Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Edk 202:Theories And Analysis Of Kiswahili Literature Question Paper

Edk 202:Theories And Analysis Of Kiswahili Literature 

Course:Bachelor Of Education (Arts)

Institution: Rongo University question papers

Exam Year:2017



JIBU SWALI LA KWANZA NA MENGINE MAWILI
1.a.Fafanua dhana ya nadharia (4mks)

b.Kwa kutumia riwaya Nyota ya Rehema,eleza namna mbali mbali ambavyo wahusika wanaweza kuainishwa(10mks)

c.Eleza umuhimu wa nadharia katika kusoma,kuchambua na kuhakiki kazi ya fasihi,tetea kauli hii kwa kurejelea nadharia zozote mbili za kifasihi unazozifahamu(10mks)

d.Huku ukirejelea riwaya za kiswahili ,eleza dhana zifuatazo(6mks)
Usimulizi
Mandhari
Msuko



2.Masuala ya kijinsia ni maudhui ambayo hayajitokezi kwa uwazi au yamebanwa katika fasihi ya kiswahili. Jadili madai haya ukionyesha jinsi masuala haya yanavyoshughulikiwa katika Mama Ee(Ari Mwachofi) (20mks)


3.Umuundo unaweza kutuongoza kujua vipengele mbalimbali vya fasihi vinavyoweza kuchanganuliwa na mwanafunzi.Taja na ufafanue vipengele vyovyote vitano vinavyoweza kuchanganuliwa katika riwaya(20mks)


4.Jadili kwa kina mambo matano muhimu yanayotokea katika riwaya ya Rosa Mistika yanayoweza kudhihirisha uhalisi wa yale yanayowakumba vijana na wanawake katika jamii ya sasa(20mks)


5.a.Eleza mihimili mikuu ya nadharia ya utabia kama inavyopendekezwa na Pavlov(10mks)

b.Jadili matumizi ya nadharia ya utabia katika maisha ya kila Sikh(10mks)






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers