Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Busia District Mock - Kiswahili Paper 2 Question Paper

Busia District Mock - Kiswahili Paper 2 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2011

Jina: …………………………………………………………………… Nambari: ………...………
Shule: ………………………………………………………………. Sahihi ....................................
Tarehe: …………….....................................................................……
102/2
KISWAHILI
LUGHA
KARATASI YA 2
JULAI/ AGOSTI 2011
MUDA: SAA 2 ½
Hati ya kuhitimu kisomo cha sekondari Kenya (K.C.S.E)
Kiswahili
Lugha
MAAGIZO
• Andika jina lako na namba yako katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
• Weka sahihi yako na tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa
• Jibu maswali yote.
• Majibu yaandikwe katika nafasi zilizoachwa wazi katika kijitabu hiki cha maswali.
Karatasi hii ina kurasa 8 zilizopigwa chapa. Watahiniwa ni lazima waangalie kama kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.
1. UFAHAMU
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali:
Janga la umaskini linayagusa makundi mbalimbali ya jamii, mikoa na maeneo mbalimbali kijiografia na kwa njia tofauti. Kwa mujibu wa takwimnu za kimataifa, mtu huhesabiwa kama maskini ikiwa,pato lake kwa siku ni chini ya dola moja. Haimkiniki kuapata taswira kamili ya umaskini bila ya kukusanya taarifa kwa njia mbalimbali na kutoka katika makundi tofauti ya kijamii. Asilimia kubwa ya wanajamii wengi katika nchi zinazoendelea wametopea kwenye mwina wa umaskini na hawana matumaini ya kujiopoa.
Hali hii haiwezi kubadilika ikiwa hazitabuniwa njia nzuri za kuupunguza na hata kuumaliza
umaskini. Juhudi za kuupunguza umaskini zinaweza kufanikiwa ikiwa zitaongozwa na malengo yaliyo dhahiri. Mikakati ya kuupunguza umaskini inapaswa kulenga kwenye matoke ya utekelezaji wa sera na shughuli zinazodhamiriwa kupunguza umaskini. Ili kufanikiwa pana haja ya kuangaza kwenye maeneo matatu makuu. Kwanza, ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini unaotokana na kipato. Pili, kuinua ubora wa maisha na ustawi wa jamii. Tatu, kuhimiza utawala bora na uwajibikaji. Maeneo haya yanahusiana na kutegemeana kwa kiwargo kikubwa. Mathalan, kuwepo kwa utawala bora ni msingi wa kujengeka kwa uchumi ambao ni msingi wa kipato kinachochangia kuinua ubora wa maisha.
Zipo sifa kuu za ukuaji wa uchumi ambazo zina nafasi muhimu katika kuupunguza umaskini.
Kwanza, ni lazima ukuaji wenyewe uwe ni ule unaowagusa watu wengi na kwa insafu. Ni sharti ziwepo sera na hatua maalumu ili kuelekeza rasilmali kwa makundi ya jamii katika sehemu za nchi au sekta zilizo maskini zaidi. Kwa kufanya hivi itakuwa rahisi kwa sehemu au sekta hizo kushiriki katika shughuli za uzalishaji au katika utoaji wa huduma za jamii. Inahalisi msaada wa kutosha utolewe na kujengwa mazingira mazuri yatakayowezesha matumizi mazuri ya rasilmali hizo.
Pili, lazima ukuaji uwe mkubwa na endelevu. Hii inamaanisha kuwa ni lazima nchi izalishe viwango vikubwa na endelevu vya akiba ya ndani na uwekezaji. Pale inapobidi kutafuta misaada kutoka nje, basi ni lazima misaada hiyo itumike kwa busara na uangalifu ili iweze kuiweka nchi katika mwelekeo thabiti wa ukuaji. Ni lazima nchi ihakikishe kuwa shughuli za maendeleo za kizazi cha sasa haziathiri mahitaji ya maéndeleo ya kizazi cha kesho. Tatu, ukuaji hauna budi pia kujumuisha mkakati wa kibiashara ili kuimarisha ubunifu na ushindani wa wazalishaji wa ndani. Uzalishaji wowote hauwezi kufanikiwa kama hamna masoko ya kuuza bidhaa hizo.
Nne ni muhimu uwepo msisitizo mkubwa kwenye kuongeza fursa za ajira. Itakuwa muhimu sana
ikiwa mkakati wa ukuaji wa uchumi kuangalia mahusiano baina ya sekta mbalimbali. Aidha uwekwe umuhimu wa kipekee kwenye viwanda vinavyohusika na mazao ya kilimo na shughuli za uzalishaji katika maeneo ya vijijini zisizohusu kilimo. Mojawapo wa sekta muhimu ni ile ya utalii. Hii ni sekta inayotoa ajira ya moja kwa moja na kuwa msingi wa watu kujipatia riziki. Mapato serikali inayoipata kutokana na sekta kama hii yanaweza kutumiwa katika kuboresha huduma za uchumi na kijamii, hivyo kuchangia katika maendeleo endelevu ya miundombinu na mtaji wa watu.
Kuinua ubora na ustawi wa jamii kunategemea utoaji, uwezo wa kumudu na upatikanaji wa huduma kama vile elimu, afya, maji, matibabu na kinga dhidi ya VVU/Ukimwi na mipango ya ulinzi au hifadhi ya jamii. Zaidi ya hayo, maisha ya watu huwa bora zaidi wanapoishi katika mazingira safi na yanayolindwa; mathalan yasiyo na uchafuzi wa hewa na maji na yasiyo na mazalia ya mbu. Maisha bora huiwezesha jamii kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji ambapo wanawake na wanaume hupata fursa sawa. Vilevile tija huongezeka na kuendelezwa pale ambapo mazingira yanalindwa na kutumiwa kwa njia endelevu.
Ili pawe na ukuaji wa uchumi unaowagusa watu wa ngazi zote na kuimarika kwa ubora wa maisha
na ustawi wa jamii ni lazima pawepo na utawala bora. Suala la utawala bora linalenga katika kuangalia mifumo na michakato ya kiuchumi kama vile usimamizi wa rasilmali za umma (fedha na maliasili), ulinzi binafsi, hali ya kuvumiliana na kuwashirikisha wananchi katika kufanya maamuzi. Kwa mfano, wanaweza kushirikishwa kuhakikisha kuwa mifumo na taratibu za utawala ni za uwakilishi na zinazowezesha uwajibikaji wa wawakilishi kwa wale wale wanaowakilishwa. Mambo muhimu katika eneo hili ni haki za binadamu, mfumo wa haki na wenye ufanisi wa sheria dhidi ya rushwa. Eneo hili linabainisha amani, utulivu wa kisiasa, umoja wa kitaifa na mshikamano. Mseto wa mambo haya yote ni msingi mzuri wa kuupunguza umaskini
(Makala hii imehaririwa upya kutoka makala ya ‘Muundo wa Mku II’,
Gazeti la Rai, Septemba 2-8, 2004)
Maswali
a) Yape makala haya kichwa mwafaka. (ala.1)
……………………………………………………………………………………………………………
b) Taja kigezo cha kupimia umaskini ( ala.1)
……………………………………………………………………………………………………………
c) Taja hatua tatu ambazo zinapaswa kuchukuliwa ili kukabiliana na umaskini. (ala.3)
……………………………………………………………………………………………………………
..……………………………………………………………………………………………………………
..……………………………………………………………………………………………………………
d) Eleza dalili nne za ukuaji wa uchumi (ala.4)
……………………………………………………………………………………………………………
..……………………………………………………………………………………………………………
..……………………………………………………………………………………………………………
..……………………………………………………………………………………………………………
e) Taja chanzo kinachotumiwa kufikia uamuzi wa kuwepo kwa umaskini (ala.1)
……………………………………………………………………………………………………………
f) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyo tumika katika makla uliyosoma. (ala. 3)
i) Insafu
……………………………………………………………………………………………………………
ii)Miundombinu
..……………………………………………………………………………………………………………
iii) Mwina
..……………………………………………………………………………………………………………
UFUPISHO
Soma taarifa hii kisha ujibu maswali yanayo fuata.
DHULUMA
Dhuluma dhidi ya wanawake imekithiri mipaka. Ingawa wanawake wengi hudhulumiwa,wengi kati
yao hawatambui kuwa wanadhulumiwa. Sababu ni kwamba hawajaelimisha kuhusu haki zao.
Kuna dhuluma za aina nyingi ambazo hazieleweki na watu wengi.Mwanamke anaweza
kudhulumiwa kisaikolojia kwa kufanya mambo yanayoweza kuathiri fikira zake. Kwa mfano,matusi yasiyo na msingi na ambayo humdunisha mwanamke kama kiumbe dhaifu humfanya awaze mara kwa mara kuhusu udhaifu wake. Huwa haridhiki na lolote atendalo kwa kujiona dhaifu.
Wakati mwingine wanawake hukandamizwa kwa kunyimwa mahitaji muhimu.Ndugu za baadhi ya
wanaume hujitenga naye kama ndwele.Hawajui pia yeye anahitaji washirika. Mwanamke
anapotengwa,hujipata mpweke na mweye mawazo mengi ambayo yanaweza kuchangia kutotulia
kiakili.vilevile,anapokosa kupewa chakula cha kutosha,huishia kuomba majirani ambao humtusi na kumkejeli. Yeye hurudi pale pale pa mawazo. Kuna wale ambao hujitia kitanzi ili kujitoa kwenye jambo hili.
Mara kwa mara ubakaji hutendewa wanawake kwa sababu hawawezi kujitetea kutokana na udhaifu
wa kimwili. Ingawa kutengwa kwa mwanamke huletwa na dhana potovu kuwaamewapokonya wenzake
njia za kupata mahitaji aliyokuwa akiwapa jamaa zake,ubakaji hutokea kwa sababu ya uchu wa
wanaume,matumizi ya dawa za kulevya na wanawake wenyewe kuteka fikira za wanaume katika
kuwabaka.
Wanawake wengi wanaweza kulemazwa kwa kupigwa,kuchomwa au kukatwa na waume zao.
Mambo haya hutokea kwa sababu wanaume huwa wamechochewa kuwa kudhulumu wanawake
kimwili,ndivyo suluhisho la pekee kupata heshima zao. Vile vile, wengine huwa hawana uwezo wa kulisha na kutunza familia zao. Wao hukimbilia kuwapiga kama njia ya mkato ya kuficha udhaifu wao (wanaume) wa kutoweza kuwatunza wake zao.
Tohara za wanawake husababisha maumivu kwa wanawake. Sio tu kwa wakati huo bali hata
baadaye anapotaka kujifungua. Mwanamke anapofikiria uchungu huu,yeye huathirika kimawazo na
hata kuogopa kujifungua baadaye. Hata hivyo aghalabu mwanamke anapopitia tu tohara
huozwa,jambo ambalo ni ovu kwani baadhi yao huwa hawajakomaa au wangali wanasoma.
Utamadumi umefanya mwanamke kuwa ndiye pekee ayayeweza kufanya kazi za nyumbani. Wakati
wanaume wanapolaza damu,wanawake huwa wanashughulika na kazi nyingi za nyumbani
kulima,kupika kufua,kutunza watoto na kadhalika. Huwa hawapati fursa kujiendeleza kielimu,kisiasa au katika kufanya kazi mbalimabli.
Kwa hakika ni vigumu kutatua tatizo la ubakaji kwani watu hujitetea vilivyo kuhusu sababu zao za kufanya hivyo. Wengine hawajui waanzie wapi, wakomee wapi,wengine huogopa kuishia kwa mikono ya wale wale wabakaji na wengine huhofia kufukuzwa au kuonekana kana kwamba wana kasoro na wanajamii wenzao.
Ni sharti mashirika yajitokeze kuokoa swala hili la sivyo wanawake watazidi kubaki nyuma kama koti kimaendeleo.
Maswali
1. Kwa nini wanawake hudhulumiwa (maneno yasizidi 65) ( ala.7)
Nakala Chafu
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………..…
Nakala safi
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
b) Kwa kutumia maneno yako mwenyewe na bila kupoteza maana fupisha aya saba za kwanza
(maneno 90-100) (ala.6)
Nakala Chafu
.……………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
Nakala safi
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………..…
..……………………………………………………………………………………………………………
3. MATUMIZI YA LUGHA
a) Andika anavyoitwa (aitwaye) mtendaji wa vitendo hivi ( ala 3)
i) Cheka
………………………………………………………………………………………………………..……
ii) Gomba
..……………………………………………………………………………………………………………
iii) Kaa
..……………………………………………………………………………………………………………
b) Taja matumizi mawili mawili kwa kila amojawapo ya alama zifuatazo za uakifishaji. (ala 4)
i) Koloni (nukta –mbili)
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
ii) Mistari wa mshazari
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
c) Geuza sentesni hizi ziwe katika usemi halisi ( ala. 4)
i) Mwenye hoteli alitaka kujua jumla ya vikombe vya chai tulivyohitaji.
