Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Butere District Mock- Kiswahili Paper 2 Question Paper

Butere District Mock- Kiswahili Paper 2 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2008



Jina: . ………………………………………………… Nambari:…………………………
Shule. ……………………………………….…………
102/2
KISWAHILI
LUGHA
KARATASI YA PILI
Julai / Agosti 2008
MUDA: SAA 2 ½
MTIHANI WA MWIGO WILAYA YA BUTERE - 2008
Cheti Cha Kuhitimu Kisomo Cha Sekondari Kenya (K.C.S.E)
102/2
KISWAHILI
LUGHA
KARATASI YA PILI
Julai / Agosti 2008
MUDA: SAA 2 ½
MAAGIZO KWA WATAHINIWA
• Jibu maswali yote
• Majibu yako yaandikwe katika nafasi zilizoachwa wazi katika kijitabu hiki.
Karatasi hii ina kurasa 10 zilizopigwa chapa
Watahiniwa lazima wahakikishe kurasa zote zimepigwa chapa sawa sawa na kuwa maswali yote yamo.
SEHEMU YA A: UFAHAMU (ALAMA 15)
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
Ajali haina kinga. Watu wengi wanapotajiwa neno ajali, fikira zao hukimbilia moja kwa moja hadi barabarani. Mara chache mawazo yao huenda viwandani, mashambani au kwenye viwanja vya
mchezo. Ni nadra sana watu kufikiria kuwa nyumbani ndiko ajali nyingi zinatokea.
Idadi kubwa ya ajali nyumbani hutokea kimchezo tu. Watu wengi wameteleza msalani na wakapata majeraha mabaya. Wengine wameteleza walipokanyaga vitu vyenye unyevu sakafuni, kama vile mafuta, mabaki ya chakula au hata maganda ya ndizi. Ulemavu walio nao watoto na hata watu wazima hutokana na ajali kama hizi wasiozifikiria watu wengi.
Ajali vilevile hutokea watu wanapozama katika shughuli au kupata jazba kuu ya kutenda. Katika hali hii, huweza kujiumiza au kuwaumiza weingine bila kujua. Hapa tunazungumzia watu ambao hujaribu kubeba mzigo wenye uzani wasioukadiria. Madhara huwa kuteguka viungo na kuchanika misuli.
Aghalabu hulemewa na kubanwa. Mwandishi wa makala haya siku moja alipanda kibao kuangika
picha ukutani. Ingawa alikuwa mfupi, ari ilimsukuma kuchuchumia. Matokeo ni kibao kilijisukuma nyuma. Mhusika alianguka akajigonga kidevu. Kitendo hiki kilisababisha yeye kujiuma ulimi vibaya,kuvunjika jino na hata kuzirai. Kwa bahati alikuwepo mtu aliyempa huduma ya kwanza na kumkimbiza hospitalini Hata hivyo ajali nyingi hutokana na vifaa vya nyumbani. Zana hizi ni pamoja na visu, meko ya gesi,mashine zinazotumia umeme, na kadhalika na huwa hatari sana, hasa kwa watoto. Kitu kidogo hata kama wembe huweza kusababisha madhara makubwa. Kwa hakika hakuna yeyote kati yetu, hata waliokulia katika makasri ya kifahari asiye na kovu. Makovu haya ambayo tunayaficha katika mavazi yetu ni ishara ya majeraha kutokana na ajali nyumbani. Je, una kovu lolote? Unakumbuka ulivyolipata?
Ingawa ajali hizi haziepukiki, yawezekana kuzipunguza. Ni muhimu kukuza tabia na mazoea ya kuwa waangalifu nyumbani. Kwa mfano, ni hatari kuepua chungu chenye maji yanayotokota mekoni kwa mikono mitupu. Aidha ni kutowajibika kuchanganya kitu chochote chenye unyevu na mafuta moto mekoni. Watu wengi wamebambuka ngozi na nyumba kuteketea kwa namna hii. Kwa hivyo ni vizuri kupata ujuzi wa jinsi ya kutumia vifaa na kuhakikisha tunavitumia ipasavyo. Jambo la tatu na muhimu zaidi ni kuwepo kwa vifaa na kubakisha pamoja na uwezo wa kutoa huduma ya kwanza.
Inawezekana kuokoa maisha au kupunguza majeraha kwa kuchukua hatua za dharura.
Maswali
1. Eleza maana ya methali ‘Ajali haina kinga’. (alama 2)
2. Kwa nini mwandishi anasema ajali nyumbani hutokea kimchezo? (alama 3)
3. Ni mambo gani mengine yanayosababisha ajali nyumbani? (alama 3)
4. Onyesha vile inavyowezekana kupunguza ajali nyumbani. (alama 3)
5. Eleza mana ya: (alama 4)
(i) Jazba
(ii) Makasri
(iii) Makovu
(iv) Kuepua
2. MUHTASARI (alama 15)
Soma makala ifuatayo kisha ujibu maswali
Nchi nyingi za ulimwengu wa tatu huathirika na biashara ya kimataifa.Biashara hiyo inaweza kuwa inafanywa kwa uagizaji ama uuzaji wa bidhaa za nchi nyingine.
Biashara ya kimataifa ina umuhimu mkubwa.Kwanza inawezesha nchi kupata bidhaa ambazo haitengenezi mbali na kusaidia kuwepo na uhusiano kati ya nchi mbalimbali.Uhusiano huu huiwezesha nchi kupata bidhaa kwa bei rahisi kuliko ambavyo ingekuwa kama zingetengenezwa kwao,hasa ikiwa nchi inayohusika haina malighafi yanayohusika katika utengenezaji wa bidhaa hizo.Pia husaidia wakati nchi imekubwa na dharura au majanga kwani itaauniwa na nchi nyingine ingawa hali kama hii haihakikishwi.ushirikiano huu vilevile huchochea upatikanaji wa nafasi za kazi kwa wengi.
Kwa sababu za kushughulikia utengenezaji wa bidhaa na utoaji huduma nyingine kutokana na uzoefu wa muda mrefu na kuwepo raslimali,nchi huwa na uzoefu fulani.Ni kwa sababu hii nchi inawezeshwa kupata pesa za kigeni na kuuza bidhaa za ziada.
Hata hivyo, kuna matatizo yanayozikumba nchi za kiafrika katika biashara hii.Kwanza, biashara ya aina hii hutatiza viwanda vichanga katika nchi zinazoendelea kwa ushindani usio sawa. Ajabu ni kwamba nchi zilizoendelea zimetumia biashara hii 'kutupa' bidhaa za hali ya chini ama zenye athari kwa hali za kijamii.Urafiki haukosi.Ikiwa nchi inaitegemea uagizaji wa bidhaa,haitaweza kuikosea ama kuhitilafiana na nchi ambayo inategemea,hivyo kuathiri uhuru wa nchi kama hiyo.
Hata hivyo, nchi mbalimbali zimeweka mikakati ya kulinda viwanda vichanga kutokana na athari ya biashara kama hii.
Baadhi zimeweka ushuru wa juu kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje kwa wasio washirika wa kibiashara.Licha ya hayo,baadhi ya bidhaa zinazonuiwa kwa nje kwa matumizi ya kielimu,utafiti wa kisayansi na bidhaa za maonyesho huagizwa bila ushuru.huo. Wakati mwingine ni banki kuu ndiyo hutoa leseni kwa niaba ya serikali kama njia ya kudhibiti bidhaa kutoka nje.Njia nyingine ya kuvisaidia viwanda nchini ni kuuza bidhaa kwa njia ya kuvipunguzia ushuru,usafirishaji nafuu na kuvipa ushuru.
Serikali nyingine huhakikisha kuwa ni bidhaa kiasi fulani tu ambazo zinaweza kuangizwa kwa kipindi fulani. Kwa mfano, kuna idadi fulani ya magari kutoka nje yanayoweza kuagizwa kuja Kenya kwa mwaka mmoja.Hata hivyo, wakati mwingine, serikali husitisha uagizaji wa bidhaa kama vile dawa, sinema, maandishi ya kisiasa na vitabu kutoka nje;bidhaa
ambazo zinachukuliwa kuwa hatari kwa nchi.
a) Fafanua mambo yote muhimu yanayozungumziwa katika aya za kwanza tatu.
(alama 7) Maneno 60 – 70
(1 ½ ya mtiririko)
Nakala chafu
……………………………………………………………………………………………………………
Nakala safi.
……………………………………………………………………………………………………………
b) Fupisha aya za mwisho mbili bila kubadilisha maana aliyokusudia mwandishi (alama 5)
maneno 50. (alama 1 ½ ya mtiririko
Nakala chafu
……………………………………………………………………………………………………………
Nakala safi
……………………………………………………………………………………………………………
3 MATUMIZI YA LUGHA
a) Onyesha ngeli husika kwa kila nomino zifuatazo kisha utungie sentensi moja moja (alama 4)
i) Kinyozi
Sentensi
……………………………………………………………………………………………………
ii) Kuimba.
Sentensi....
b ) Neno kijana linaweza kutumika kama kivumishi au Kielezi. .Tunga sentensi kudhihirisha
haya. (alama 2)
i) Kivumishi
……………………………………………………………………………………………………
ii) Kielezi
……………………………………………………………………………………………………
c) Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli zilizoonyeshwa mabanoni. (alama 2)
i)_fa(tendeana).
……………………………………………………………………………………………………
ii) _nywa(kutendeka)
……………………………………………………………………………………………………
d) Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia mishale (alama 4)
Watoto wanacheza vizuri ilhali wazazi wakorofi wanawabeza vikali sana
……………………………………………………………………………………………………
e) Tumia alama zifuatazo kuakifisha katika sentensi kudhihirisha matumizi yake (alama 2)
(i) Mshazari
……………………………………………………………………………………………………
ii) parandesi
……………………………………………………………………………………………………
f) Tunga sentensi kuonyesha maana ya maneno haya. (alama 2)
(i) chana
……………………………………………………………………………………………………
ii)jana
……………………………………………………………………………………………………
g)Sahihisha sentensi zifuatazo (alama2)
i) Mwanafunzi ambaye aliyecheza vizuri ni huyu
……………………………………………………………………………………………………
ii)Pahali alikoingia ni humu ndani
……………………………………………………………………………………………………
h) Kanusha (alama 2)
i) Ukicheza utaadhibiwa vikali
……………………………………………………………………………………………………
ii)Juma amecheza na kukinai
……………………………………………………………………………………………………
I) Andika katika usemi wa taarifa (alama 3)
"Nitaleta kitabu hiki kesho iwapo utakuwepo" Maria alimwambia rafikiye.
……………………………………………………………………………………………………
j) Kamilisha methali ifuatayo kisha ueleze matumizi yake (alama 3)
Mla nawe hafi nawe …………………………………………………………………………….
k) Unda majina mawili mawili kutokana na maneno yafuatayo (alama 4)
safari - ............................... ........................................
rithi - ............................... .......................................
faraja - ............................ ........................................
ogopa - ........................... .......................................
I) Tumia viunganishi vifuatavyo katika sentensi (alama2)
i) almradi
ii)japo
m) Bainisha viwakilishi nafsi viambata katika sentensi hii (alama 2)
Aliwapiga wanafunzi watundu na wakatoroka
n)Bainisha aina ya vitenzi katika sentensi hizi (alama 2)
i) Mama alikuwa akienda kwake usiku
ii)Huyu ni dereva mzuri
o) Sentensi hizi ni za aina gani? (alama 2)
q i) Mkulima aliyekata rufani atasaidiwa kesho...........................................................................
ii)Walimu na wazazi watajenga bweni .......................................................................................
p)Onyesha kishazi huru na kishazi tegemezi katika sentensi hii
i) Jiwe lililomgonga limeondolewa (alama 2
4. ISIMUJAMII
"Timu yetu iliweza kuichabanga Simba F.C Magoli tatu kwa nunge.”
Mwalimu wetu alituhutubia.
a)Eleza sajili ilyotumiwa hapa. (alama 2)
b) Eleza sifa zozote nane za sajili hii (alama 8)
Mwisho






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers