-
(a) Fafanua fani zifuatazo za fasihi simulizi (i)Ngano za mtanziko (ii) Mazingara (iii)Kifunga nyama (b) Umeombwa kusimulia darasani mughani wa Fumo Liyongo, eleza namna utakavyofanikisha uwasilishaji wako.
Date posted:
April 18, 2018
-
Eleza maana ya neno ulumbi.
Date posted:
April 18, 2018
-
Kwa kutoa mifano yoyote Kumi, fafanua matumizi ya nyimbo katika Tamthilia ya Kigogo.
Date posted:
April 13, 2018
-
Taja na ueleze vipera vyovyote vitano vya utanzu wa hadithi
Date posted:
April 13, 2018
-
Eleza maana ya hurafa.
Date posted:
April 12, 2018
-
Taja aina za wahusika katika fasihi simulizi.
Date posted:
April 12, 2018
-
Eleza dhima ya fasihi simulizi.
Date posted:
April 12, 2018
-
Taja Vipengele muhimu Katika uwasilishaji wa fasihi simulizi.
Date posted:
April 12, 2018
-
Eleza maana ya semi
Date posted:
April 11, 2018
-
Eleza maana ya Ngomezi.
Date posted:
April 11, 2018
-
Fafanua aina zozote kumi za migogoro ijitokezayo katika tamthilia ya kigogo
Date posted:
April 10, 2018
-
Eleza umuhimu wa hadithi.
Date posted:
April 9, 2018
-
Maudhui ya elimu katika Kidagaa.
Date posted:
April 8, 2018
-
Fafanua miundo yoyote saba ya silabi za Kiswahili
Date posted:
April 7, 2018
-
Jadili maudhui ya tamaa katika tamthilia ya Kigogo.
Date posted:
April 6, 2018
-
Taja na ueleze aina mbili za usikilizaji.
Date posted:
March 29, 2018
-
Uakifishaji ni nini?
Date posted:
March 29, 2018
-
Mawasiliano ni nini?
Date posted:
March 29, 2018
-
Misimu ni nini?
Date posted:
March 27, 2018
-
Tenga viambishi tamati katika neno: kupiganishia
Date posted:
March 26, 2018
-
Je, ni sababu zipi zilizopelekea kusanifishwa kwa kiswahili?
Date posted:
March 23, 2018
-
Asili ya lugha ya Kiswahili
Date posted:
March 22, 2018
-
Toa maana mbili ya neno kinyonyoke.
Date posted:
March 20, 2018
-
Taja lahaja za Kiswahili na mahali zinakozungumzwa.
Date posted:
March 4, 2018
-
Eleza umuhimu wa sajili.
Date posted:
March 4, 2018
-
Taja mambo yoyote yanayoathiri matumizi ya lugha.
Date posted:
March 4, 2018
-
Nini maana ya Isimu Jamii?
Date posted:
March 4, 2018
-
a) Badilisha sentensi ifuatayo iwe katika hali ya kuamuru katika wingi.
Njoo hapa.
b)Tunga sentensi yenye kitenzi kishirikishi kipungufu.
c) Yakinisha sentensi ifuatayo.
Asingepigiwa kura, asingekuwa rais wa Kenya.
d) Unganisha sentensi zifuatazo kwa kutumia kiunganishi mwafaka.
Mtoto alikula sana.
Mtoto hakushiba.
e)Tunga sentensi moja ukitumia kihisishi na nomino maalum.
f)Taja aina mbili za mofimu na utolee mfano mmoja mmoja.
g) Tumia amba rejeshi katika sentensi ifuatayo:
Mchezaji ninayempenda ni Messi.
h)Taja sauti mbili za nazali.
i) Andika katika msemo wa taarifa.
Naapa ya kwamba nitatumikia wananchi wa Kenya na nitakuwa mwaminifu, Rais Mteule alisema.
Date posted:
March 4, 2018
-
a) Onyesha vishazi katika sentensi ifuatayo.
Uchaguzi uliofanywa nchini Kenya ulikuwa wa amani.
b) Bainisha aina za shamirisho katika sentensi:
Shule nzuri ilijengewa wanafunzi kwa matofali.
c) Eleza sifa mbili za sentensi ambatano na utoe mfano mmoja.
d) Unda nomino kutokana na vitenzi vifuatavyo:
-Tafakari:.
-Sujudu:
e) Eleza maana ya chagizo na utunge sentensi moja kuonyesha maana yake.
Date posted:
March 4, 2018
-
Swali hili linahitaji kubainisha mbinu ambazo mwalimu atazitumia anapofunza ili kumrekebisha mwanafunzi asiyeweza kutamka lugha ya pili ipasavyo.
Date posted:
March 2, 2018