Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Kiswahili Karatasi La 3 Question Paper

Kiswahili Karatasi La 3 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2008



102/3
KISWAHILI
KARATASI YA TATU
FASIHI
JULAI / AGOSTI 2008
MUDA: SAA 2 ½
JARIBIO LA TATHMINI YA PAMOJA WILAYA YA
BOMET 2008
HATI YA KUHITIMU KISOMO CHA SEKONDARI KENYA
(K.C.S.E)
102/3
KISWAHILI
KARATASI YA TATU
FASIHI
JULAI / AGOSTI 2008
MAAGIZO
_ Jibu maswali manne pekee.
_ Swali la kwanza ni la lazima.
_ Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja
Karatasi hii ina kurasa nne zilizopigwa chapa. Mtahiniwa ahakikishe kwamba kurasa zote zimepigwa
chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.
SEHEMU YA A: TAMTHLIA (KIFO KISIMANI- KITHAKA WA MBERIA)
1. “Tayari mateso ndiyo wanayopumua wanabutangi,” Dhihirisha ukirejelea tamthilia ya kifo
kisimani. (alama 20)
SEHEMU B: RIWAYA (Mwisho wa kosa -2 Burhani)
2

2. “ Ninakwambia tena hii nyumba yangu na wewe ni mke wangu hapana yeyote anayeweza kunizuia
au kuingilia kati”
a) Fafanua muktadha wa dondoo hili (alama5)
b) Eleza kasoro zozote za msemaji (alama 6)
c) Ni masharti gani msemezwa anawekewa (alama 2)
d) Je msemezwa alitii masharti aliyowekewa (alama 3)
e) Hali hii inatimia vipi baadaye? (alama 4)
3. Mwandishi ameshughulikia kwa kina swala la uadilifu.
Fafanua rai hii kwa kutoa mifano maridhawa. (alama 20)
SEHEMU C: HADITHI FUPI (Diwani mayai waziri wa maradhi na hadithi nyingine)
4. Onyesha athari za ulevi kama zilivyowasilishwa na sinjiri mukuba msanii wa kisa ‘Fumbo la
mwana’ (alama 20)
5. Hadithi - uteuzi wa moyani – Rayya Timmamy.
“ Pengine mwanangu hutimizi wajibu wako.”
a) Mzungumziwa aliamua kufanya uteuzi mwafaka na kuutekeleza eleza kwa kutolea
mifano mitano (alama 10)
b) Kutokana na hadithi “uteuzi wa moyoni” thibitisha kuwa wanawake ndio maadui
wakubwa wa wanawake wenzao. (alama 10)
SEHEMU D:FASIHI SIMULIZI
6.
a) Taja mbinu zozote tatu zinazotumiwa kuhifadhi fasihi simulizi huku ukitolea mifano
(alama 6)
b) Eleza umuhimu wa kuhifadhi fasihi simulizi (alama 6)
c) Semi ni utanzu wa fasihi simulizi ambao ni mfupi na uundwao kwa maneno machache
au sentensi kadha.Taja na ujadili vipengele vyovyote vinne vinavyojumuishwa na
kundi hili (alama 8)
SEHEMU E: USHAIRI
7. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
NYOOSHA MKONO
1. Nyoosha mkono, uviringe ngumi, unyanyuwe kwa hasira
Nyoosha mkono, sema hunitumi, ila kwa haki ujira
Nyoosha mkono, alama ya kukataa
Alama ya nguvu
2. Nyoosha mkono, na macho makali, uwaonyeshe kukerwa
Nyoosha mkono, wataka halali, kwamba hutaki kuporwa
Nyoosha mkono, alama ya kukataa
Alama ya nguvu
3

3. Nyoosha mkono, jiunge umoja, na wateswaji wenzako
Nyoosha mkono, mwonyeshe miuja, yaondoke masumbuko
Nyoosha mkono, alama ya kukataa
Alama ya nguvu.
4. Nyoosha mkono, umekula njama, uyakatae madhila
Nyoosha mkono, nyanyua kwa hima, watambue hukujaja
Nyoosha mkono, alama ya kukataa
Alama ya nguvu.
5. Nyoosha mkono, Ivume sauti, inayojaa kitisho
Nyoosha mkono, mume jizatiti, kwa mengi maamrisho
Nyoosha mkono, alama ya kukataa
Alama ya nguvu.
6. Nyoosha mkono, mumeshikamana, huo ukuta wa chuma
Nyoosha mkono kitisho hakuna wao watarudi nyuma
Nyoosha mkono, alama ya kukataa
Alama ya nguvu.
MASWALI
a) Hili ni shairi la aina gani (alama 1)
b) Taja bahari zozote mbili zilizotumika katika utunzi wa shairi hili (alama 2)
c) Mwandishi wa shairi hili anapiga vita mambo gani? (alama 5)
d) Eleza muundo wa shairi (alama 4)
e) Kunyoosha mkono ni alama ya nini? (alama 2)
f) Mshairi ametumia mbinu gani ya lugha ili kafanya ujumbe wake ukolee? (alama 2)
g) Mwandishi wa shairi hili alizingatia arudhi zipi za ushairi? (alama 4)
8. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
1) Tunda la elimu zote, wasema wanazuoni
Ni kwamba mtu apate, kumtambua manani
Ndipo hadhi apate, akumbukwe duniani.
2) Elimu bila ukweli, haizidi asilani
Giza na nuru muhali, katu havitangamani
Uwongo ufe kwa kweli, itue nuru moyoni
3) Elimu ni kama mali, haichoshi kutamani
Ni bora yashinda mali, taji la wanazuoni
Elimu njoma miali, langazayo gizani.
4) Mtu hachomwi na mwiba, na viatu miguuni
ulimwengu una miiba, tele tele majiani
Elimu ukiishiba, u salama duniani
5) Wafu ni wasiosoma, watazikwa ardhini
Hai ndio maulana, wapaao maangani
Elimu jambo adhima, aso nayo maskini
6) Toa wakfu ujana, elimu ukitamani
na uwe mzee sana, kujua usijihini
Elimu ni jambo adhima, aso nayo maskini
4

7) Elimu ina malipo, utoyalipwa mwishoni
Pale uitafutapo, ujira usitamani
Mwanachuoni afapo, mbingu huwa na huzuni
8) Haki ya kuheshimiwa, ni yao wanachuoni
Wao wameongolewa, na ni taa duniani
Kweli wanapoijua, watoe bila kuhuni
9) Elimu bila amali, mti usio majani
Haumtii kivuli, aukaliaye chini
Inakuwa mushkeli, wa kughuri insani.
MASWALI
a) Pendekeza kichwa kifaacho kwa shairi hili (alama 2)
b) (i) Ushairi wa aina hii huitwaje? (alama 2)
(ii) Taja sifa zozote tatu za aina hii ya ushairi. (alama 3)
c) (i) Ni mbinu gani ya lugha inayotumiwa katika mloto wa ubeti wa saba (alama 2)
(ii) Huku ukitoa mfano, onyesha upungufu wa sheria za utunzi wa mashairi katika ubeti
wa nne kwa upande wa mizani. (alama 2)
(d) Andika ubeti wa mwisho wa lugha ya nathari. (alama 4)
(e) Maneno yafuatayo yana maana gani katika shairi
i. miali
ii. ulimwengu una miiba
iii. maulama
iv. wakfu
v. wameongolewa (alama 5)






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers