Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Sotik District Mock - Kiswahili Paper 3 Question Paper

Sotik District Mock - Kiswahili Paper 3 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2011



Jina: …………………………………………………………………… Nambari: ………...………
Shule: ………………………………………………………………. Sahihi ....................................
Tarehe: …………….....................................................................……
102/3
KISWAHILI
FASIHI YA KISWAHILI
KARATASI YA 3
JULAI/AGOSTI 2011
MUDA: SAA 2 ½
Hati ya Kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya.( K.C.S.E)
Kiswahili
Fasihi
MAAGIZO
• Jibu maswali manne pekee katika kijitabu cha majibu ulichopewa
• Swali la kwanza ni lazima
• Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki yaani: Riwaya, Hadithi
fupi, Fasihi simulizi na ushairi.
• Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
Karatasi hii ina kurasa 4 zilizopigwa chapa. Watahiniwa ni lazima waangalie kama kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.
SEHEMU YA A: THAMTHILIA
KIFO KISIMANI: Kithaka wa Mberia
LAZIMA
1. “Bahati nasibu inapomteremkia mtu mara nyingi uhalisi huonekana……”
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (al.4)
(b) Onyesha bahati inayorejelewa. (al.4)
(c) Kwa kutoa mifano mwafaka, jadili dhana ya usaliti tamthiliani. (al.12)
SEHEMU YA B: RIWAYA
S.A Mohamed : UTENGANO
Jibu swali la 2 au la 3
2. “Pesa iweke mbele. Pesa mwanzo. Sisi tuna msemo wetu. Watose. Ndio, watose maana sisi
tumeshatoswa.”
(a) Liweke dondoo hili katika muktadha wake. (al.4)
(b) Eleza mawaidha mawili ambayo msemaji alimpa msemewa katika muktadha huu. (al.4)
(c) Eleza maana ya “sisi tumeshatoswa” kwa kurejelea riwaya ya utengano. (al.12)
3. Thibitisha ufaafu wa methali “Majuto ni mjukuu” ukirejelea riwaya ya utengano. (al. 20)
SEHEMU YA C : HADITHI FUPI
MAYAI WAZIRI WA MARADHI NA HADITHI NYINGINE.
Jibu swali la 4 au la 5
4. ‘Mnavyojua vizuri na yote hayo si kweli. Hata wengine wenu mmekuwa sungura. Kwani wewe Abdala ulikuwa humfuatifuati, si hata ulimposa? Nyoo! Basi haifai hata kama hamtampa kura si vizuri kumtukana.’
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (al.4)
(b) Eleza ukweli kuhusu mrejelewa katika dondoo. (al.2)
(c) Taja na utoe mfano wa mbinu yoyote ya lugha ambayo imejitokeza katika dondoo. (al.2)
(d) Jamii inayorejelewa katika hadithi husika ilisheheni maovu makubwa. Fafanua kauli hii. (al.12)
5. Kwa kurejelea diwani ya Mayai Waziri wa Maradhi na hadithi nyingine, fafanua athari za uongozi
barani afrika. (al.20)
SEHEMU YA D: USHAIRI.
Jibu swali la 6 au la 7
6. SHAIRI
Alipokwenda kwao, mamaye alimwambia
Nipa fedha au nguo, nataka kwenda tumia!
Nikosapo hivi leo, nipa kisu tajitia !
Huzunguka akilia kwa maana ya uketo.
Ndipo mamaye kawaza, pamwe na kuzingatia,
Fedha zako umesoza, na leo zimekwisha,
Kisu sikukukataza, twaa upate jitia!
Mbele zangu n’ondokea! Wende na ukiwa wako!
Ulipogeuka nondo, nguo ukazingilia,
Kakaka kwa vishindo, usisaze hata moya,
Leo wanuka uvundo, wambeja wakukimbia!
Mbele zangu n’ondokea! Wende na ukiwa wako.
Ukijigeuza nyama, kama Simba ukilia,
Watumwa ukawaegema, ukawala wote pia,
Pasi kuona huruma, kutoa wahurumia,
Mbona hukuzingatia? Wende na ukiwa wako!
Si mimi naliokupa, ukata huo sikia !
Kwamba utakuja hapa, nipate kuondolea,
Naapa thama, naapa, sina la kukutendea!
Mbele zangu n’ondokea ! Wende na ukiwa wako !
Tamati nalikomile, ni hayo nalokwambia,
Hapahitaji kelele na kujirisha mabaya
Na kwamba yakutukie, sema yapate n’elea !
Zidi radhi kuniwea ! wende na ukiwa wako !
Maswali
(a) Lipe shairi hili anwani mwafaka. (al.2)
(b) Ni maudui gani yanayojitokeza katika shairi hili. (al.4)
(c) Taja na ueleze tabia za mnenewa katika shairi hili. (al.4)
(d) Mshairi ametumia uhuru wa utunzi. Taja sehemu mbili alikotumia uhuru huo. (al.4)
(e) Eleza umbo la shairi hili. (al.4)
(f) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi :- (al.2)
(i) Uketo
(ii) Ukata
FASIHI SIMULIZI
7. (a) Fafanua dhana hizi za fasihi simulizi.
(i) Nyiso
(ii) Mbolezi
(iii) Bembelezi (al.6)
(b) Eleza tofauti kati ya methali na vitendawili. (al.4)
(c) (i) Eleza sifa mbili za methali (al.4)
(ii) Eleza sifa mbili za vitendawili (al.4)
(d) Ni nini umuhimu wa methali? (al.2)






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers