Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Teso District Mock - Kiswahili Paper 3 Question Paper

Teso District Mock - Kiswahili Paper 3 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2007



Jina………………………………………………… Nambari. …………………….
Shule ………………………………………………...
102/3
KISWAHILI
KARATASI 3
(FASIHI)
JULAI/AGOSTI 2007
SAA: 2 ½
WILAYA YA TESO BARAZA LA MITIHANI - 2007
Hati ya kuhitimu kisomo cha sekondari (K.C.S.E)
102/3
KISWAHILI
KARATASI 3
(FASIHI)
JULAI/AGOSTI 2007
SAA: 2 ½
• Jibu maswali MANNE pekee
• Swali la kwanza ni la lazima
• Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki yaani; Tamthilia,
Riwaya, hadithi fupi na Fasihi Simulizi.
• Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
Dharau ni maapizo!
2
Karatasi hii ina kurasa 8 zilizopigwa chapa
Watahiniwa lazima wahakikishe kurasa zote zimepigwa chapa sawa sawa na kuwa maswali yote yamo.
SEHEMU A – USHAIRI
Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuatia
Sehemu A
1. Dharau ije kwa bezo mtu kumkata pua
Iwile kamajumizo ghafula kuja muua
Dharau ni angamizo kwa wale wasotambua
Mtu humkata pua!
2. Dharau ije kwa mzo mja humuuangamiza
Kwa ufanyae vikwazo dharau ishakuweza
Kama vile mtelezo dharau hukubwatiza
Mja humuangamiza!
3. Dharau ni mwambuzo kidonda inaambuza
Kipele cha mkwaruzo machozi huja kuliza
Yazidipo matatizo mguu ukipoteza
Kidonda inaambuza!
4. Dharau kwa kazi twezo hwenda ukaipoteza
Haikupi kishikizo wewe na kazi kucheza
Malipo yako na tuzo kazini hukufukuza
Hwenda ukaipoteza!
5. Dharau mfwatilizo inangoja kumaliza
Haiwi haiwi hizo kuwa kutakutimiza
Dharau si ya chetezo kinga haitapatiza
Inangoja kumaliza!
6. Dharau si maliwazo kukaa kizungumza
Na nyakati zipitazo wewe uli ukichuza
Dharau ni fumanizo ghafla huja kupaza
Dharau ni maliwazo!
7. Dharau ni mabwagizo maisha kudidimiza
Hukuvunjia uwezo kutenda na kufanyiza
Na mingi kwako mizozo kote imekuzingiza
Dharau ni mabwagizo!
8. Dharau ni maapizo laana ya kuapiza
Hupungukiwa mawazo na watu hukupuuza
Muokwako matutizo na kuzama na kuviza
9. Dharau ni matelezo Chini yatakubwagiza
Na hakuna mazuizo telezi ukiteleza
Purr chini hunasazo kuinuka hutaweza
Dharua ni matelezo!
10. Dharau ni hitimizo wasia wangu chukua
Ninafunga beti hizo kumi niloziambua
Ikimbie ndugu guzo dharau inaumbwa
Dharau ni hitimizo!
Maswali
(a) Lipe shairi hili kichwa mwafaka. (Alama 1)
(b) Fafanua maudhui ya shairi hili, (Alama 5)
(c) Onyesha muundo wa shairi hili (Alama 3)
(d) Taja na ueleze tamathali tatu za lugha zilizotumika katika shairi hili. (Alama,6)
(e) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi:
(i) bezo (ii) mzo (iii) mwambuzo
(iv) fumanizo (v) kuapiza, (Alama 5)
TAMTHILIA
KITHAKA WA MBERIA: KIFO KISIMANI
2. Eleza kwa tafsili mikakati aliyotumia mtemi Bokono katika kudumisha na kuendeleza utawala wake. (alama 20)
RIWAYA
Z. BURHANI: MWISHO WA KOSA
3. “Sikiliza…….. umesahau hivi juzi ile safari ya yule msichana? Jina lake nani vile ….. mpaka
Marekani. Tena kwa matumizi tu, na pesa kiasi gani vile alizochukua? Nina hakika wenye
magazeti wangependa mtu awadokezee habari hizo”.
a) Fafanua muktadha wa dondoo hili (alama 4)
b) Nia ya msemaji kutoa maneno hayo ni ipi? (alama 2)
c) Fafanua maudhui yoyote matatu kama yanavyojitokeza kwenye dondoo hili. (alama 6)
d) Eleza sifa zozote nne za msemaji. (alama 8)
HADITHI FUPI
K.W WAMITILA: Mayai waziri wa maradhi
Jibu swali la 4 au 5
4. Jadili matumizi ya jazanda katika hadithi ya mayai waziri wa maradhi. (alama 20)
5. a) Fafanua mtindo na muundo wa hadithi ya ngome ya nafsi. (alama 8)
b) Eleza maudhui yanayojitokeza katika hadithi hii. (alama 10)
c) Andika methali mbili zinazoweza kutumika kueleza mafunzo ya hadithi hii. (alama 2)
FASIHI SIMULIZI
Jibu swali la 6 au 7
6. a) Eleza kikamilifu sifa zozote tano za mtambaji katika fasihi simulizi (alama 10)
b) Fasihi simulizi aghalabu hutambulika kutokana na sifa zake kuu. Jadili. (alama 10)
7. a) Ngomezi ni nini? (alama 2)
b) Eleza umuhimu wa ngomezi katika jamii. (alama 4)
c) Methali zina umuhimu gani katika jamii? (alama 10)
d) Eleza jukumu la fomula za ufunguzi katika hadithi. (alama 4)






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers