Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Nakuru District Mock - Kiswahili Paper 2 Question Paper

Nakuru District Mock - Kiswahili Paper 2 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2011



Jina………………………………………………… Namba yako …………………….
Sahihi:………………………………………………... Tarehe…………………………..
102/2
KISWAHILI
Karatasi ya 102/2
LUGHA
Julai / Agosti - 2011
Muda: Saa 2½
MTIHANI WA MWIGO WA WILAYA YA NAKURU –
2011
MAAGIZO
• JIBU MASWALI YOTE
KWA MATUMIZI YA MTAHINI PEKEE
(1) UFAHAMU
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
Janga la matumizi ya dawa za kulevya limetanda kila pembe ya janibu. Watu wengi wamepoteza
maisha yao, uchumi wa nchi ukadhoofika misingi ya serikali ikatetemeka na maisha ya wanadamu wengi yamo hatarini.
Dawa za kulevya hutumiwa na watu wa hali mbalimbali kama vile wazee, vijana, matajiri, maskini, wanawake na wanaume. Zaidi ya hayo, ndoa nyingi zimevunjika na kusababisha kuongezeka na kusambaa kwa ugonjwa wa ukimwi miongoni mwa maafa mengine.
Nchi ya Kenya haijaepukana na mkasa huu. Visa vya watu wanaotumia dawa za kulevya
vinaongezeka kila uchao. Wale ambao wameathirika zaidi ni vijana. Kwa sasa, la muhimu ni
kukabiliana na mkasa huu ambao unatisha kuangamiza vizazi vya sasa na vijavyo.
Hivi karibuni kumekuwa na visa vingi vya ukosefu wa nidhamu katika shule nyingi humu nchini.
Utovu wa nidhamu ambao umesababisha vifo , kuharibiwa kwa mali ya mabilioni ya pesa miongoni mwa maafa mengine yametokana na ongezeko la matumizi ya dawa za kulenya miongoni mwa wanafunzi. Baadhi ya dawa za kulevya ambazo hutumiwa sana na wanafunzi ni kama vile tembe za aina mbalimbali, sigara, bangi, miraa, kubere na zingine mbazo zinaingia nchini kutoka nchi za nje kama heroini, kokeini na madra.
Kenya imeshuhudia kwa hofu kubwa kuongezeka kwa watoto wa mitaani ambao wanatumia gundi
na petroli. Kuenea kwa matumizi ya dawa za kulevya miongoni mwa watu wa Kenya ni jambo
ambalo linatisha nchi nzima. Kati ya miaka ya 1980-1990 idadi ya shule ambazo zilikumbwa na
ukosefu wa nidhamu iliyotokana na matumizi ya dawa za kulevya iliongezeka kutoka shule 22 hadi 187.
Tunakumbuka kuwa katika mwaka wa 1981 shule ya mseto ya Mtakatifu Kizito ilishuhudia maafa
ambayo wengi wetu tungali tukifikiria ni jinamizi. Wanafunzi wa kiume waliwavamia wasichana
wenzao na kuwanajisi na kuua wasichana 19. Katika mwaka wa 1991 wanafunzi wa shule ya
wavulana ya Nyeri waliwashambulia vinara wao na kuwachoma kwa moto na wanne wao wakafa
katika mkasa huo. Mwaka wa 2001 nao wavulana wa shule ya Kyanguli walishuhudia vurugu
ambayo ilisababisha vifo vya wanafunzi 68.
Visa hivi vyote vimetokana na matumizi ya dawa za kulevya miongoni mwa wanafunzi. Dawa za
kulevya mbali na kuathiri wale wanaohusiana na wahasiriwa wale wanaotumia pia huathirika vibaya sana kwa upande wa afya. Baadhi yao hupoteza macho yao, wengine wanapata maradhi ya akili, mapafu, maini na hata viungo vya uzazi.
Janga hili lahitaji mipango madhubuti ya kuliangamiza. Baadhi ya mikakati ambayo yaweza
kuchukuliwa ni kuelimisha vijana juu ya maafa ambayo husababishwa na matumizi ya dawa za
kulevya kwa maisha yao na maisha ya wanajamii wengine. Isitoshe, serikali yapaswa kuwa na sera ambayo itaangamiza matumizi ya dawa za kulevya katika maisha ya wanajamii na hasa vijana. Zaidi ya hayo, wanajamii wote wapaswa kujitundika mzigo wa kukabiliana na dawa hizi kibinafsi na kijamii kwani kilio kinachotokana na maafa ya dawa za kulevya huwafikia watu wote.
MASWALI
a) Kwa mujibu wa taarifa hii, fafanua madhara yanayotokana na dawa za kulevya (alama 4)
…………………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………………..
………………………………………………………………………………………………….
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
b) Dawa za kulevya zimesababisha matatizo gani katika taasisi za elimu nchini Kenya ( alama 5)
………………………………………………………………………………………………….
…………………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………………..
………………………………………………………………………………………………….
c) Eleza njia tatu za kuzuia uenezaji wa dawa za kulevya (alama 3)
…………………………………………………………………………………………………..
………………………………………………………………………………………………….
…………………………………………………………………………………………………..
……………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………………….
…………………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………………
(d) Eleza maana ya naneno yafuatayo yalivyotumiwa kulingana na kifungu. (alama 3).
(i) Jaribu
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(ii) Janga
……………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………..
(iii) Jinamizi
……………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………...
2. MUHTASARI
Kuna fikra inayotawala siku hizi kuwa jela si mahali pa adhabu bali matibabu. Yaani lengo la kumfunga mhalifu si kumuadhibu bali kumtibu kwa njia ya kurekebisha tabia ili aweze kuchangia katika maendeleo ya jamii yake anapoachiliwa.
Wataalamu wa masuala ya urekebishaji tabia wanasema kuwa mhalifu akiadhibiwa sana na
kufanyishwa kazi ngumu anapokuwa kifungoni, huishia kuwa sugu zaidi kuliko alipofungwa. Kwa
hivyo , wataalamu wanasisitiza umuhimu wa kutilia mkazo lengo la kumtia mtu jela kuwa ni kumjenga kitabia. Mijizi, minyang’anyi na wauaji wanapotoka gerezani kama hawakubadilishwa hurejelea tabia zao na kuhatarisha zaidi maisha ya watu wengi.
Ajabu na kinaya ni kwamba baadhi ya wahalifu nchini na kwingineko wametokea kupata faida kuu kutokana na vifungo vyao. Kuna wafungwa ambao wamewahi kuandika hadithi za kusisismua kuhusu maisha yao na kutokea kuwa mabilionea. Magazeti na vyombo vya habari pia huvutiwa na habari kuhusu maisha yao. Mara kwa mara , magazeti hujaa habari kuhusu mambo kama haya. Pia kuna sinema nyingi ambazo zimetungwa kufuata maisha ya wahalifu fulani.
Watetezi wa haki za kibinadamu wanadai kuwa yale wafungwa walikuwa wakitendewa, na bado
wanatendewa katika nchi nyingine, ni kinyume na haki za kimsingi za binadamu. Hali hii imepelekea magereza mengi kukarabatiwa ili kuweza kukidhi mahitaji ya “ubinadamu”.
Nchini Kenya, wafungwa sasa wameanza kushughulikiwa kwa kila hali. Sikwambii wanapata chakula kizuri chenye viinilishe bora, malazi bora, maji safi na mazingira nadhifu kwa jumla. Kumeanzishwa pia mpango wa elimu ambao ni maalumu kwa wafungwa magerezani. Sasa wafungwa wanapata elimu na kuhudhuria madarasa na hata kuufanya mtihani wa kitaifa. Vilevile magereza nchini yameanzisha pia mpango wa kuwa na mashindano ya kila aina ya kati ya magereza mbalimbali. Kuna mashindano ya michezo mathalan kandanda, voliboli, na michezo mingine na juu ya yote, maajuzi magereza yalianzisha mashindano ya urembo baina ya wafungwa wa kike.
Kilele cha kuboreshwa kwa hali za magereza nchini Kenya ni kuanzishwa kwa huduma za
kuwastarehesha wafungwa hao. Sasa wafungwa wa humu nchini wanaweza kusoma magazeti na hata
kutazama runinga ili kupata habari kuhusu yanayotendeka nchini wanapoendelea kutumikia vifungo vyao.
Hata ingawa serikali imeanzisha mipango hii ya kuboresha hali katika magereza ya Kenya, kuna matatizo mbalimbali ambayo yanaendelea kukumba taasisi hii. Kwanza, ni msongamano wa wafungwa uliopo. Magereza mengi yana wafungwa maradufu ikilinganishwa na idadi yanayofaa kuwa nayo. Hali hii imepelekea kuzuka kwa magonjwa na madhara mengine. Hii imewafanya watetezi wa haki za kibinadamu kuitaka serikali ianzishe mpango wa kutoa vifungo vya nje kwa wahalifu wenye makosa madogo madogo ili kuondoa msongamano huo.
(a) Kwa nini wataaalamu na watetezi wa haki za binadamu wanapinga hali ya kuwaadhibu
wafungwa? ( Maneno 20-30 alama 5, moja ya utiririko)
Nakala chafu
……………………………………………………………………………………………….
…………………………………………………………………………………………………..
Jibu
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………..
(b) Eleza mabadiliko ambayo yamefanywa katika idara ya magereza nchini Kenya
(maneno 60-70)
Nakala chafu
………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………………..
Jibu …………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………………..
3. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
(a) Toa mfano wa neno lenye muundo wa silabi ya konsonanti tatu mwambatano pamoja na
irabu (alama 1)
……………………………………………………………………………………………….
…………………………………………………………………………………………………..
(b) Toa mfano wa sauti ya nazali (alama 1)
………………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………………..
(c) Andika sentenzi hii katika hali ya ukubwa na wingi.
Mtoto amefunga mlango wa nyumba yao (alama 1)
………………………………………………………………………………………………..
(d) Tunga sentensi kutofautisha vitate hivi kimaana (alama 2)
(i) Hawala
(ii) Hawara
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
(e) Kanusha bila kutumia “amba” (alama 1)
Nitajenga nyumba ambayo ni dhabiti
……………………………………………………………………………………………………
(f) Taja nomino zinazotokana na vitenzi vifuatavyo (alama 2)
(i) Wia…………………………………………………………………………………………
(ii) Zika ………………………………………………………………………………………
(g) Ukitumia njia ya jedwali, changanua sentensi ifuatayo (alama 4)
Gofu hushabikiwa na watu wachache sana
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………..
(h) Akifisha kifungu hiki (alama 4)
nilipowasili tu nilishika tama
nikashangaa lo moto huo ulianza vipi
na ulikuwa umesababishwa na nini
nilishikwa na bumbwazi magoti yangu
yakaanza kuchezacheza
………………………………………………………………………………………………….
…………………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………………
(i) Tunga sentensi sahihi ukitumia kitenzi – nywa katika kauli ya kutendesha (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………..
(j) Eleza maana mbili tofauti za sentensi hii. (alama 2)
Watoto walisimamia watu wakubwa
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………….
(k) Eleza matumizi ya ‘ni’ katika (alama 2)
(i) Amina ni mgeni
(ii) Nyooni hapa
………………………………………………………………………………………………….
…………………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………………..
(l) Ainisha maneno haya katika ngeli zake (alama 2)
(i) Mvule
(ii) Ufunguo
………………………………………………………………………………………………….
…………………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………………..
(m) Yakinisha sentensi hii (alama 2)
Mpishi asipokuwa mwangalifu chakula hakitaiva vizuri
………………………………………………………………………………………………….
…………………………………………………………………………………………………..
(n) Andika sentensi ifuatayo katika usemi halisi (alama 4)
Mama alimwuliza mwanawe alikochelewa na kisha akamtahadharisha kuwa haitakuwa tabia
njema kwa mtoto wa kike kama yeye kuzoea kutembea usiku
…………………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………………..
(o) Ainisha viwakilishi katika sentensi hii (alama 2)
Usibanduke papa hapa
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
(p) Katika kila kipashio tunga sentensi moja moja kubainisha matumizi ya (alama 3)
(i) kwa
………………………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………………….
(ii) na
………………………………………………………………………………………………….
…………………………………………………………………………………………………..
(iii) Ku
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………..
(q) Sahihisha sentensi zifuatazo (alama 4)
(i) Nisingekuja hungaliniadhibu vile
…………………………………………………………………………………………………..
(ii) Kiumbe ambacho kilichoumbwa lazima kiwe na umuhimu
………………………………………………………………………………………………
4. ISIMUJAMII (ALAMA 10)
(a) Eleza juhudi zozote tano za serikali ya Kenya katika kukuza Kiswahili (alama 5)
………………………………………………………………………………………………….
…………………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………………..
(b) Taja na ueleze pingamizi zozote tano zinazokwamiza juhudi za kukuza Kiswahili (alama 5)
………………………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………………….






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers