Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Got a question or eager to learn? Discover limitless learning on WhatsApp now - Start Now!

Kisw 311: Mbinu Za Utafiti Katika Kiswahili Question Paper

Kisw 311: Mbinu Za Utafiti Katika Kiswahili 

Course:Bachelor Of Education Arts

Institution: Egerton University question papers

Exam Year:2016



KISW 311
EGERTON UNIVERSITY
UNIVERSITY EXAMNATIONS
REGULAR - MORO CAMPUS
FIRST SEMESTER. 2016/2017 ACADEMIC YEAR
THmD YEAR EXAMINATION FOR DEGREE OF BACHELOR OF ARTS AND
BACHELOR OF EDUCATION (ARTS)
KISW 311: MBINU ZA UTAFITI KATIKA KISWAHILI
STREAM: BA AND B.ED (ARTS) rrnn: 2 HOURS EXAMINATION SESSION: DECEMBER YEAR: 2016

i. Jibu maswali Matatu pekee. Swali la Kwanza ni la lazima.
ii. Usiandike chochote kwenye karatasi ya maswali.
Swali la Kwanza
Soma maelekezo yafuatayo ya utafiti wa kidhanifu kisha uyatumie kujibu maswali yanayofuata.
Kumebainika kuwa na matumizi mabaya ya viåmbishi ngeli katika maandishi ya Kiswahili cha wanafunzi wengi wa gatuzi lako. Kunahitajika mikakati ya dharura kuzuia mwelekeo huu. Kama msomi umeazimia kufanya utafiti ili kuzipa Shule mwongozo wa kitaaluma wa kulishughulikia swala hili.
a) Unda mada inayofaa utafiti huu. (Alama 3)

"Transforming Lives through Quality Education " EgertonUniversity is ISO 9001:2008 Certified
Page 1 of 2

b) Buni suala la utafiti kwa utafiti wako. (Nama 4)
c) Andika madhumuni yoyote mawili ya utafiti huo. (Alama 2)
d) Bainisha nadhariatete utakazodhamiria kuthibitisha nyanjani. (Alama 2)
e) Eleza vibadiliki vyovyote viwili katika utafiti wako. (Alama 2)
f) Ukitoa udhaifu wa kila mojawapo, fafanua mbinu zozote mbili utakazotumia kukusanyia
data ya utafiti huu.
g) Kwa hoja nne, fafanua umuhimu wa utafiti huo kwa wasomi.
h) Eleza mbinu ya utafiti mwafaka itakayofaa utafiti huu. (Nama 6) (Alama 4)
(Alama 3)
SWaIi la Pili
Huku ukirejelea maswala yoyote matano yanayofaa kuzingatiwa na mtafiti katika kubuni muundo wa sampuli, jadili masiala manne yanayosababisha upendeleo katika mchakato wa utafiti. (Alama 22)
Swali la Tatu
Fafanua dhima ya mapitio ya maandishi ya awali katika utafiti. (Alama 22)
Swaii la Nne
Wadili vipengee vyovyote vinavyotumiwa kupima ubora wa utafiti. (Alama 22)
Swali la Tano
Utafiti ni mchakato wa kiutaratibu. Thibitisha ukweli wa rai hili kwa kurejelea wanayopendekeza Mauch na Birch (1998: 1 10). (Alama 22)
Swali la Sita
Pambanua aina zozote saba za utafiti. (Alama 22)

"Transforming Lives through Quality Education ¥ertonUniversity is ISO 9001:2008 Certified
Page 2 of 2






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers