Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Kakamega East District Mock - Kiswahili Paper 2 Question Paper

Kakamega East District Mock - Kiswahili Paper 2 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2011

Jina: …………………………………………………………………… Nambari: ………...………
Sahihi ................................................................................ Tarehe: ………….....................................
102/2
KISWAHILI
LUGHA
KARATASI YA 2
JULAI/ AGOSTI 2011
MUDA: SAA 2 ½
Hati ya kuhitimu kisomo cha sekondari Kenya (K.C.S.E)
Kiswahili
Lugha
MAAGIZO
• Andika Jina lako na Namba yako katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
• Weka sahihi yako na tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa
• Jibu maswali yote.
• Majibu yaandikwe katika nafasi zilizoachwa wazi katika kijitabu hiki cha maswali.
Karatasi hii ina kurasa 10 zilizopigwa chapa. Watahiniwa ni lazima waangalie kama kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na
kuwa maswali yote yamo.
1. UFAIIAMU
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
Huku ulimwengu unapoingia katika teknolojia ya tarakilishi na sera ya utandaridhi, ukweli
wa mambo ni kuwa akina mama wamezinduka. Suala la usawa wa kijinsia limeanza kushamiri kote
duniani na ole wake mwanamume yeyote ambaye hajawa tayari kutembea na majira. Lakini hebu
tuchunguze jambo hili kwa makini zaidi.
Usawa wa jinsia ni nini? Usawa wa kijinsia ni usawa wa binadamu wote; wawe wake au
waume. Usawa huu unapaswa kudhihirika katika kugawa nafasi za kazi, utoaji wa elimu, nafasi za uongozi na nyanja nyinginezo zozote za maisha.
Ubaguzi wa aina yoyote ile hasa dhidi ya mwanamke ni jambo linalokabiliwa na vita vikali
sana ulimwenguni kote.
Dahari na dahari, hasa katika jamii za kiafrika, kumekuwa na imani isiyotingisika kuwa
mwanamke ni kiumbe duni akilinganishwa na mwanaume. Kwa hivyo mwanamke amekuwa
akifanyiwa kila aina ya dhuluma ikiwepo kupigwa, kutukanwa, kudharauliwa, kunyimwa haki zake, kunyimwa heshima na mambo kama hayo. Lakini je, ni kweli kuwa mwanamke ni kiumbe duni
asiyefaa kutendewa haki?
Tukichunguza jamii kwa makini tunaweza kuona mara moja kuwa hiyo ni imani potofu isiyo
na mashiko yoyote. Ukiimulika familia yoyote ile iliyopiga hatua kimaendeleo, uwezekano mkubwa ni kuwa mume na mke wa familia inayohusika wana ushirikiano mkubwa. Mume anamthamini mke wake na hadiriki kufanya maamuzi muhimu yanayoweza kuathiri maendeleo ya familia bila kumhusisha mke. Mume kama huyu huketi na mkewe, wakishauriana na kufikia uamuzi bora.
Tukitoka katika muktadha wa kifamilia na kumulika ulimwengu wa kazi iwe ni katika afisi za
kiserikali au kwenye makampuni binafsi, ukweli ni kwamba kiongozi yeyote yule aliyefaulu katika usimamizi wake mara nyingi huwa na mke nyumbani ambaye wanashauriana kila uchao kuhusu kazi anayofanya hata kama mke hafanyi kazi mahali pale. Hisia na mawaidha anayotoa mke kwa mume wake ni tunu na huenda asiyapate kwingineko kokote hata katika vitabu vya kupigiwa mifano. Hii ni mojawapo ya sababu ambayo huwafanya viongozi wa nchi mbalimbali kupenda sana kuwatambulisha wake na familia zao waziwazi kwa vile wanajua kuwa jamii inathamini sana msingi wa jamii. Kiongozi ambaye hana mke au familia au yule ambaye mke wake hatambulikani, hutiliwa mashaka na jamii hata kama kiongozi huyu ana hulka ya uongozi. Jamii inaamini kuwa mke ni johari kwa mume wake hasa yule aliye na azma ya kushikilia kazi ngumu ya kuongoza umma.
Tukirudi nyuma kidogo na kupiga darubini mataifa ya mbali, tunaweza kuwaona wanawake
mashuhuri waliotoa uongozi ambao hadi waleo unapigiwa mfano. Wanawake hao walisimamia mojawapo ya mataifa yenye uwezo na ushawishi mkubwa zaidi duniani. Ingawa wengi wao sasa
wemeng’atuka, uongozi wao bado unakumbukwa hata baada ya miaka mingi ya wao kuamua
kupumzika. Mifano ni kama: Bi Margaret Thatcher aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza, Bi
Bandranaike wa Sri Lanka, Golda Meir wa Israeli na wengine wengi katika mataifa kama Indonesia, Ufilipino, Bangladesh, Pakistani na kwingineko.
Katika kufikia tamati, tunapozungumza kuhusu jinsia, hatuna budi kugusia kitafsili masuala
nyeti. Kwanza, imani ya kushikilia ki ki ki tamaduni zisizofaa, ni jambo linalofaa kuchunguzwa kwa makini. Kwa mfano, kuna baadhi ya jamii ambazo humlazimu mke kurithiwa baada ya kifo cha mumewe. Vile vile baadhi ya jamii za kiafrika zinashikilia kuwa mwanamke hana haki ya kurithi.
Kutokana na imani hii, wanawake wengi huishi maisha ya taabu baada ya kutengana na waume zao kwa vile hawana haki ya kurithi chochote kutoka kwa wazazi wao hata kama wazazi hao wana mali nyingi kupindukia. Mali ya wazazi ni haki ya watoto wa kiume wala si watoto wa kike! Hili ni jambo la kusikitisha mno. Isitoshe, wanawake hukumbwa na kizingiti kingine wanapojaribu kumiliki mali ya waume zao baada ya waume hao kukata kamba. Sababu ni kuwa, baada ya hao wenda zao
kuwekwa kaburini, vita vya umiliki wa mali huanza mara moja na mwishowe yule mke maskini
hujikuta hana hata mahali pa kulala sembuse mali waliyochuma na mumewe. Hatimaye mke hujikuta matatizoni anapoamriwa kufunganya virago na mali yake yote kunyakuliwa na aila ya mumewe.
Jambo hili linaonyesha namna tulivyoachwa nyuma na uhalisia wa mambo. Ni lazima jamii izinduke na itoke kwenye kiza hiki chenye maki nzito.
MASWALI
(a) Ni kwa vipi ambavyo vita dhidi ya ubaguzi vimepiga hatua, hasa dhidi ya wanawake. (ala.3)
………………………………………………………………………………………………..…..…
.………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………..…..…
.………………………………………………………………………………………………………
(b) Ina maana gani kusema .. “familia yoyote ile iliyopiga hatua kimaendeleo...” (ala.2)
………………………………………………………………………………………………..…..…
.………………………………………………………………………………………………………
(c) Mwanamke ni johari kwa mume wake. Dhibitisha dai hili kwa mujibu wa ufahamu. (ala.3)
………………………………………………………………………………………………..…..…
.………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………..…..…
.………………………………………………………………………………………………………
(d) Ni mambo gani yanayoweza kuonyesha kuwa wanaume katika baadhi ya jamii hawatembei na
majira. (ala.4)
………………………………………………………………………………………………..…..…
.………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………..…..…
.………………………………………………………………………………………………………
(e) Eleza maana ya maneno yafuatayo jinsi yalivyotumiwa katika muktadha. (ala.3)
(i) Kushamiri
………………………………………………………………………………………………..…..…
.………………………………………………………………………………………………………
(ii) Hulka
………………………………………………………………………………………………..…..…
.………………………………………………………………………………………………………
(iii) Azma
………………………………………………………………………………………………..…..…
.………………………………………………………………………………………………………
2. UFUPISHO (ALAMA 15)
Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, kumekuwa na mfumko wa bei ya bidhaa muhimu hivi
kwamba idadi kubwa ya raia wanalala njaa. Uchunguzi uliofanywa na mashirika ya kijamii kuhusu bei ya bidhaa hizo umeonyesha kuwa familia za kawaida zinatumia nusu ya mapato yao kununua chakula. Bila shaka yoyote, hili ni janga linaloendelea kutokota. Tunafahamu kuwa kupanda kwa bei ya petroli kimataifa kumechangia kuongezeka kwa bei hiyo ya vyakula, kwa namna moja au nyingine.
Mbali na vyakula, gharama ya kupangisha nyumba, maji, stima na mafuta imepanda kwa muda wa
miezi mitatu iliyopita kati ya Disemba na Januari 2011. Kwa mujibu wa Benki ya dunia
iliyozinduliwa hivi majuzi, kupanda kwa bei ya vyakula kumesukuma familia nyingi katika lindi la umaskini.
Ingawa serikali haina uwezo wa kuthibiti baadhi ya sababu zinazochochea kuongezeka kwa bei ya vyakula nchini, haipaswi kutulia tuli ikisubiri suluhisho litokee kisadfa. Inasikitisha kwamba viongozi wetu wanatumia muda mwingi kuchapa siasa huku raia wa kawaida wakiendelea kuumia.
Iweje basi kwamba katika vikao vyao vya hadhara wanasiasa wanatumia muda mwingi kuzungumzia
maswala ya kugawana wananchi na kufichua njama za kuwaangamiza wapinzani wao badala ya
kueleza namna watakavyokabiliana na janga lililopo la njaa. Ni lini watafahamu kwamba hauwezi kumtawala mtu mwenye njaa?
Kwa muda mrefu, baa la njaa limekuwa likihusishwa na maeneo ya Kaskazini mwa nchi yetu; lakini kama uchunguzi ulivyoonyesha, familia nyingi nchini zinaumia na wengi hawawezi kumudu bei ya bidhaa muhimu kama sukari, unga, mafuta ya kupikia na kadhalika.
Wakati umewadia kwa serikali kuchukua hatua madhubuti kwa kuwa, kama ilivyo, ni vigumu
kumtawala mtu aliye na tumbo tupu na ambaye hajijui wala hajitambui kuhusu atakakopata lishe.
MASWALI
(a) Ukizingatia taarifa uliyosoma, fafanua athari za mfumko wa bei kwa wananchi. (al. 4)
(Maneno 35)
Matayarisho
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………..…
Nakala safi

(b) Eleza mambo muhimu anayoyazungumzia mwandishi katika aya za mwisho nne
(Maneno 55-60) (ala.8)
Matayarisho
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………..…
..……………………………………………………………………………………………………………
Nakala safi
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………..…
..……………………………………………………………………………………………………………
3. SEHEMU YA 3: MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
(a) Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya visanduku. (al.4)
Abiria waliojeruhiwa walipelekwa hospitalini.
…………………………………………………………………………………….……………..……
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………..…………..…
…………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………..……………..……
(b) Tambua sifa mbili bainifu za sauti zifuatazo. (al.4)
/dh/
……………….………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………..……
/ch/
……………….………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………..……
(c) Tunga sentensi ukitumia kihusishi cha;
(i) Hali (al.1)
……………….………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………..……
(ii) Ulinganisho (al.1)
……………….………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………..……
d) Tambua aina za sentensi zifuatazo. (al.2)
(i) Kondoo aliyekata kamba ni wa mkulima yule.
……………….………………………………………………………………………………………
(ii) Alikuja jioni lakini hakunipata.
……………….………………………………………………………………………………………
(e) Andika kwa wingi:
Ukumbi ulipambwa ukapambika. (al.1)
……………….………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………..……
(f) Tambua yambwa katika sentensi ifuatayo: (al. 3)
Wazazi wanawalipia karo watoto kwa hundi.
……………….………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………..……
……………….………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………..……
(g) Eleza matumizi ya alama zifuatazo: (al.2)
(i) Ritifaa
……………….………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………..……
(ii) Kistari kifupi
……………….………………………………………………………………………………………
(h) Tunga sentensi mbili zinazotumia neno halafu kama: (al.2)
(i) Kielezi
……………….………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………..……
(ii) Kiunganishi
……………….………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………..…
(i) Andika kwa usemi wa taarifa. (al.3)
Mamboleo alilia, “Marafiki zangu, majambazi wamenipiga na kunipora pesa zangu zote. Hali
yangu sasa ni mbaya”.
……………….………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………..……
(j) Andika sentensi ifuatayo katika ukubwa kisha wingi. (al.2)
Kitoto hiki hakitosheki na maziwa, kinapenda kulia.
……………….………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………..……
……………….………………………………………………………………………………………
(k) Tunga sentensi tatu kuonyesha maana tatu tofauti za neno taka. (al.3)
……………….………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………..……
……………….………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………..……
(l) Onyesha kirai katika sentensi ifuatayo na ueleze ni cha aina gani. (al.2)
Watoto wa kike hudunishwa katika jamii nyingi
……………….………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………..……
……………….………………………………………………………………………………………
(m) Bainisha matumizi mawili ya kiambishi ka katika sentensi. (al.2)
……………….………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………..……
(n) Tunga sentensi ukitumia kitenzi pa katika hali ya kutendeka. (al.2)
……………….………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………..……
(o) Andika kinyume cha kitenzi kilichopigiwa mstari. (al.1)
Alikashifiwa kwa kazi aliyofanya.
……………….………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………..…
(p) Kanusha sentensi (al.1)
Kuliko na kiangazi kwahitaji msaada.
……………….………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………..……
(q) Andika viwakilishi vya ngeli vya nomino zifuatazo; (al.2)
(i) Amri (umoja)
……………….………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………..……
(ii) Kwetu
……………….………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………..……
(r) Unda vitenzi kutokana na maneno yafuatayo (al.2)
(i) Dhuluma
……………….………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………..……
(ii) Maskini
……………….………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………..……
4. ISIMU JAMII (ALAMA 10)
Huku ukitoa mifano mwafaka, onyesha sifa tano za sajili katika muktadha wa utaalamu. (al.10)
……………….………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………..……
……………….………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………..……

More Question Papers

Popular Exams

Return to Question Papers