-
Jadili jinsi Mambo yalivyopamba sagamoyo kutokana na mazungumzo Kati ya Hashima na Siti
Date posted:
May 1, 2019
-
Uongozi mbaya unaiathiri pakubwa Sagamoyo. Fafanua
Date posted:
April 30, 2019
-
UTENGANO: SAID. A. MOHAMMED.
4. “Kuna heri gani kuonana na kisabaluu huyu uso wa kifuu”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili
b) Eleza umuhimu wa mzungumzaji
Date posted:
April 30, 2019
-
Eleza maana ya nahau hizi?
Date posted:
April 23, 2019
-
Jadili ufaafu wa jalada la tamthilia ya Kigogo.
Date posted:
April 22, 2019
-
Mayai waziri wa maradhi na hadithi nyingine.
Adui ya mwanamke ni mwanamke. Eleza kauli hii ukirejelea hadithi ya ngome ya nafsi na uteuzi wa moyoni
Date posted:
April 19, 2019
-
Mayai waziri wa maradhi na hadithi nyingine
. “Karibu ndugu yangu waumini ni kukirimiana tunashukuru, alhamdulilahi sifa zote ni zake Maulana a)Eleza muktadha wa dondoo hili
b) Wahusika hawa walikirimiana vipi?
c) “Kukirimiana” huko kulikuwa na hasara gani?
Date posted:
April 19, 2019
-
Eleza sifa za utungaji wa kisanii.
Date posted:
April 15, 2019
-
Anwani chozi la heri Ni kinaya. Thibitisha.
Date posted:
April 12, 2019
-
Chakula cha mkulima,
ni maharage na sima
Mtazame mkulima,
hapendezi hana dhima
Bali huyu mkulima,
ndiye chanzo cha uzima
Maisha ya mkulima,
ni ya dhiki na nakama
Kibanda cha mkulima,
huvuja na kutetema
Mgongo wa mkulima,
daima umeinama
Bali huyu mkulima,
ndiye mama wa uzima
Mke wake mkulima,
si wa pambo, wa huduma
Huyu mke mkulima,
hana muda wa kusoma
Halalami mkulima,
hunywa maji ya kisima
Bali huyu mkulima,
ndiye nguzo ya uzima
Nafasi ya mkulima,
aghalabu ni ya nyuma
Magarini mkulima,
hadhi yake kusimama
Hadharani mkulima, huambiwa hana jema
Bali huyu mkulima,
ndiye nguvu ya uzima
Elimu ya mkulima,
si kusoma si kupima
Lugha yake mkulima,
si kizungu ni ya mama
Sayansi ya mkulima,
kupanda nyanya na nduma
Bali huyu mkulima,
ndiye raha va uzima
Hunyanyaswa mkulima,
ofisi akijitoma
Anabezwa mkulima,
na watu waliosoma
Akiumwa mkulima,
hata dawa wamnyima
Bali huyu mkilima.
ndiye ngao ya uzima
Huyo ndiye mkulima,
mjueni mkulima
Akigoma mkulima,
nani atakayepuma?
Namsitu mkulima, adhaniwaye wa nyuma
kumbe huyu mkulima.
ndiye chanzo cha uzima
maswali
a) Eleza dhamira ya shairi hili
b) Taja na kueleza mikondo yoyote miwili inayojitokeza katika shairi hili
c) Taja na kueleza mbinu zozote tatu za lugha zinazojitokeza katika shairi hili
d)Andika ubeti wa pili kwa lugha nathari
e) Eleza maana ya msamiati ufuatao
i)Anabezwa.
ii)Akijitoma
iii)Atakayepuma
iv) Hadhi
Date posted:
April 10, 2019
-
Taja na ueleze kwa kifupi mambo ambayo hutawala matumizi ya lugha.
Date posted:
April 10, 2019
-
Taja irabu mbili za nyuma ya ulimi.
Date posted:
April 9, 2019
-
Fafanua sehemu kuu za uandishi wa ripoti ya utafiti.
Date posted:
March 17, 2019
-
Katika Jimbo La Sagamoyo uhuru ni ndoto ambayo haijatimia dhihirisha ukweli wa Kauli hii kwa kutumia tamthilia ya kidogo by Pauline Kea
Date posted:
March 17, 2019
-
Eleza sababu za kutamba ngano usiku?
Date posted:
March 12, 2019
-
Ukirejelea tamthilia ya Kigogo,eleza jinsi nafasi ya vijana katika jamii inavyojitokeza.
Date posted:
March 12, 2019
-
Fafanua maudhui ya umenke katika riwaya chozi la heri.
Date posted:
March 9, 2019
-
Tambua shamirisho na chagizo katika sentensi ifuatayo.
Mama alipika chakula kitamu.
Date posted:
March 8, 2019
-
Sadfa imetumiwaje katika riwaya ya chozi la heri?
Date posted:
March 6, 2019
-
Eleza maana ya methali; "Kibaya chajitembeza kizuri chajiuza".
Date posted:
March 6, 2019
-
Eleza maudhui yanayodhihirika katika tamthilia kigogo
Date posted:
March 2, 2019
-
Chumba cha vijana huitwaje?
Date posted:
February 25, 2019
-
Eleza matumizi ya vipengele vya ushairi katika tamthilia ya Kigogo
Date posted:
February 24, 2019
-
Eleza hatua tano zinazofuatwa na mkusanyaji wa data ya fasihi simulizi.
Date posted:
February 23, 2019
-
Mofimu ni nini?
Date posted:
February 23, 2019
-
Swali la marudio kwa Kidato cha nne.
Date posted:
February 22, 2019
-
Toa mifano miwili ya viyeyusho.
Date posted:
February 20, 2019
-
Eleza sifa tano za Ridhaa katika chozi la heri.
Date posted:
February 20, 2019
-
(A)(i)Andika neno moja ili kuonyesha silabi inayoundwa na konsonanti pekee.
(ii)Onyesha mzizi wa neno lililopewa kualika.
Kualika
Date posted:
February 19, 2019
-
(A)Maghani ni nini?
(B)Eleza fani zifuatazo za Maghani.
(i)Vivugo.
(ii)Tondozi.
(iii)Pembezi.
(iv)Rara.
Date posted:
February 19, 2019