Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Turkana District Mock-Kiswahili Paper 3 Question Paper

Turkana District Mock-Kiswahili Paper 3 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2006



102/3
KISWAHILI
KARATASI YA 3
FASIHI YA KISWAHILI
MUDA: SAA 1 ½
WILAYA YA TURKANA BARAZA LA MITIHANI- 2006
Hati Ya Kuhitimu Kisomo Cha Sekondari (K.C.S.E.)
102/3
KISWAHILI
KARATASI 3 –
FASIHI YA KISWAHILI
MUDA: SAA 1 ½
_ Jibu maswali manne pekee.
_ Swali la kwanza ni la lazima
_ Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki yaani;
tamthilia, riwaya, hadithi fupi na fasihi simulizi.
_ Usijibu maswali mawili kutoka katika sehemu moja.
Maagizo2
Karatasi hii ina kurasa 4 zilizopigwa chapa
Watahiniwa wanastahili kuona kuwa maswali yote yako na hakuna yaliyooachwa.
1. USHAIRI:
Soma shairi lifuatalo na kisha ujibu maswali yafuatayo.
UKUBWA JAA
Dunia yetu dunia, watu wanakufitini,
Dunia huna udhia, watu wanakulaani,
Dunia huna hatia, wabebeshwa kila zani,
Dunia unaonewa, umetenda kosa gani!
Dunia umenyamaza, umetua kwa makini,
Dunia vitu mejaza, watu wanataka nini?
Dunia wanakucheza,binadamu maluuni,
Dunia unaonewa, umetenda kosa gani!
Dunia mtu akose, hukutia mdomoni,
Dunia hebu waase, hao watu mafatani,
Dunia chuki mpuse, muipate afueni,
Dunia unaonewa, umetenda kosa gani!
Dunia una lawama, za uongo si yakini,
Dunia wanokusema, ni manjunju si razini,
Dunia huna hasama, waja ndio kisirani,
Dunia unaonewa, umetenda kosa gani!
Dunia kuharibika, hayo amezusha nani?
Dunia watu humaka, hao wanokuhini,
Dunia umejazika, kila tunu ya thamani,
Dunia unaonewa, umetenda kosa gani!
Dunia unatukisha, bwerere bila undani,
Dunia unatukosha, maji tele baharini,
Dunia unaotehsa, mimea tosha shambani,
Dunia unaonewa, umetenda kosa gani!
Dunia hujageuka, tangu umbwe na manani
Dunia watu ndo, nyoka, mahaini na wahuni

3
Dunia una baraka, mwenye pupa hazioni
Dunia huna ubaya, wabaya ni insani.
Maswali:
(a) Shairi hili ni la bahari gani? Toa sababu yako. (alama 3)
(b) (i) Kichwa cha shairi hili kinaoanaje na maudhui ya shairi?. (alama 2)
(ii) Andika methali moja inayoeleza maudhui ya shairi hili. (alama 3)
© Eleza sifa tatu za wanadamu kama anavyoeleza mshairi. (alama 3)
(d)Kwa kutoa mifano kutokana na shairi hili, eleza mbinu tatu za lugha alizotumia
mshairi. (alama 6)
(e) Eleza maana ya vifungu vifuatavyo vya maneno kama vilivyotumika katika shairi.
(i) bwerere bila undani
(ii) hao watu mafatani
(iii) afueni
(iv) insani (alama 4)
TAMTHILIA
KIFO KISAMINI: Ithaka Wa Mberia
2. "Ukombozi sio lelemama." Dhihirisha ukweli wa kauli hii kufuatana na yaliyomo kwenye
tamthilia ya "Kifo Kisimani" (alama 20)
3. "Kwa ushirikiano. Kwa njia ya nipe nikupe. Mtemi yuko tayari kumsamehe, iwapo atakubali
hadharani kwamba ataacha uchochezi wake."
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 6)
(b) Eleza sifa za anayetarajiwa kumsamehe mzungumziwa. (alama 12)
(c) Ni nini hatima ya anayezungumziwa (alama 2)
RIWAYA
MWISHO WA KOSA: Z. Burhani:
4. Riwaya ya "Mwisho wa kosa" imejaa migogoro.
Fafanua kauli hii kwa kutoa mifano mwafaka (alama 20)
5. Anwani ya riwaya ya "Mwisho wa Kosa" ni anwani mwafaka. Jadili (alama 20)
HADITHI FUPI
MAYAI WAZIRI WA MARADHI NA HADITHI NYINGINE
6. Ukirejelea hadithi ya 'Uteuzi wa moyoni' - Rayya
Timammy, jadili ujumbe unaoibuka katika jamii inayozungumziwa. (alama 20)
FASIHI SIMULIZI
7. (a) Taja vipera vine vya tanzu fupi na utoe mfano mmoja kwa kila tanzu. (alama 8)
(b)Methali zifuatazo zimetumia tamathali gani za usemi na kwa nini?
(i) Jambo usilojua ni kama usiku wa giza. (alama 2)
(ii) Mgeni ni kuku mweupe. (alama 2)
(iii) Hawi Musa kwa kuchukua fimbo. (alama 2)
(iv) Kiburi si muungwana. (alama 2)
( c) Nini maana ya nahau zifuatazo
(i) Ana jicho la nje. (alama 1)
(ii) Yeye ni jamvi la wageni. (alama 1)
(iii) Mkono birika (alama 1)
(iv) Mfua uji (alama 1)






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers