-
``Hakuna aliyeweza kukitegua kitendawili chenyewe lakini…’’
a)Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Tambua tamathali ya usemi iliyotumiwa katika dondoo hili.
c) Fafanua chanzo na hatima ya kitendawili kinachorejelewa katika dondoo hili.
d) Eleza wasifu wa warejelewa katika dondoo hili.
Date posted:
May 6, 2019
-
‘… lakini shogake… shogake… shogake dada nikamwona ana ndevu.’
a) Eleza muktadha wa dondoo hili
b) Bainisha sifa tatu za ‘shoga’ anayezungumziwa katika dondoo hili.
c) Jadili umuhimu wa ‘dada’ anayerejelewa katika kuendeleza dhamira ya hadithi.
Date posted:
May 6, 2019
-
Fafanua jinsi mwandishi wa ‘Tumbo Lisiloshiba’ alivyotumia kinaya kufanikisha maudhui yake
Date posted:
May 6, 2019
-
Fafanua changamoto zinazokabili asasi ya ndoa ukirejelea hadithi ya Masharti ya kisasa
Date posted:
May 6, 2019
-
Ulezi umewapa wazazi wengi changamoto nyingi. Ukirejelea hadithi ya shogake, dada ana ndevu dhihirisha ukweli wa kauli hii
Date posted:
May 6, 2019
-
Aliyeumwa na nyokaakiona ung’ong’o hushtuka
a) Weka dondoo hili katika muktadha
b) Eleza namna mzungumziwa alivyoumwa na nyoka
c) Mzungumziwa anaendeleza vipi maudhui ya ushauri na ukosefu wa utu?
Date posted:
May 6, 2019
-
Dhihirisha ukweli wa methali “mzoea sahani vya vigae haviwezi” katika hadithi ya mapenzi ya kifaurongo
Date posted:
May 6, 2019
-
Jadili matatizo yanayowakumba wakaazi wa Madongo poromoka katika tumbo lisiloshiba
Date posted:
May 6, 2019
-
“Masharti ya Kisasa”
“…mapenzi ni mateso,ni utumwa, ni ukandamizaji , ni ushabiki usio na maana.”
Thibitisha ukweli wa kauli hii kama unavyojitokeza kwenye hadithi.
Date posted:
May 6, 2019
-
“Mame Bakari”
Kwa mujibu wa hadithi hii, ubahaimu anaotendewa mwanamke unakuwa na athari mbaya kwake. Onyesha kwa mifano mwafaka.
Date posted:
May 6, 2019
-
“Ndugu yangu kula kunatumaliza”
“Kunatumaliza au tunakumaliza”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Fafanua maana ya kitamthali katika kauli ‘kula tunakumaliza’
c) Kwa mujibu wa hadithi hii, nbi kwa namna gani wasemaji wanadai kula kunawamaliza?
Date posted:
May 6, 2019
-
Jadili maudhui ya usaliti katika hadithi ,’Mapenzi ya kifaurongo’ na ‘Mame Bakari.
Date posted:
May 6, 2019
-
“ Naapa na mola wangu sitofanya tena biashara hii.”
a. Eleza muktadha wa dondoo hili
b. Tathmini umuhimu wa mzungumzaji
c. “Biashara inayorejelewa ilikuwa na athari basi kwa jamii.” Huku ukirejelea hadithi hii,thibitisha ukweli wa kauli hii kwa hoja kumi.
Date posted:
May 6, 2019
-
Thibitisha kuwa ulitima ni kati ya maudhui ya hadithi ya mkubwa.
Date posted:
May 6, 2019
-
Mhini na mhiniwa njia yao moja. Jadili ukweli wa methali hii ukirejelea hadithi ya mkubwa
Date posted:
May 6, 2019
-
Kwetu tunapigania mikono ielekee vinywani. Mzoea vya sahani, vya vigae haviwezii”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili
b) Taja tamathali mbili za usemi zinazojitokeza katika dondoo hili
c) Fafanua sifa za msemaji
d) Jadili maudhui ya utabaka ukjirejelea hadithi husika.
Date posted:
May 6, 2019
-
Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika ‘Tumbo lisiloshiba na Hadithi nyingine’, fafanua maudhui ya utabaka.
Date posted:
May 6, 2019
-
Huku ukirejelea hadithi za:
i) Mapenzi ya kifaurongo
ii) Shogake dada ana ndevu
iii) Mame Bakari
Fafanua maudhui ya mapenzi kama yanavyosawiriwa.
Date posted:
May 6, 2019
-
Fafanua sifa kumi za mzee Mago katika hadithi ya tumbo lisiloshiba.
Date posted:
May 6, 2019
-
Anwani ya hadithi TUMBO LISILOSHIBA ni mwafaka kwa hadithi hii. Fafanua
Date posted:
May 6, 2019
-
Kwa kurejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba na ya Mapenzi ya Kifaurongo, fafanua maudhui ya utabaka.
Date posted:
May 6, 2019
-
‘’Acha nijiondelee duniani niwaachie wafanisi wafanikiwe.”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili
b) Fafanua sifa za mhusika katika dondoo hili.
c) Fafanua mbinu zozote nne za kifani katika hadithi hii.
Date posted:
May 6, 2019
-
‘Shogake dada ana ndevu’ Safia
Eleza sifa za wahusika wafuatao.
i) Mwalimu Musi
ii) Jairo
iii) Sera
iv) Mke wa Jairo
Date posted:
May 6, 2019
-
Huku ukirejelea diwani ya Tumbo lisiloshiba fafanua matatizo yanayokumba vijana katika jamii
Date posted:
May 6, 2019
-
Ilikuwa kama vile katia saini ya kutiwa kitanzi bila ya kutambua vipengele vya sheria za utiaji huo wa kitanzi.
a)Fafanua tamathali mbili zilizotumika katika dondoo.
b)Jadili vipengele vitano vya sheria zinazorejelewa katika hadithi nzima.
c)Onyesha dhiki iliyompata mrejelewa kwa kukosa kivitambua vipengele hivyo.
Date posted:
May 6, 2019
-
Kwa kuzingatia hadithi zozote tano eleza uozo wa jamii kama unavyojitokeza katika tumbo lisiloshiba (Diwani)
Date posted:
May 6, 2019
-
“Kesho panapo majaaliwa. Kesho kama sote tutaamka…….. kama tutafungua milango ya nyumba zetu zinazosimamia juu ya ardhi hii adhimu…”
a Eleza muktadha wa dondoo hili
b Eleza sifa nne za msemaji
c) Taja mbinu zozote mbili za lugha zinazojitokeza katika dondoo hili
d Kwa kurejelea hadithi nzima onyesha namna jamii ya kisasa ina tumbo lisiloshiba
Date posted:
May 6, 2019
-
Ukengeushi huzorotesha maendeleo ya kijamii. Jadili kauli hii ukirejelea hadithi ya ‘Mkubwa’.
Date posted:
May 6, 2019
-
“Kesho kama sote tutaamka salama……….kama tutafungua milango ya nyumba zetu”….
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili
(b) Eleza tamathali mbili za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili.
(c) Eleza sifa sita za msemaji wa maneno haya.
(d) Hadithi hii inaakisi mambo mengi yanayotendeka katika bara la Afrika.
Taja mambo sita
Date posted:
May 6, 2019
-
Jadili uhalisia wa hadithi ya Tumbo Lisiloshiba katika jamii ya leo kwa kutoa hoja kumi.
Date posted:
May 6, 2019