Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Kidagaa Kimemwozea “....usiniweke pembeni kama tanbihi, mimi na wanawake wenzangu kama wanaume wengine wafanyavyo waandikapo...” a) Fafanua muktadha wa dondoo hili (alama 4)

Kidagaa Kimemwozea
“....usiniweke pembeni kama tanbihi, mimi na wanawake wenzangu kama wanaume wengine wafanyavyo waandikapo...”
a) Fafanua muktadha wa dondoo hili (alama 4)
b) Fafanua mbinu mbili za uandishi zilizotumika hapa (alama 2)
c) Hakiki usawiri wa wahusika wa kike katika riwaya hii (alama 14)

Answers


ESTHER
Dondoo hili lapatikana mwishoni mwa riwaya.
- Ni kauli ya Imani akimsemea Amani.
- Punde baada ya sherehe ya amu yake Amani kuachiliwa huru,Imani anamshajisha Amani kuandika tawasifu yake.
- Anamrai awasawiri vilivyo wanawake katika tawasifu ile. (alama 4*1=4)
b) Mbinu za uandishi.
- Nahau- usiniweke pembeni
- Tashbihi – kama tanbihi

c) Usawiri wa Wahusika wa kike.
Kuna wale wenye utu- Imani na Zuhura.
- Kuna wale wasio nao-Lowela,Michelle,na Mashaka.
- Walezi wema – Imani na Zuhura.
- Walezi wasio wema ni kama Lowela.
- Waadilifu kama Imani na mama yake.
- Wasio waadilifu kama Lowela.
- Wanaowajibika kazini kama imani na mama yake.
- Wa umri wa makamo kama Dora na Zuhura.
- Aidha kuna vijana kama Imani,Lowela na Mashaka.
- Jasiri- Imani na kwa kiwango fulani, Dora.
- Wengine wanaonekana kuishi kwenye vivuli vya wanaume
ESTHER STEVE answered the question on May 14, 2018 at 19:53

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions