Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Hatua ya serikali kuu kumpa kila mwanafunzi wa darasa la kwanza tarakilishi ni ya manufaa sana. Jadili.

Hatua ya serikali kuu kumpa kila mwanafunzi wa darasa la kwanza tarakilishi ni ya manufaa sana. Jadili.

Answers


ESTHER
Manufaa
i) Tarakilishi itarahisisha ufunzaji wa masomo mbalimbali kwa upande wa mwalimu
ii) Itakuza na kuimarisha ubunifu miongoni mwa wanafunzi
iii) Hatua hii itamtanguliza mapema mwanafunzi katika ulimwengu wa tarakilishi na teknohama.
iv) Itasahihisha kuelewa haraka wa masomo kwa kurahisisha mada ngumu katika silibasi kwa mwanafunzi
v) Itaboresha matokeo ya mitihani kwa wanafunzi husika.
vi) Itaimarisha Uchumi wa watengenezaji wa tarakilishi na programu.
vii) Zitatumika katika utafiti
viii) Zitapunguza mzigo kwa wanafunzi wa kubeba vitabu vingi
Hasara
102/1,102/2,102/3 kiswahili
Top grade predictor publishers Page | 118
i) Ni ghali kutekeleza – itahitaji fedha nyingi
ii) Bila kuwepo kwa walimu walio na umilisi wa kutosha wa kompyuta, hatua hiyo haitakuwa na manufaa
iii) Kutakuwa na tatizo la usalama wa wanafunzi na tarakilishi zenyewe.
iv) Baadhi ya shule hazina miundo-msingi ya kutekeleza masomo kwa tarakilishi k.v. kawi na madarasa.
v) Zisipodhibitiwa, tarakilishi zitaweza kusababisha utovu wa maadili kwa wanafunzi kupitia mitandao (hoja 5 katika kila upande)
Tanbihi
- Hii ni insha ya mjadala
- Iwe na upande wa kuunga na ule wa kupinga
- Katika hitimisho mwandishi aonyeshe msimamo wake
ESTHER STEVE answered the question on May 14, 2018 at 20:01

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions