Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Kwanza District Mock- Kiswahili Paper 3 Question Paper

Kwanza District Mock- Kiswahili Paper 3 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2010



102/3
KISWAHILI (FASIHI)
KARATASI 3
JULAI/AGOSTI 2010
SAA 2 ½
MITIHANI YA UTATHMINI WA PAMOJA, WILAYA YA KWANZA- 2010
Hati Ya Kuhitimu Kisomo Cha Sekondari Kenya (K.C.S.E.)
102/3
KISWAHILI FASIHI
KARATASI 3
JULAI/AGOSTI 2010
SAA 2 ½
1. Jibu maswali manne pekee.
2. Swali la kwanza ni la lazima.
3. Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki, yaani
tamthilia, Riwaya, Hadithi fupi na fasihi simulizi.
4. Usijibu maswali mawili kutoka katika sehemu moja
Karatasi hii ina kurasa 4 zilizopigwa chapa
Watahiniwa wanastahili kuona kuwa maswali yote yako na hakuna yaliyooachwa.
HADITHI FUPI – Mayai Waziri wa Maradhi na hadithi Nyingine (Mhariri K.W. Wamitila)
1. LAZIMA
Kwa kurejelea Hadithi ya mkimbizi, eleza:
a) Athari za vita vya kikabila (Alama 10)
b) Matatizo yanayowakumba wakimbizi (Alama 10)
2. USHAIRI
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Sahiba umenisema , kwa mchana na laili,
Munaondoa lazima, muenendo wa kiasili,
Kujenga ulipohama, mtu huaje aili,
Kupewa usikubali, wajataka usipewe.
Wajataka usipewe,kupewa usikubali,
Haiwi mtu mwanawe,na pia asimjali,
Ulikataa mwenyewe, kwa ghadhabu na ukali,
Kupewa usikubali, wajataka usipewe.
Wajataka usipewe, kupewa usikubali,
Ndipo wewe ushukiwe, ukajifanya mkali,
Na sitaki uambiwe, mtu asije kwa hili,
Kupewa usikubali, wajataka usipewe.
Wajataka usipewe, kupewa usikubali,
Kwani ulihama wewe, kugura hapo mahali,
Enenda sinisumbuwe, siniudhi yangu hali,
Kupewa usikubali, wajataka usipewe.
Wajataka usipewe, kupewa usikubali,
Na hili langu ujuwe , kwangu hili ni jamali,
Siachi ninga kwa mwewe, wala siwezi badili
kupewa usikubali, wajatoka usipewe.
Wajataka usipewe, kupewa usikubali,
Na hapa ndiyo mwishowe, tamati shairi hili,
Kaa usinizuzuwe, nasuburi filihali,
Kupewa usikubali, wajataka usipewe.
Na Said Karama
Maswali
a) Andika kichwa mwafaka cha shairi hili. (Alama 2)
b) Mwandishi anadhamiria nini katika shairi hili? (Alama 4)
c) Hili ni shairi la aina gani? Eleza (Alama 4)
d) Ni methali gani inayoafiki maelezo katika ubeti wa kwanza? (Alama 2)
e) Ni nini maana ya kifungu “Kupewa usikubali, wajataka usipewe“ (Alama 2)
f) Andika ubeti wa mwisho katika lugha nathari. (Alama 4)
g) Bainisha maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika shairi. (Alama 2)
i) Sahiba
ii) Laili
3. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Falaula ngalijua, singalikuwa kijana,
Kwa sababu sikujua, kajipata mvulala,
Mengi mambo nikajua, nikashinda wasichana,
Kweli ujana ni moshi, ukienda haurudi.
Mwili wangu kabadilli, toto hadi utu uzima,
Sauti yangu kabadili, nikajiola mzima,
Kakiuka maadili, dunia nikaizima,
Kweli ujana moshi, ukienda haurudi.
Masikiongu katonga, herini nikavalia,
Nywele yangu nikasonga, na mikufu kuvalia,
Video pia runinga, tazama bila tulia,
Kweli ujana ni moshi, ukienda haurudi.
Malaika kapata, moyo wangu kapambika,
Jina lake kaloreta, mie wangu malaika,
Penzi langu kalipata,mambo mengi katendeka,
Kweli ujana ni moshi, ukienda haurudi.
Moyongu kausumbua, nilipomtia mboni,
Penzi lanisumbua, aingiapo moyoni,
Sautiye kazindua, yatoa nyoka pangoni,
Kweli ujana ni moshi, ukienda haurudi.
Penzi lake kalionja, kwangu likawa asali,
Nikawa kionjaonja, kuliwasha kawa kali,
Vitabungu nikakunja, navyo kavitupa mbali,
Kweli ujana ni moshi , ukienda haurudi.
Mzigo kabebesha, ukamwachisha skuli,
Mashakani kaniingisha, nikawa sasa silali,
Kulisaka suluhisho, likawa sasa ghali,
Kweli ujana ni moshi, ukienda haurudi.
Majuto nikayapata, kwa matendengu awali,
Mifano nikaipata, Yakimwagika yazoli.
Na Oncharo P. Wycliffe
SHAIRI LA B
Mhariri nipe fursa, nifichue jambo hili,
Nipige wengi msasa, nakusihi tafadhali,
Ukweli wajue sasa, wamakinike ki hali,
Samaki pale barini,kweli huwa si mmoja.
Nawajuza mahawara, pale walipo hakika,
Si ya neni kihasira, ukweli nautamka,
Wayaepuke madhara, wazidi kumakinika
Samaki pale barini, kweli huwa si mmoja.
Dunia imegeuka, waja leo wana shani,
Wazidi kuhangaika, watatizika moyoni,
Utesi umeshazuka, mashambani na mijini,
Samaki pale barini, kweli huwa si mmoja.
Mahaba yakigeuka, hakika huwa ni dhiki,
Ugomvi uje kuzuka, uharibu urafiki,
Wakosane washirika, wapigane kila mwezi,
Samaki pale barini, kweli si mmoja.
Lakini sasa tengeni, vigogo niwasaili,
Iwapo ni hayawani,mpungufu kiakili,
Unisamehe sabini, kwa kosa moja kwa kweli,
Samaki pale barini kweli huwa si mmoja.
Hakika huwa si vyema, kibaya kukimiliki,
Mchongaji nayasema, natangaza uhakika,
Mtu mate huyatema, iwapo hayamezeki,
Samaki pale barini, huwa si mmoja.
Nafumbua fumbo wazi, mnielewe vizuri,
Nafasili ya mapenzi, yalokumbwa nazo zari,
Yalofitinika wazi, hapo ndipo nashauri,
Samaki pale barini, huwa si mmoja.
Na Petro Lubale Wa Akungwi
Maswali
a) Linganisha shairi la A na B kwa upande wa maudhui. (Alama 6)
b) Eleza muundo wa shairi la A (Alama 4)
c) Toa mifano ya uhuru wa utunzi uliotumiwa katika shairi la B. (Alama 2)
d) Andika ubeti wa nne wa shairi la A katika lugha nathari. (Alama 4)
e) Eleza msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika mashairi haya. (Alama 4)
i) Nikajiola
ii) Mzigo kambebesha
iii)Shani
iv) Zari
RIWAYA S.A. MOHAMED: UTENGANO.
4. Utengano ni anwani mwafaka wa Riwaya hii ya S.A. Mohamed. Kwa kurejelea riwaya ya utengano,
eleza sababu zilizochangia hali mbalimbali za utengano. (Alama 20)
5. “Usione kwenda mbele kurudi nyuma si kazi“ Kwa kurejelea wahusika mbalimbali wa riwaya ya
utengano, eleza ufaafu wa methali hii. (Alama 20)
TAMTHILIA : KITHAKA WA MBERIA: KIFO KISIMANI
6. “Nilibadilika na kuwa mkisi! Nilichukua gogo la mwangati .....................................“
a) Eleza muktadha uliosababisha dondoo hili (Alama 4)
b) Bainisha tamathali ya usemi iliyotumika katika dondoo hili. (Alama 6)
d) Je, Msemaji na wenzake walichangia vipi katika kudumisha utawala wa mtemi Bokono?
(Alama 12)
FASIHI SIUMULIZI
7.a) Eleza mbinu ambazo mtafiti wa fasihi simulizi hutumia katika kukusanya data ya fasihi simulizi
(Alama 10)
b) Nyiso ni nini? (Alama 2)
c) Fafanua sifa zozote nne za nyiso. (Alama 8)
MWISHO






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers