Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Kiswahili Form 2 Question Paper

Kiswahili Form 2 

Course:Kiswahili

Institution: Form 2 question papers

Exam Year:2011



1)Bainisha mzizi katika sentensi hizi

a)Aliwasamehe.

b)Jipangeni

2)Nomino ambazo zimetumika katika sentensi hizi ni za aina gani?

a)Kundi la watoto lilifika katika mkutano.

b)Ujinga wa wafanyikazi umezidi.

3)Zitungie sentensi nomino hizi ili kuonyesha ngeli zake.

a)Kibua.

b)Mshono

4)Andika ukanusho wa sentensi hizi.

a)Chakula kitamu kimepikwa na wanawake.

b)Alienda Mombasa kumwona mpwa wake.

5)Andika kinyume cha sentensi hizi.

a)Baba mzuri humpikia mkewe chai.

b)Mtoto alifurahi aliponunuliwa mwanasesere.

6)Kuna sifa mbili kuu ya nomino za ngeli ya ya-ya. Zitaje.

7)Tunga sentensi ukitumia vitenzi hivi.

a)Sambamba.

b)Kishirikishi kipungufu.

8)Tunga sentensi ukitumia nafsi ya pili kwa wingi kisha uikanushe.

9)Andika sentensi hizi upya kama ambavyo umeagizwa.

a) Jitu lililomkata limetoweka lisionekane (Andika kwa udogo)

b) Maji yakimwagika hayazoleki. (Andika kwa wakati ujao)

10)Tunga sentensi ukitumia vitenzi hivi na hali zilizoko kwenye mabano.

a) Twanga (fanyika)

b) Lewa (tendesha)








More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers