Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Taswira inajitokeza vipi katika samaki wa nchi za joto

      

Taswira inajitokeza vipi katika samaki wa nchi za joto.

  

Answers


KELVIN
? Deogracius amepinda mgongo kwa umri na mwenye miguu ya matege.
? Kwa Peter, michoro ya kisana ilitundikwa ukutani, makabati ya vioo yaliyosheheni vinywaji vya aina aina na vyombo vya kichina-utajiri.
? Chumba cha Zac kina kuta zilizobambuka rangi, balbu iliyotoa mwangaza hafifu, picha kubwa ya Bob Marley iliyorarukararuka, vitabu vikuukuu viwili vya ‘Penguin Classics’, kitanda chake kimetandikwa blanketi ya rangi ya kahawia.
? Zac kufungua kikabati kidogo cheusi akatoa sahani mbili nyekundu za plastiki zilizoonyesha kuwa na mafutamafuta, kikombe cha kijani kibichi cha plastiki na glasi iliyokuwa na mavumbi.
? Nikatabasamu nikitaka aone meno yangu yenye weupe wa maziwa.
? Noti za dola za kijani kibichi.
? Wajihi wa Peter ulikuwa wa wekundu usiokoza na wala sio weupe usiotakata. Nywele zake tu ndizo zilikuwa nyeupe
? Tankhill, makasri ya mabalozi yalizungushwa kuta za mawe, juu ya kuta hizo kumechomekwa vigae vya chupa. Kuna mabwawa ya kuogelea na walinzi wa kulipwa-kuonyesha utabaka.
? Peter, akiwa na bombo (kaptula) aliyoipenda sana, alionekana kama mvulana wa miaka 14.
? Alikuwa na maungo mviringo ya ujana, mwili laini kama wa mwanamke na miguu iliyobonyea na iliyopuuka.
? Miriam rafiki yake Christine ni Mtutsi aliyekuwa na wembamba waliopendelea wazungu na macho ya vikombe.

kalvinspartan answered the question on August 15, 2018 at 12:34


Next: onyesha matumizi ya tashhisi katika hadithi fupi ya samaki wa nchi za joto
Previous: Eleza jinsi mdokezo ulivyotumika katika samaki wa nchi za joto

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions