-
Tom: Vipi Tracey? Naona leo unalinga sana.
Umenivaria miwani, mbona hivi? Is it because you are very smart today?
Tracey: Niko poa! Hata hivyo naona una yako mengine wewe! Siringi! Nikobusy tu sana. Plus company yako inatisha, hujui siku hizi nimechill.Tena umenubore.
Tom: Kumbe wewe ni……………………………
(a) Taja sajili inayojitokeza katika dondoo hii. (alama 1)
(b) Taja mifano inayojitokeza katika dondoo ya
(i) Kubadili msimbo (alama 1)
(ii) Kuchanganya msimbo. (alama 1)
(c) Ni kwa nini wazungumzaji hubadili na kuchanganya msimbo. (alama 2)
(d) Ni mzungumzaji yupi ana lafudhi? Ni nini maana ya lafudhi? (alama 3)
(e) Taja sababu mbili za kuwa na lafudhi. (alama 2)
Date posted:
April 30, 2018
-
(a) Katika jamii huwa wakati mwingine kuna matumizi ya lugha isiyo ya kistaarabu.taja mifano mitano ya lugha ya sampuli hiyo. ( alama 5)
(b) Taja mambo matano yanayoathiri jinsi tunavyoweza kutumia lugha katika jamii(mtindo nafsi na mtu)
MAJIBU
Date posted:
April 30, 2018
-
(a) Eleza maana ya istilahi zifuatazo za isimu jamii.
i) Lafudhi
ii) Lahaja
iii) Rejesta
Taja sifa nne za sajili ya wanasiasa (alama 4)
Date posted:
April 30, 2018
-
Mifano miwili ya fomyula ya ufunguzi wa hadithi
Date posted:
April 30, 2018
-
Eleza vigezo vya kutumia katika uchambuzi wa lugha
Date posted:
April 30, 2018
-
Jadili ufaafu wa anwani "kigogo" katika tamthilia ya kigogo
Date posted:
April 29, 2018
-
“Mwendazake alikuwa mcha Mungu pengo aliloacha halijaziki. Atakumbukwa milele
daima. Mungu ….”
(i) Tambua muktadha wa rejista hii.
(ii) Eleza sifa za rejista hii.
Date posted:
April 28, 2018
-
(a) Nini maana ya kufa kwa lugha.
(b) Eleza sababu zozote tano zinazochangia kufa kwa lugha.
(c) Taja aina tatu za makosa ya lugha.
Date posted:
April 28, 2018
-
(a) Vijana huchangia pakubwa katika kuhujumu maendeleo ya lugha ya kiswahili. Jadili ukweli wa kauli hii ukitoa mifano miwili.
(b) Pendekeza njia tatu ambazo kwazo vijana wanaweza kushiriki katika kuikuza lugha ya kiswahili.
Date posted:
April 28, 2018
-
1. Eleza maana ya istilahi hii: Usanifishaji
2. Eleza mambo manne yaliyochangia maenezi ya kiswahili kabla ya uhuru.
Date posted:
April 28, 2018
-
"Starehe za nyani kuchezea tagaa mbovu nazo ni starehe?"
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Tambua mbinu ya lugha katika dondoo na ueleze maana.
c) Eleza sifa sita za:
i. Msemaji
ii. Msemewa
Date posted:
April 28, 2018
-
Tamaa inatawala katika Tamthilia ya Kigogo. Dhibitisha
Date posted:
April 28, 2018
-
Jadili maudhui ya utabaka katika tamthilia ya Kigogo.
Date posted:
April 28, 2018
-
Ichambue jalada ya tamthilia ya Kigogo
Date posted:
April 28, 2018
-
Eleza tofauti kati ya malumbano ya utani na mawaidha
Date posted:
April 27, 2018
-
Eleza umuhimu wa ngomezi
Date posted:
April 27, 2018
-
(a) Eleza maana ya mivigo na inakotumika
(b) Eleza sifa za miviga
(c) Onyesha umuhimu wa miviga.
Date posted:
April 27, 2018
-
Fafanua sifa za mawaidha ukizingatia
hadhira
fanani
maudhui
fani
Date posted:
April 26, 2018
-
Fafanua aina za nyimbo zifuatazo bembelezi, za sifa, za mapenzi.
Date posted:
April 24, 2018
-
Taja sifa Tano bayana Kati ya pijini na Krioli
Date posted:
April 24, 2018
-
Tumia neno vibaya kama: kivumishi, kielezi na kiwakilishi
Date posted:
April 24, 2018
-
Weka majina haya katika ngeli mbili tofauti. 1.Ua 2. Maziwa 3. Nyanya 4. Tikiti
Date posted:
April 24, 2018
-
Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli ya kutendewa.1. Twika 2. Tata
Date posted:
April 24, 2018
-
Taja matumizi matatu ya kiambishi KI
Date posted:
April 24, 2018
-
Andika sentensi sahihi ukitumia viambishi vya hali na nyakati vifuatavyo.
1. Ku
2. Ja
3. A
Date posted:
April 24, 2018
-
Eleza jinsi ya kuandika ripoti ya utafiti.
Date posted:
April 23, 2018
-
Utawala mbaya ni tatizo kuu linalozikumba nchi nyingi za kiafrika. Jadili kwa kurejelea matukio mbalimbali katika tamthilia ya kigogo.
Date posted:
April 23, 2018
-
Eleza suala la nafasi ya ndoa katika kigogo
Date posted:
April 22, 2018
-
Utengano wa kitabaka umechangia kuwepo Kwa dhuluma barani Afrika. Ukirejelea hadithi zifuatazo katika diwani ya Tumbo lisiloshiba, Dhibitisha. 1.Tumbo lisiloshiba 2.shibe inatumaliza...
Date posted:
April 21, 2018
-
Taja aina za sentensi.
Date posted:
April 20, 2018