Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Mbinu Za Lugha Na Fasihi Question Paper

Mbinu Za Lugha Na Fasihi 

Course:Diploma In Education

Institution: Kenyatta University question papers

Exam Year:2008



KENYATTA UNIVERSITY
UNIVERSITY EXAMINATIONS 2007/2008
SELF- SPONSORED PROGRAM -SCHOOL BASED
FIRST SEMESTER EXAMINATION FOR THE POSTGRADUATE DIPLOMA OF EDUCATION
.ECTIPG/20: MBINU ZA LUGHA NA FASIHI
DATE: Tuesday 29th April 2008 TIME: 8.00 am -10.00 am

=======================================================================================================
MAAGIZO:
Jibu maswali matatu likiwemo swali la kwanza ambalo ni la lazima.

1.(a)(i) Taja na kufafanua sifa zozote tatu ambazo zinajitokeza katika fasili ya lugha. (3 )

(ii) Ukirejelea sifa zo zote mbili ulizotaja, eleza kanuni za kufundishia
lugha unazoweza kupata kutokana na sifa hizo. (4)

(b) i)Taja sifa za kimsingi ambazo lengo bora la kipindi hustahili kuwa nazo. (3)
(ii) Ukizingatia sifa hizo, andika:

>Lengo moja la kipindi linalohusiana na ufundishaji wa lugha na, (2~)
>Lengo moja la kipindi linalohusiana na ufundishaji wa fasihi.

(c) Toa hoja za kuunga mkono au kupinga masharti ya kufundisha lugha na
fasihi kama somo moja. (5)

2.(a)Kwa kutoa mifano inayofaa, elezajinsi lugha ya mama inavyoweza kuathiri Kiswahili cha mwanafunzi katika vipengele vifuatavyo:
(i) Matamshi
(ii) Msamiati
(iii) Sarufi (9)

(b) Eleza kwa kutoa mifano kamili jinsi utakavyomshughulikia mwanafunzi mwenye shida ya kutofautisha kimatamshi kati yajozi za sauti zifuatazo:
(i) p- f
(ii) dh-z

3.a)Je ni mambo gain ambayo huelekea kufanya wanafunzi kutopenda somo la
mashairi? (7)

b)Wewe kama mwalimu unaweza kufanya nini kuhakikisha kwamba hali hii
inabadilika? (8)

4.a)Je msamiati na sarufi vinahusiana vipi? (3)

b)Elezajinsi unavyoweza kuukabili ufundishaji wa maneno yafuatayo ukitaka wanafunzi wang'amue matumizi yake na waweze kuyatumia kwa njia inayofaa:
(i) -ki-
(ii) piga (12)

5. "Mbinu ya Kimapokeo imepitwa na wakati, na haina tena nafasi katika ufundishaji
wa Kiswahili katika shule humu nchini." Jadili kauli hii.






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers