Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Educ 331:Mbinu Za Kufunzia Kiswahili  Question Paper

Educ 331:Mbinu Za Kufunzia Kiswahili  

Course:Education

Institution: Kenya Methodist University question papers

Exam Year:2014



CHUO KIKUU CHA KIMETHODISTI, KENYA

MTIHANI WA MWISHO WA TREMESTA YA TATU, 2014

(MCHANA)
KITIVO : ELIMU NA SAYANSI YA JAMII
IDARA : ELIMU
KODI : EDUC 331
ANWANI : MBINU ZA KUFUNZIA KISWAHILI
MUDA : SAA MBILI




Maagizo

Jibu maswali Matatu

Swali la Kwanza

Dhihirisha mambo matano ya kuimarisha wanafunzi katika stadi ya kusoma.

(Al 10)

Eleza sababu tano za mwalimu kuwa na maazimio ya kazi.

(Al 10)

Swali la Pili

Eleza umuhimu wa mwalimu wa Kiswahili kujaza na kuhifadhi rekodi endelezi za kazi.

(Al 10)

Fafanua njia zozote tatu ambazo unapaswa kutumia kufanikisha lugha ya wanafunzi katika mijadala.

(Al 10)

Swali la Tatu

Nyenzo ni muhimu katika kufunzia lugha ya Kiswahili. Thibitisha ukweli huu.

(Al 10)

Fafanua hoja tano kubainisha umuhimu wa kutahini na kutathmini wanafunzi katika somo la Kiswahili.

(Al 10)

Swali la Nne

Jadili mambo ambayo yanaweza kuwafanya wanafunzi wasielewe ufahamu.

(Al 10)

Fafanua vile mwalimu wa Kiswahili anaweza kuwasaidia wanafunzi wenye shida hizo.

(Al 10)

Swali la Tano
Tayarisha maazimio ya kazi ya wiki moja kwa kidato cha tatu. (Al 20)






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers