Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Narok District Mock- Kiswahili Paper 3 Question Paper

Narok District Mock- Kiswahili Paper 3 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2007



Jina………………………………………………… Namba yako …………………….
Shule………………………………………………...
102 / 3
KISWAHILI ( FASIHI)
KARATASI 3
JULAI \ AGOSTI 2007
SAA 2 ½
MTIHANI WA MWIGO WILAYA YA NAROK - 2007
Cheti cha Elimu ya Sekondari Kenya
102 / 3
KISWAHILI ( FASIHI)
KARATASI 3
JULAI \ AGOSTI 2007
SAA 2 ½
MAAGIZO KWA MTAHINIWA
• Jibu maswali MANNE pekee.
• Swali la KWANZA ni la LAZIMA
• Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki, yaani, Tamthilia,
Riwaya, Hadithi fupi na fasihi simulizi.
• Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
2
Karatasi hii ina kurasa 4 zilizopigwa chapa
Watahiniwa lazima wahakikishe kurasa zote zimepigwa chapa sawa sawa na kuwa maswali yote yamo.
USHAIRI
1. Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata
Kaka: Kusoma nilikosoma, kambiwa sipati kazi,
Yapata mwaka mzima, nategemea shangazi,
Wasiojuwa husema, ‘ sababu sina ujuzi,’
Huno uhaba wa kazi, mesababishwa ni wake.
Dada: Mbona watuingilia, kaka acha ubaguzi,
Likukeralo twambia, tulijuwe waziwazi,
Au unalochukia ni wake kufanya kazi?
Mambo ya siku hizi,watu ni bega kwa bega.
Kaka: Siwangilie kwa nini, nanyi mwatukopa kazi
Kwani tokea zamani, hazikuwa shida hizi,
Mtu kitoka shuleni, kibaruwa si tatizi,
Leo hatupati kazi, kisa nyinyi wanawake
Dada: Hapo kaka hujasema, kuwa wake ndiyo chanzi,
Chanzo cha hii nakama, waume kukosa kazi,
Bure mwatupa lawama, wenyewe mna ajizi,
Mtindo wa siku hizi, watu ni bega kwa bega.
Kaka: Hayo unayotamka, yote niya upuuzi,
Mumetoroka kupika, kazi yenu toka enzi,
Bilashi mwahangaika, kushabihi vijakazi,
Sasa hatupati kazi, kisa nyinyi wanawake.
Dada; Mbona wafanya ukali, ishakuwa ni chukizi?
Hata na yangu kauli, umekuwa husikizi,
Nisemaye ni halali,ukweli uliowazi,
Mtindo wa siku hizi, watu ni bega kwa bega.
Kaka: Yana uhalali gani, mbona basi huelezi?
Kipita maofisini, mumejaa kama inzi,
Mwataka tuwe mekoni, wala halitupendezi,
Na nje hakuna kazi, kisa nyinyi wanawake.
Dada: kakangu una matata, kuyaelewa siwezi,
Wasema unamopita, wambiwa hakuna kazi?
Na sisi wake twapata, haraka pasi ajizi,
Sababu siku hizi, watu ni bega kwa bega.
Kaka: Sisi kazi hatupati, wengi wetu ni mijizi,
Elanyi muna bahati, mabosi hawawaizi,
Hampotezi wakati, ni kidogo pingamizi,
Nasi hatupati kazi, kisa nyingi wanawake..
Dada: kakangu wanichekesha, hadi sina kizuizi,
Vipi lakukasirisha, sisi tukifanya kazi?
Hujui ndivyo maisha, yaendavyo siku hizi?
Mtindo wa siku hizi, watu ni bega kwa bega.
Kaka: Huna haja ya kucheka, nisemayo si upuzi,
Kazi inayojulika, yenu ni kukuna nazi,
Kisha mwenda zianika, mukaziuze takizi,
Leo hatupati kazi, kisa nyinyi wanawake.
Dada: Yalikuwa ni ya kale, kuuza chicha za nazi,
Ela leo twenda mbele, na nyuma hatujibanzi,
Hakuna aliyelele, kushiriki usingizi,
Kwani mambo siku hizi, watu ni bega kwa bega.
Kaka: kulla kitu mwakitaka, kiwe chenu siku hizi,
Ishakuwa na miaka, pia mwataka ihozi,
Nasikia mwatamka, mwaka huno wa ledizi,
Mwisho mutataka myezi, iwe yenu wanawake.
Hai mana kubishana, nikashabihi mkizi,
Mengi niliyoyanena, yafanyie uchunguzi,
Iwapo tutafanana, yupi taleya vizazi?
Sisi hatupati kazi, hadi murudi mekoni.
Dada: Baba mbele mama nyuma, yamekuwa simulizi,
Muradi sote twasoma, soteni tuwe walezi,
Wake haturudi nyuma, tunataka mapinduzi,
Maisha ya siku hizi, watu ni bega kwa bega.
MASWALI
a) Lipe shairi hili kichwa mwafaka. (Alama 2)
b)Dada anatoa sababu gani ya wanawake kuajiriwa maofisini? (Alama2)
c) Kaka anataja sababu zipi za wanaume kukosa kuajiriwa kazi? (Alama2)
d) Eleza umbo la shairi hili (Alama3)
e)Dondoa na ueleze mifano miwili tofauti ya uhuru wa kishairi katika shairi (Alama4)
f) Kwa mujibu wa shairi hili, kazi za wanawake ni zipi? (Alama2)
g) Eleza ubeti wa mwisho kwa maneno yako mwenyewe (Alama2)
h) Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika shairi. (Alama3)
(i) Kulla
(ii) Nakama
(iii) Ajizi
TAMTHILIA
KITHAKA WA MBERIA: KIFO KISIMANI
Jibu swali la 2 au la 3
2. Eleza jinsi maudhui ya ujinga yalivyodhihirishwa kwenye tamthilia kifo kisimani na wahusika
wafuatao: (Alama20)
a) Kaloo
b) Mtemi Bokomo
c) Gege
d) Askari
e) Zigu
3. “ ……. Siyo uongozi wangu! Kamwe siyo uongozi wa Mtemi Bokomo! Niwaruhusu
watokomeshwa. Watakomeshwa wakome kama walivyokoma kunyonya matiti ya mama zao.
a) Eleza muktadha wa maneno haya (Alama 5)
b) Taja mbinu za lugha zilizotumiwa katika kifungu hiki huku ukitoa mifano mwafaka
c) Taja na ueleze sifa zozote tano za mhusika nyalwe. (Alama5)
4. RIWAYA
MWISHO WA KOSA. Z. BURHANI
“ Kuna waliosoma mabuku, kuna waliosoma vitabu na kuna waliosoma maisha- nafikiri inategemea
kile kipimo cha elimu na namna gani mtu anavyoitumia elimu yake”
Maswali
Eleza kwa tafsili muktadha wa dondo hili na ufafanue aina za elimu. Eleza taaluma na
umuhimu.
(alama20)
HADITHI FUPI
K.W Wamitila : Mayai waziri wa Maradhi
5. a) Eleza namna wanawake walivyochorwa katika hadithi zifuatazo:
i) Uteuzi wa moyoni (Ryya Timammy) (alama4)
ii) Ngome ya nafsi (Clara Momanyi) (alama7)
b) i) Eleza sifa zozote tano za mhusika mayai waziri wa maradhi. (alama5)
ii) Taja tabia zozote nne za mhusika mzee savalanga. (alama4)
FASIHI SIMULIZI
Jibu swali la 6 au la 7.
6. a) Mighani ni nini? (alama2)
b) Eleza tofauti kati ya wahusika Jagina na Jahili (alama4)
7
c) Taja sifa nne za mighani (alama2)
d)Maghani ni nini? (alama2)
e) Eleza fani zifuatazo za maghani (alama8)
(i) Vivugo
(ii) Tondozi
(iii) Pembezi
(iv) Rara
7. a) Eleza maana ya neno ULUMBI (alama2)
b) Bainisha sifa tisa ( 9 ) za mlumbi. (alama18)






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers