
kama wembe huweza kusababisha madhara makubwa. Kwa hakika hakuna yeyote kati yetu, hata
waliokulia katika makasri ya fahari asiye na kovu. Makovu haya ambayo tunayaficha katika mavazi
yetu ni ishara ya majeraha kutokana na ajali nyumbani. Je una kovu lolote?
Unakumbuka ulivyolipata?
Ingawa ajali hizi haziepukiki, yawezekana kuzipunguza. Ni muhimu kukuza tabia na mazoea ya kuwa
waangalifu nyumbani. Kwa mfano, ni hatari kuepua chungu chenye maji yanayotokota mekoni kwa
mikono mitupu. Aidha ni kutowajibika kuchanganya kitu chochote chenye unyevu na mafuta moto
mekoni. Watu wengi wamebambuka ngozi na nyumba kuteketea kwa namna hii. Kwa hivyo ni vizuri
kupata ujuzi wa jinsi ya kutumia vifaa na kuhakikisha tunavirudisha ipasavyo.
Jambo la tatu na muhimu zaidi ni kuwepo kwa vifaa pamoja na uwezo wa kutoa huduma ya kwanza.
Inawezekana kuokoa maisha au kuounguza majeraha kwa kuchukua hatua za dharura.
Maswali
1. Eleza maana ya methali ‘Ajali haina kinga’
2. Kwa nini mwandishi anasema ajali nyumbani hutokea kimchezo?
3. Ni mambo gani mengine yanayosababisha ajali nyumbani?
4. Onyesha vile invyowezekana kupunguza ajali nyumbani.
5. Eleza maana ya:
(i) Jazba
(ii) Makasri
(iii) Makovu
(iv) Kuepua
Date posted:
November 22, 2022
-
Fafanua dhima tano za fasihi simulizi katika jamii yako.
Date posted:
November 22, 2022
-
Sanaa ni nini?
Date posted:
November 22, 2022
-
Taja majukumu mawili ya lugha rasmi.
Date posted:
November 22, 2022
-
Taja sifa mbili za lugha ya kitaifa.
Date posted:
November 22, 2022
-
Eleza sifa tatu za sajili ya hospitali.
Date posted:
November 22, 2022