Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Lswa 400:Nadharia Ya Uhakiki Wa Fasihi Na Sanaa Za Maonyesho Question Paper

Lswa 400:Nadharia Ya Uhakiki Wa Fasihi Na Sanaa Za Maonyesho 

Course:Elimu

Institution: Kenya Methodist University question papers

Exam Year:2011



CHUO KIKUU CHA KIMETHODISTI, KENYA

MTIHANI WA MWISHO WA TREMESTA YA TATU, 2011

(MASOMO YA LIKIZO)
KITIVO : ELIMU NA SAYANSI YA JAMII
IDARA : ELIMU
KODI : LSWA 400
ANWANI : NADHARIA YA UHAKIKI WA FASIHI NA SANAA ZA MAONYESHO
MUDA : SAA MBILI




Maagizo:

Jibu maswali yoyote matatu

Swali la Kwanza.

Fafanua dhana zifuatazo:

Nadharia

(ala. 4)

Uhakiki

(ala. 4)

Eleza shabaha ya nadharia katika kazi ya fasihi

(ala. 6)

Eleza aina zozote tatu za uhakiki

(ala. 6)

Swali la Pili.

Fafanua nadharia zifuatazo kwa mujibu wa fasihi.

Nadharia ya uhalisia

(ala. 5)

Nadharia ya ubwege

(ala. 5)

Nadharia ya ufeministi

(ala. 5)

Nadharia ya umaksi

(ala. 5)

Swali la Tatu
Tathmini mchango wa Plato na Aristotle katika kazi ya sanaa. (ala. 20)

Swali la Nne.

Eleza maana ya istilahi zifuatazo kama zinavyojitokeza katika fasihi

Uhusika

(ala. 2 )

Wahusika

(ala. 2)

Fafanua wahusika wafuatao

Mhusika bapa

(ala. 4)

Mhusika kinyago

(ala. 4)

Mhusika mviringo

(ala. 4)

Mhusika mkinzani

(ala. 4)

Swali la Tano.
Eleza maana ya sanaa ya maonyesho na ufafanue vipengele vyake muhimu. (ala. 20)






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers