Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Questions and Answers - Kenyaplex.com

Q&A Categories


Do you have Q&A pairs? Post them here

61049 Questions  View: All | Solved | UnsolvedSearch Results...
 • Onyesha vivumishi vya sifa katika sentensi zifuatazo. (i) Anayetaka chakula kitamu ni nani? (ii) Kiatu kirefu kimeng’oka kikanyagio. (Solved)

  Onyesha vivumishi vya sifa katika sentensi zifuatazo. (i) Anayetaka chakula kitamu ni nani? (ii) Kiatu kirefu kimeng’oka kikanyagio.

  Date posted: November 24, 2022.  

 • Tunga sentensi mbili kuonyesha tofauti kati ya maneno haya. (i) shuka (ii) suka (Solved)

  Tunga sentensi mbili kuonyesha tofauti kati ya maneno haya. (i) shuka (ii) suka

  Date posted: November 24, 2022.  

 • Eleza maana ya misemo ifuatayo. (i) kupiga domo (ii) kupiga kijembe(Solved)

  Eleza maana ya misemo ifuatayo. (i) kupiga domo (ii) kupiga kijembe

  Date posted: November 24, 2022.  

 • Bainisha vitenzi halisi katika sentensi zifuatazo. (i) Nyanchama hakufika mkutanoni (ii) Horukut amerudi kutoka masoni(Solved)

  Bainisha vitenzi halisi katika sentensi zifuatazo. (i) Nyanchama hakufika mkutanoni (ii) Horukut amerudi kutoka masoni

  Date posted: November 24, 2022.  

 • Onyesha nomino za jamii katika sentensi zifuatazo (i) Chuki baina ya jamii lazima ikomeshwe barani Afrika. (ii) Wageni watatumbuizwa na bengi ya kayamba Afrika.(Solved)

  Onyesha nomino za jamii katika sentensi zifuatazo (i) Chuki baina ya jamii lazima ikomeshwe barani Afrika. (ii) Wageni watatumbuizwa na bengi ya kayamba Afrika.

  Date posted: November 24, 2022.  

 • Onyesha kundi nomino na kundi tenzi katika sentensi hii. Nyayo za wanyama hao zimeonekana hapa. (Solved)

  Onyesha kundi nomino na kundi tenzi katika sentensi hii. Nyayo za wanyama hao zimeonekana hapa.

  Date posted: November 24, 2022.  

 • Eleza tofauti kati ya: (i) Mofimu huru (ii) Mofimu tegemezi (Solved)

  Eleza tofauti kati ya: (i) Mofimu huru (ii) Mofimu tegemezi

  Date posted: November 24, 2022.  

 • Eleza tofauti kati ya sauti /z/ na /f/ (Solved)

  Eleza tofauti kati ya sauti /z/ na /f/

  Date posted: November 24, 2022.  

 • Soma taarifa hii kisha ujibu maswali Kuna wataalamu siku hizi wanaosema kuwa jela si pahala pa adhabu bali pa matibabu. Yaani madhumuni ya kumtia mhalifu jela isiwe...(Solved)