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
ii) Mtoto alisema kuwa angewatembelea kwao mwezi amabo ungefuata.
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
d) Ainisha shamirisho na chagizo katika sentensi (ala. 2)
Wachimba migodi wanafanya kazi haraka ipasavyo
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
e) Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia jedwali. (ala.4)
Mchuuzi shupavu ameuza samaki wote sokoni.
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………..……
f) Vitenzi vilivyopigwa mistari ni vya aina gani? (ala.2)
i) Wanafunzi walikuwa hawajawahi kukariri mashairi
………………………………………………………………………………………………………..……
ii) Wanasiasa ni watu wa kustaajabisha.
………………………………………………………………………………………………………..……
g) Tunga sentensi sahihi ukitumia vitenzi vifuatavyo katika kauli ulizopewa. (ala. 2)
i) Nywa (tendeka)
………………………………………………………………………………………………………..……
ii) La (tendesha)
………………………………………………………………………………………………………..……
h) Eleza matumiza mbalimbali ya ‘ni’ katika sentensi ifuatayo. (ala.2)
Nendeni mkamwite Kanini ambaye ni mwanafunzi wangu niliyemwacha maktabani.
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
i) Taja ala zinazotumika katika kutamka sauti zifuatazo ( ala.2)
(i) /dh/
………………………………………………………………………………………………………..……
(ii) /gh/
………………………………………………………………………………………………………..……
j) Ainisha sentensi hii. (ala.3)
Aliyenichokoza .
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………..……
k) Eleza maana ya semi zifuatazo. (ala.2)
(i) Kumbatia chui
………………………………………………………………………………………………………..……
(ii) Kunjua jamvi
………………………………………………………………………………………………………..……
l) Eleza maana ya methali
Ukitema kini temato (ala. 1)
………………………………………………………………………………………………………..……
……………………………………………………………………………………………………………
m)Yakinisha sentensi hizi (ala. 1)
i) Asingenda safari asingepata ajali
………………………………………………………………………………………………………..……
ii) Usije
………………………………………………………………………………………………………..……
n) Tofautisha maana baina ya sentesnis hizi. (ala.2)
(i) Gari la Omari limeibwa
………………………………………………………………………………………………………..……
(ii) Gari la Omari limeibiwa.
………………………………………………………………………………………………………..……
o) Andika sentensi hii upya bila kubadilisha maana ukitumia ‘O’ rejeshi na kiambishi ngeli. (ala.2)
Mwanafunzi alitumwa nyumbani juzi na hajapata karo hadi leo.
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
p) Andika sentensi ifuatayo katika wingi hali ya udogo ( ala.2)
Kitabu kilichonunuliwa hakimfai mwanafunzi huyu
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
q) Hii ni nomino aina gani? (ala.1)
Wema.
………………………………………………………………………………………………………..……
4. ISUMU JAMII
“Nawashukuru wote kwa kufika hapa kwa nia ya kupata ukweli…. Hivyo ndivyo tumetumia fedha hizo za misaada na misaada mingine tuliyopata. Asanteni sana wananchi na mnakaribishwa tena wakati wowote mnapokuwa na haja ya kujua mipango ya maendeleo katika eneo hili tena. Kwaherini”.
a) Taja sajili inayorejelewa na dondoo la maneo haya. (ala.2)
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
b) Taja sifa za sajili hii. (ala.4)
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
c) Eleza maana ya istilahi zi fuatazo za Isimu Jamii (ala.4)
i) Pijini
………………………………………………………………………………………………………..……
ii) Krioli
………………………………………………………………………………………………………..……
iii) Lahaja
………………………………………………………………………………………………………..……
iv) Lugha.
..……………………………………………………………………………………………………………

More Question Papers

Popular Exams

Return to Question Papers