  Soma taarifa hii kisha ujibu maswali Kuna wataalamu siku hizi wanaosema kuwa jela si pahala pa adhabu bali pa matibabu. Yaani madhumuni ya kumtia mhalifu jela isiwe kumwadhibu kwa makosa aliyofanya bali iwe kumtibu na kujaribu kumrekebisha tabia yake ili awe raia mwema. Zamani wahalifu waliadhibiwa kwa mujibu wa makosa waliyoyafanya. Mhalifu aliyefanya makosa madogo madogo alifungwa lakini mtu aliyeua naye aliuawa. Sasa wataalamu wanatuambia kuwa mhalifu akiadhibiwa anapokuwa kifunguno,basi akitoka hurejea tena kufanya uhalifu. Madhumuni ya kumtia jela iwe si kumwadhibu bali kumfunza tabia njema. Wanatuambia kuwa makosa afanyayo mhalifu yanatokana na matatizo ya jamii kwa jumla,nayo ni matatizo kama ya umaskini, msongamano wa watu, kosa afanyalo mhalifu si kosa lake pekee bali ni kosa la jamii nzima. Jitu lilizoea kuua halioni kitu kumpiga mtarimbo au rungu la kichwa na kumyang’anya kila alicho nacho. Siku hizi,jitu kama hili baadhi ya wataalamu husema lisiuawe lifungwe maisha tu. Lakini ‘kifungo cha maisha’ ni kama tunavyokijua. Muuaji hufungwa pengine miaka kumi tu kisha husamehewa muda uliobaki. Hapo tena huwa huru ama kuifichua mali aliyoiiba na kuistarehea raha mustarehe au kurejea tena kufanya uhalifu. Haya ni kinyume kabisa na mambo yalivyokuwa zamani. Aliyeua aliuawa kwa hivyo watu waliogopa kuua. Raia na pia askari waliokuwa wakiwasaka wahalifu walinusurika vifo kwani wahalifu wengine walichukua silaha za hatari kama bastola na bunduki. Sasa wale wahalifu wabaya sana – mijizi, minyang’anyi na wauaji ndio wanaotukuzwa. Magazeti huwashawishi makatili hawa na kuwapa mapesa chungu nzima waeleze maisha yao ya kikatili. Magazeti haya sasa ndiyo yanayopata wasomaji wengi. Pia wachapishaji vitabu vya hadithi zinazohusikia na uhalifu, biashara zao zinazidi kustawi. Kadhalika sinema zinazoonyesha picha za ukatili; wizi na mauji hujaa watazamaji wanaoshangilia uhalifu ufanywao. Wahalifu kwa upande mmoja wanatukuzwa na masinema vitabu na magazeti na kwa upande mwingine “haki” zao zinapiganiwa na baadhi ya wataalamu. Watu wanaowalaani wahalifu ni wale waliohasirika tu na kuteswa na wahalifu . Baadhi yao hata kulaani hawawezi kwa sababu wameshauawa,hawana tena kauli. MASWALI (a) Fupisha aya ya kwanza hadi ya tatu kwa maneno 50. Matayarisho Nakala safi (b) Fupisha aya mbili za mwisho kwa maneno kati ya 45-50 Matayarisho Nakala safi

  Date posted: November 23, 2022.  

 • Soma taarifa hii kisha ujibu maswali ifuatayo. UKANDAJI Je,unajua kuwa ukandaji wa mwili umetumika kama njia mojawapo ya matibabu toka jadi?(Solved)

  Soma taarifa hii kisha ujibu maswali ifuatayo. UKANDAJI Je,unajua kuwa ukandaji wa mwili umetumika kama njia mojawapo ya matibabu toka jadi? Watu wanaofahamika kutumia ukandaji kimatibabu toka jadi ni Wahindi,Wachina,Wagiriki,Warumi na Waafrika. Ukandaji unajulikana kuwa na manufaa makubwa kimatibabu. Mathalani,ukandaji hufungua vitundu vya ngozi. Ufunguzi huu huondoa sumu mwilini kupitia kwa utoaji jasho. Pili,ukandaji hupunguza mkazo wa misuli. Misuli ikiwa na mkazo zaidi kwa muda mrefu huleta urundikaji wa asidi. Ukandaji huondoa asidi hii,huufanya mwili kuwa mlegevu,humletea mtu uchangamfu na kuondoa uchovu. Halikadhalika,ukandaji huimarisha mzunguko wa damu mwilini kwa wepesi. Hali hii huhakikisha kuwa virutubishi vya mwili huweza kufikia viungo vyote vya mwili. Hili nalo huchangia kuzidisha uwezo wa mwili kujikinga na maradhi. Hewa safi ya oksijeni huweza pia kusambaa kote mwilini kupitia kwa uimarishaji wa mzunguko wa damu. Aidha,ukandaji wa taratibu na polepole hupunguza mkazo wa neva na kuziliwaza ukandaji wa kasi huchangamsha neva na kuimarisha utendaji kazi wake. Ukandaji unaweza kufanyiwa kiungo chochote mwili ni. Ukandaji huu huweza kuwa na matokeo mbalimbali mwilini. Mathalani,ukandaji wa njia ya chakula mwilini,hasa tumbo na utumbo,huimarisha usagaji wa chakula na kuchangia uondoaji wa uchafu na sumu mwilini. Nao ukandaji wa njia ya mkonjo hustawisha uondoaji wa chembechembe za sumu mwilini. Kwa kawaida,viganja vya mikono hutumika katika ukandaji. Viungo hivi vinapaswa kuwa na wororo. Wororo huu hupatikana kwa kutumia mafuta. Mafuta ambayo ni bora zaidi kwa shughuli za ukandaji ni ya ufuta au simsim. Matumizi ya kitu chochote kama ungaunga kinachoweza kuziba vitundu vya ngozi hayapendekezwi. Ukandaji wapaswa kutekelezwa kwa njia ifuatayo. Mtu aanzie mikono na miguu. Kisha aingie kukanda kifua,tumbo,mgongo na makalio. Hatimaye,akande uso na kichwa. Mtu anaweza kutumia kitambaa kukandia mgongo. Ni bora kutumia viganja vya mikono kukandia. Kwa njia hii,manufaa huwa maradufu. Kwanza,tutanufaika na ukandaji na wakati huo huo tutakuwa tukifanya mazoezi ya viungo. Wasioweza kujikanda,wanaweza kuomba msaada. Ni muhimu ukandaji ufuatiwe na kuoga kwa maji vuguvugu. Kwa walio na tatizo la shinikizo au mpumuko wa damu wanaweza kubadilisha utaratibu wa ukandaji. Waanzie kichwani,kisha waelekee usoni,kifuani,tumboni,mgongoni,makalioni,miguuni na kuhitimisha mikononi. Hata hivyo,ukandaji haupaswi kufanywa wakati mtu anaugua maradhi yoyote. Wanawake wajawazito nao wanatakiwa kuepuka ukandaji wa tumbo. Halikadhalika,ukandaji wa tumbo hauruhusiwi wakati mtu anaendesha,ana vidonda vya tumbo au uvimbe tumboni. Hatimaye,ukandaji haupendekezwi iwapo mtu ana maradhi ya ngozi. MASWALI (a) Ukandaji ni nini? (b) Eleza manufaa matatu ya ukandaji. (c) Ukandaji unatakiwa kutekelezwa kwa njia gani? (d) Ukandaji unatakiwa kutekelezwa na nani na kwa nini? (e) Onyesha ni lini ukandaji haupendekezwi. (f) Eleza maneno yafuatayo kama yalivyotumika: (i) ufunguzi (ii) auni (iii) maradufu (iv) maji vuguvugu (v) shinikizo la damu

  Date posted: November 23, 2022.  

 • David Mulwa, Inheritance “Lacuna represents the evil that bedevils our leaders.” With reference to David Mulwa’s Inheritance, write an essay to support this statement.(Solved)

  David Mulwa, Inheritance “Lacuna represents the evil that bedevils our leaders.” With reference to David Mulwa’s Inheritance, write an essay to support this statement.

  Date posted: November 22, 2022.  

 • Nani kuku....? Sosi poa leo .... Mate ndo! ndo! ndo!. Ukimanga hii hutaona daktari kwa miaka kumi..... Ng’ombe je? nani? ......nani!... Ni wewe.... poa basi naja...... a....(Solved)

  Nani kuku....? Sosi poa leo .... Mate ndo! ndo! ndo!. Ukimanga hii hutaona daktari kwa miaka kumi..... Ng’ombe je? nani? ......nani!... Ni wewe.... poa basi naja...... a. Je, sajili hii inapatikana wapi? b. Huku ukitoa mifano mwafaka, eleza sifa nne za sajili hii.

  Date posted: November 22, 2022.  

 • Tumia kirejeshi amba- katika sentensi ifuatayo: Jembe lililonunuliwa limepotea.(Solved)

  Tumia kirejeshi amba- katika sentensi ifuatayo: Jembe lililonunuliwa limepotea.

  Date posted: November 22, 2022.  

 • Andika katika udogo: Mbwa amekanyagwa na gari.(Solved)

  Andika katika udogo: Mbwa amekanyagwa na gari.

  Date posted: November 22, 2022.  

 • Chris Wanjala (Ed.), Memories We Lost and Other Stories“An eye for an eye can only make the whole world blind” Paying close attention to Mariatu...(Solved)

  Chris Wanjala (Ed.), Memories We Lost and Other Stories “An eye for an eye can only make the whole world blind” Paying close attention to Mariatu Kamara’s story The President, write an essay in support of this saying.

  Date posted: November 22, 2022.  

 • Sahihisha sentensi ifuatayo. Ukienda mle pao atakuweko. (Solved)

  Sahihisha sentensi ifuatayo. Ukienda mle pao atakuweko.

  Date posted: November 22, 2022.  

 • Tunga sentensi moja kubainisha tofauti kati ya maneno haya: Paka na baka(Solved)

  Tunga sentensi moja kubainisha tofauti kati ya maneno haya: Paka na baka

  Date posted: November 22, 2022.  

 • Henrik Ibsen, A Doll’s House Using Tovald Helmer for illustrations, write an essay on how one can have wrong judgement about others drawing your illustrations...(Solved)

  Henrik Ibsen, A Doll’s House Using Tovald Helmer for illustrations, write an essay on how one can have wrong judgement about others drawing your illustrations from Henrik Ibsen’s A Doll’s House.

  Date posted: November 22, 2022.  

 • Akifisha sentensi ifuatayo: mwalimu kazungu alimuuliza mwanafunzi je unataka kunidanganya kuwa ulifika shuleni mapema(Solved)

  Akifisha sentensi ifuatayo: mwalimu kazungu alimuuliza mwanafunzi je unataka kunidanganya kuwa ulifika shuleni mapema

  Date posted: November 22, 2022.  

 • Choose the correct word from those in brackets i) We were all visitors of ............. (him/his/he) ii) (All over sudden/all of a sudden) ............ there...(Solved)

  Choose the correct word from those in brackets i) We were all visitors of ............. (him/his/he) ii) (All over sudden/all of a sudden) ............ there was a loud bang on the door. iii) We had cooked ............ for lunch (fowl/foul)

  Date posted: November 22, 2022.  

 • Andika kinyume cha sentensi hii: Alipoinama nilifurahi.(Solved)

  Andika kinyume cha sentensi hii: Alipoinama nilifurahi.

  Date posted: November 22, 2022.  

 • Tambua aina za maneno katika sentensi zifuatazo: Msichana mrembo amechora haraka sana. Yeye ataenda sokoni.(Solved)

  Tambua aina za maneno katika sentensi zifuatazo: Msichana mrembo amechora haraka sana. Yeye ataenda sokoni.

  Date posted: November 22, 2022.  

 • Tia shadda ili kutoa maana mbili tofauti ya neno ‘katakata’.(Solved)

  Tia shadda ili kutoa maana mbili tofauti ya neno ‘katakata’.

  Date posted: November 22, 2022.  

 • Huku ukitoa mifano mwafaka, eleza maana ya aina zifuatazo za silabi: Silabi funge Silabi wazi Silabi mwambatano(Solved)

  Huku ukitoa mifano mwafaka, eleza maana ya aina zifuatazo za silabi: Silabi funge Silabi wazi Silabi mwambatano

  Date posted: November 22, 2022.  

 • Eleza sifa za sauti zifuatazo: /e/ /p/(Solved)

  Eleza sifa za sauti zifuatazo: /e/ /p/

  Date posted: November 22, 2022.  

 • Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali FADHILA ZA PUNDA Rita na Evelyn walikuwa marafiki wa chanda na pete kwa muda mrefu.(Solved)

  Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali FADHILA ZA PUNDA Rita na Evelyn walikuwa marafiki wa chanda na pete kwa muda mrefu. Waliishi katika mtaa wa Kibokoni jijini Mombasa. Evelyn alikuwa mwanafunzi wa masomo ya uhazili katika chuo kimoja pale mjini. Naye Rita alifanya kazi ya ukarani papo hapo mjini. Waliishi kidugu katika chumba kimoja walichopanga pale mtaani. Ingawa marafiki hawa walishirikiana kwa kila njia katika shughuli za upishi, kupiga deki, kufagia, kufua na kazi nyinginezo za nyumbani, aliyekuwa akitoa msaada mkubwa zaidi alikuwa ni Rita. Rita alikuwa na mazoea ya kutunza pesa zake vyema. Aidha alijua maana ya haba na haba hujaza kibaba. Alijua kuwa Evelyn, kama mwanafunzi, hakuwa na uwezo wa kuyakidhi baadhi ya mahitaji yake. Alijitolea sabili hata kumnunulia Evelyn nguo, viatu na vim vingine alivyohitaji. Mara nyingine ilibidi Rita kulipa kodi ya nyumba peke yake kwa vile mwenzake hangeweza kupata pesa kwa wakati. Hakuwahi hata siku moja kumkera wala kumtesa Evelyn kwa jinsi yoyote ile. Fauka ya hayo, hakuwahi kumsemesha vibaya wala kuonyesha dharau kwake. Aliamini kama wanavyosema watu kuwa dunia rangi rangile, huenda siku moja atahitaji kusaidiwa yeye pia. Siku kama hiyo atamtegemea Evelyn, mwandani wake. Evelyn alipomaliza masomo yake alikuwa na bahati ya mtende. Alipata kazi nzuri mara moja katika kampuni moja ya maffita papo hapo jijini. Lakini muda si muda, mambo ya ajabu yalianza kutokea. Baada ya kupata kazi yenye kipato kizuri, kichwa cha Evelyn kilianza kufura mfano wa kaimati. Badala ya kunisaidia mwenzake katika kazi za pale nyumbani pamoja na gharama za maisha, alifhatilia raha za jijini kwa kuamini ule msemo wa ponda raha kufa kwaja. Rita alipomwuliza alimjibu kwa ukali, “Nikusaidie nini? Sasa si kama wakati nilipokuwa mwanafunzi. Kila mtu ana pesa zake.Ala!” Rita hakumwelewa tena Evelyn.Isistoshe, alianza kumwibia Rita vitu vyake wakati alipokuwa hayupo nyubani. Mara kwa mara Rita aligundua kuwa pesa alizokuwa ameficha sehemu Fulani nyumbani zimedokolewa. Alipomwuliza, Evelyn alikujajuu, “Unafikiri mimi sina pesa? Unadhani ni wewe tu uliyeajiriwa?” Rita alizidi kushangaa, Muda wote alioishi na kumfadhili rafiki yake aliamini kuwa atamlipa mema. “Kumbe fadhila za punda ni mateke?” Alijiuliza Rita. Baada ya muda, urafiki wao ulivunjika na Evelyn akahamia mtaa wa Furaha alikoendelea na maisha yake ya starehe na ureda. Hata hivyo mambo yalianza kumwendea mrama Evelyn. Wakubwa wake kazini hawakupendezwa najinsi alivyoendesha shughuli zake pale ofisini. Mara nyingi alifika kazini akiwa amechelewa na kila wakati alitoa vijisababu mbalimbali ambavyo havikumridhisha yeyote. Aidha, alipokuwa ofisini hakufanya mengi isipokuwa kutembea kutoka ofisi hii hadi nyingine akiwasumbua watu kazini mwao. Mara kwa mara alionekana akisinzia wakati wenzake walipokuwa wakichapa kazi. Lakini lililowakera zaidi wakuu wa kampuni hiyo ya mafuta ni jambo fulani lililoanza kutendeka pale. Vitu vya watu vilianza kupoteapotea.Mara mfanyikazi huyu anapoteza saa yake, mara mwingine anapoteza pesa, mara hiki mara kile. Wakuu walipoyatupa mawazo yao nyuma wakagundua kuwa mambo haya yalianza kutendeka mara tu alipowasili Evelyn. Wakaamua kumwekea mtego. Evelyn alioshikwa kimasomaso akidokoa mkoba wa msichana mwenzake. Mkoba huo ulikuwa umeaehwa juu ya dawati kimakusudi ili kumvuta Evelyn. Evelyn alifutwa kazi papo hapo. Fauka ya hayo, alitiwa mikononi na kukabidhiwa poisi waliomtupa korokoroni. Kesho yake Evelyn alifikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kosa la wizi. Alitozwa faini ya shilingi elfu tano au kifungo cha miezi sita. Hakuwa na pesa zozote za kulipia faini hii. Akawekwa rumande. Hata rafiki mmoja hakuwa naye wa kumuauni katika wakati huo wa majaribu. Kwa bahati, Rita alisikia kuhusu kadhia hiyo.Hakupoteza muda. Akashika njia moja kwa moja hadi kituo cha polisi. Mpango ukafanywa na akamlipia. Evelyn ile faini. Evelyn alipoachiliwa hum akashangaa. “Yaani nimesamehewa ama nini?”Aliuliza.“La. Hujasamehewa.Faini uliyotozwa imelipwa na msichana yule.” Evelyn akageuka na kumwona Rita. Alimtazama kwa muda bila kujua la kusema. Mwishowe alimsogea kisha wakakaribiana polepole na kukumbatiana. Machozi yakaanza kumdondoka Evelyn, nde! Nde! Nde! Akalia kilio cha uchungu na soni. Akamwomba Rita msamaha, “Nisamehe, sikujua nililokuwa nikifanya.Nilidhani kuwa baada ya kupata kazi sitahitaji tena urafiki wako. Haya yaliyonipata yamenifunza,” alisema kwa masikitiko. “Evelyn, kijengacho mtu ni uth na tabia,” alisema Rita.“Ni kweli rafiki yangu” alitamka Evelyn, Sasa nimejitia kwenye shida.Hata kazi yangu nzuri nimeipoteza.Sina mahali pa kuishi. Itabidi nirudi kijijini kwa baba na mama. Kwaheri rafiki yangu naasante kwa yote uliyofanya.”“La! Hutaondoka”. Rita alimwambia lcwa dhati, “Tutakwenda nawe nyumbani mwangu tukaishi pamoja kama zamani. Nitayagharamia mahitaji yako yote hadi utakapopata kazi”. Basi Rita na Evelyn wakaungana tena na kuishi vizuri katika nyumba ile ile mtaani Kibokoni. Kweli akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki. MASWALI: 1. Maisha ya Evelyn na Rita yalikuwaje kabla ya Evelyn kupata kazi? 2. Kutokana na jinsi Rita alivyomtunza Evelyn, unafikiri yeye alikuwa ni mtu wa ama gani? 3. Eleza baadhi ya mambo ambayo Rita alimtendea mwenzake. 4. Baada ya kupata kazi Evelyn alikuwa mtu mkarimu. Je, unakubali?Eleza ilivyokuwa. 5. Evelyn alipokuwa mwanafunzi hakuwa na tabia ya udokozi. Unafikiri ni kwa nini alianza tabia hiyo baada ya kuajiriwa? 6. ‘Asiyefunzwa na mama hufunzwa na ulimwengu.’ Methali hii inahusianaje na Evelyn? 7. ‘Akufaaye ukiwa dhiki ndiye rafiki.’ Methali hii inahusianaje na Rita? 8. Eleza maana ya misemo ifuatayo kama ilivyotumika kwenye kifungu: (alama 3) (a) marafiki wa chanda na pete (b) enda mrama (c) jitolea sabili

  Date posted: November 22, 2022.  

 • Fill in the blanks with the most appropriate preposition i) The candidates are very good ............ languages. ii) Give us the details ............ your courses....(Solved)

  Fill in the blanks with the most appropriate preposition i) The candidates are very good ............ languages. ii) Give us the details ............ your courses. iii) The police wanted proof ........... their explanation. iv) Her performance was amazing ........... any standards

  Date posted: November 22, 2022.  

 • Explain the differences between the following sentences i) She paid him to do the work. ii) She paid him for doing the work.(Solved)

  Explain the differences between the following sentences i) She paid him to do the work. ii) She paid him for doing the work.

  Date posted: November 22, 2022.  

 • Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali. Hapo zamani za kale paliishi sungura na ndovu. Wanyama hawa waliishi baharini.(Solved)

  Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali. Hapo zamani za kale paliishi sungura na ndovu. Wanyama hawa waliishi baharini.Maulana alikuwa amewatunukia mapenzi si haba.Makazi yao yalikuwa yamepambwa yakapambika. Walitegemea matunda mbalimbali yaliyokuwa baharini kama mapera, matomoko matikitimaji na kadhalika. Siku moja usiku wa manane, maji yakaanza kupwa. Ndovu aliathirika zaidi.Alijaribu kuinama majini lakini hakuweza.Alimwita sungura amsaidie lakini sungura alikuwa ametoweka. Ndovu aliamua kwenda kumtafuta sungura.Alimtafuta hadi msituni lakini hakumpata.Alihofia kurudi baharini na hadi wa leo yumo msituni. Maswali a. Tambua utanzu na kijipera chake. b. Taja fomyula zingine mbili za kutanguliza kifungu hiki. c. Eleza umuhimu wa kijipera hiki. d. Eleza sifa za kifungu hiki. e. Eleza umuhimu wa fomyula ya Kuhitimisha

  Date posted: November 22, 2022.  

 • Rewrite the following sentences according to the instructions, given without changing the meaning. i) You are asked not to make your work dirty (Rewrite using...(Solved)

  Rewrite the following sentences according to the instructions, given without changing the meaning. i) You are asked not to make your work dirty (Rewrite using the word “dirty” as a verb) ii) I will not give you the dress unless you pay for it. (Rewrite using; on condition) iii) The book is both informative and very interesting to read (Rewrite using: Not only…but also…)

  Date posted: November 22, 2022.