Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Rachuonyo South District Mock - Kiswahili Paper 2 Question Paper

Rachuonyo South District Mock - Kiswahili Paper 2 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2011

Jina: …………………………………………………………………… Nambari: ………...………
Shule: ………………………………………………………………. Sahihi ....................................
Tarehe: …………….....................................................................……
102/2
KISWAHILI
LUGHA
KARATASI YA 2
JULAI/ AGOSTI 2011
MUDA: SAA 2 ½
Hati ya kuhitimu kisomo cha sekondari Kenya (K.C.S.E)
Kiswahili
Lugha
MAAGIZO
• Andika jina lako na namba yako katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
• Weka sahihi yako na tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa
• Jibu maswali yote.
• Majibu yaandikwe katika nafasi zilizoachwa wazi katika kijitabu hiki cha maswali.
Karatasi hii ina kurasa 8 zilizopigwa chapa. Watahiniwa ni lazima waangalie kama kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.
1. UFAHAMU (ALAMA 15)
Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali.
Lugha imekuwa kikwazo kikubwa katika kukuza teknolojia ya habari na mawasiliano
(TEKNOHAMA) barani Afrika. Lugha ambazo zimekuwa zikitumiwa ni za kimagharibi kama vile
Kijerumani, Kifaransa na Kiingereza. Idadi kubwa ya Waafrika, hasa wanaoishi vijijini,
hawazifahamu lugha hizi.
Uamuzi wa Shirika la Microsoft wa kutumia lugha ya Kiswahili katika programu za
kompyuta kuanzia mwaka 2005 ni mchango mkubwa Kuzinduliwa kwa mradi huu ni tukio la
kipekee kuimarisha teknolojia sehemu za mashambani. Mradi huu umewawezesha wananchi
takribani milioni 150 wa janibu za Afrika Mashariki kufaidi huduma za tarakilishi.
Utekelezaji wa mradi huu halikuwa jambo jepesi. Kwanza, ilibidi Shirika la Microsoft chini
ya uongozi wa Bill Gates kulishawishi Bodi lake la wakurugenzi. Bodi liliposhawishika kuwa
Kiswahili ni lugha inayotumiwa na mamilioni ya watu liliidhinisha kuzinduliwa kwa mradi. Hatua iliyofuatia ilikuwa kuteua maneno 700,000 ya kimsingi ya Kiingereza ambayo yangetafsiriwa kwa Kiswahili.
Hatua iliyofuata ilikuwa ushirikiano na dola pamoja na mashirika ya kibiashara na taasisi za kielimu ulimwenguni. Ilipobainika kuwa matumizi ya lugha ya Kiswahili yangehamasisha uwekezaji katika vituo vya mtandao vijijini, ushirikiano katika kuendesha mradi huu uliafikiwa bila shida.
Mradi huu ulichukua muda wa miezi 18 kukamilika. Uliwashirikisha wahusika katika uwanja wa
teknolojia ya habari, mawasiliano, elimu, biashara na idara za Kiswahili katika vyuo vikuu vya Afrika Mashariki. Vyuo vikuu hivi ni pamoja na Dar es Salaam, Nairobi, Kenyatta na Makerere, Wataalamu walioshirikishwa walisaidia katika kubuni faharasa ya istilahi za Kiswahili 3,000.
Hizi ni zile ambazo zinafaa kwa matumizi ya kompyuta ya kawaida na ya kila siku. Mradi huu
umeshangiliwa na wakereketwa na wapenzi wa Kiswahili katika nyanja zote. Wasomi, wanariadha,wanamuziki, watalii, wafanyabiashara, wanasiasa, wafuasi wa dini mbali mbali na wakulima; wote wamefurahia hatua ya Kiswahili kuingizwa kwenye mtandao.
Watu ambao walikuwa hawawezi kuturisha tarakilishi kwa sababu ya kutojua Kiingereza
sasa hawana kisingizio. Matumizi ya Kiswahili yatapanua na kuimanisha mawasiliano baina ya watu wanaoishi vijijini na pembe zote za ulimwengu.
Jambo la kutia moyo zaidi ni kuwa sasa vyuo vikuu vinavyotoa masomo kwa kutumia
mitandao vimepewa idhini ya kutumia programu hizi. Walimu na wanafinzi wanapata habari moja
kwa moja kwa Kiswahili bila kutafsiri. Kuna uwezekano sasa wa kusambaza mafunzo katika nyanja na viwango vyote kwa mfumo wa elimu ya mbali.
Katika ulimwengu wa utandawazi, tukio kama hili lina manufaa makubwa. Wananchi wa
vijijini wanaweza kupata habari na maarifa kutoka pembe zote za dunia na kuhusu masuala tofauti tofauti kwa lugha wanayoielewa barabara.
Kusambaa kwa matumizi ya ngamizi vijijini kutaimarisha biashara inayofungamana na
teknolojia ya mawasiliano. Hali hii itainua maendeleo ya kiteknolojia na kiwango cha maisha vijijini.
Bila shaka mwachano uliopo baina ya sehemu za mijini na vijijini utapungua.
Haya ndiyo maendeleo anayokamia kila mja wa siku hizi. Lililopo ni serikali kupania
kupanua na kusambaza muundo mbinu kama umeme na simu katika sehemu zote za nchi. Pamoja na
haya, kuna haja ya kupunguza bei ya ngamizi na vipuri vyake ili kuwatia motisha watu kununua kompyuta kwa wingi. Ikumbukwe kuwa lengo la kuanzisha mradi huu lilikuwa kuisaidia serikali kupanua na kusambaza matumizi ya huduma za kompyuta na mtandao katika shule, vituo vya kijamii na maeneo ya makaazi. Huduma hizi ni msingi wa elimu, biashara na mawasiliano ya kisasa.
Maswali
(a) Eleza hatua zilizotekelezwa ili kuingiza Kiswahili katika mtandao. (ala. 4)
………………………………………………………………………………………………..…..…
.………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………..…..…
.………………………………………………………………………………………………………
(b)Lugha imekuwa kikwazo kikubwa katika kukuza teknolojia ya habari na mawasiliano barani
Afrika. Thibitisha kauli hii. (ala.2)
………………………………………………………………………………………………..…..…
.………………………………………………………………………………………………………
(c) Fafanua faida za mradi wa kutumia Kiswahili katika ratiba ya tarakilishi. (ala.3)
………………………………………………………………………………………………..…..…
.………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………..…..…
(d) Serikali inahitaji kufanya nini zaidi ili kufanikisha mradi huu? (ala. 3)
………………………………………………………………………………………………..…..…
.………………………………………………………………………………………………………
.………………………………………………………………………………………………………
(e) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyo tumiwa katika taarifa. (ala.3)
i) Faharasa
………………………………………………………………………………………………..…..…
ii) Wakereketwa
.………………………………………………………………………………………………………

4
iii) Ngamizi
………………………………………………………………………………………………..…..…
2. UFUPISHO
Soma makala haya kisha ujibu maswali.
Aibu kubwa ya taifa kushindwa kukabiliana na tatizo sugu La ajali za barabarani bado
inaendelea kuwafedhehesha wahusika katika sekta ya uchukuzi na mawasiliano licha ya matumizi ya vidhibiti mwendo na kanda za usalama.
Ajali za baraza barabarani zinaangamiza idadi kubwa ya watu kila mwaka wakiwemo
viongozi na watu mashuhuri.Miongoni mwa sababu ambazo zinaleta maafa barabaraii n pamoja na
uendeshaji kasi kupita inavyotakikana, yaani kukiuka masharti yaIyowekwa na wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano.Madereva wengi hung’oa vidhibiti mwendo viivyowekwa, hawarekebishi mikanda ya usalama, wala hawayapeleki magari yao kukaguliwa mara kwa mara kama inavyopaswa. Yale yanayopelekwa kwa ukaguzi, mengi hushindwa kutekeleza kanuni zilizowekwa kwa hivyo hutegemea hongo kuwa barabarani.Fauka ya hayo, madereva wa malori na matrela mara nyingi huendesha rnagari hayo wakiwa walevi., Dawa za kulevya, kama miraa na bangi hutumiwa sana na hawa na rnatokeo yake huwa ajali mbaya.
Hata hivyo, lawama haiwezi kuelekezewa madereva pekee. Ukiangazla barabara nchini
Kenya utapata kuwa barabara haziko katika hali nzuri. Zile za lami zimekuwa na mashimo makubwa ambapo mvua ikinyesha hufanya vidibwi mithili ya michimbo ya madini yaliyojaa maji
baada ya kuachwa wazi. Na zile barabara zisizokuwa na lami zimeharibika kiasi kwamba ni vigumu kuzitofautisha na njia za ng’ombe kwenye maeneo kame kinachohitajika kuzirudisha katika kiwango ambacho zitaweza kufaa tena.
Wananchi pia inafaa waelimishwe iii wasikubali kupanda magari ambayo tayari yamejaa.
Hili litawasaidia wananchi wenyewe kudumisha usalama wao barabarani. Pia inawafaa watambue ya kwamba wana jukumu Ia kuwaarifu walinda usalama endapo dereva anaendesha kwa kasi kuliko ile ya kilomita themanini kwa saa iliyokubaliwa.Inafahamika kuwa maafisa wa usalama ndio wafisadi zaidi, hivyo basi huchangia katika kuongeza idadi ya vifo barabarani. Katika vita vya ufisadi na ajali za barabarani ni mwananchi mwenyewe ambaye atawezesha kukomesha hali hii. Kwa mfano, afisa
wa usalama akipatikana akichukua bongo, yeye pamoja na yule aliyetoa bongo wakamatwe na
kupelekwa kwenye vituo vya kukabiliana na ufisadi na kuchukuliwa hatua kali, matatizo haya
yataisha. Lakini kabla kufikia hapo, ni muhimu kumhamasisha mwananchi kuhusu haki zake na
namna ya kukabiliana na suala hill La ufisadi. Hali hii inatuonyesha kwamba mipango maalum
inapaswa kufanywa na serikali iii kuwaelimisha wananchi kama hatua ya kwanza yakukabiliana na ufisadi hatimaye izilainishe sekta zote wala si ya uchukuzi na mawasiliano pekee.
Maswali
a)Eleza mambo yote muhimu anayozungumzia mwandishi katika aya ya pili na tatu. (maneno 50)
(ala.7)
Nakala chafu
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………..…
Nakala safi
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………..…
..……………………………………………………………………………………………………………
(b)Bila kubadilisha maana iliyokusudiwa, fupisha aya ya mwisho. (maneno 40) (ala. 6)
Nakala chafu
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………..…
Nakala safi
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………..…
..……………………………………………………………………………………………………………
3. MATUMIZI YA LUGHA:
a)Eleaza dhana hizi: (ala.2)
(i) Shadda
…………………………………………………………………………………………………..……
(ii) Kiimbo
…………………………………………………………………………………………………..……
b)Hizi ni konsonanti za aina gani na zinatamkiwa wapi? (ala.4)
Aina Mahali pa kutamkia
i) ch
ii) f
c) Andika kwa udogo (ala.2)
Ndege huyu alimla kifaranga
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
d) Onyesha kishazi huru na tegemezi katika sentensi hii (ala.2)
Ijapokuwa kulikuwa na baridi kali niliondoka kwenda sokoni.
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
e)Bainisha vitenzi katika sentesni hizi na ueleze ni vya aina gani. (ala.2)
i) Ouma amekuwa uwanjani
………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
ii) Huyu ndiye mwalimu mkuu.
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
f)Yakinisha.
(i) Hakula chakula wala kunywa maji. (ala.2)
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
(ii) Andika kwa umoja
Pulikeni wanetu,msicheze na dunia Mnasikia? (ala.2)
…………………………………………………………………………………………………..……
………………………………… ………………………………………………………………..……
h)Eleza matumizi matatu tofauti ya ‘ki’ (ala.3)
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
i) Sahihisha sentensi ifuatayo: (ala.2)
Mama mwenye alikufa amezikwa katika makaburini
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
j)Eleza maana mbili za sentenis hii: (ala. 2)
Alitimua mbio kuona ndovu
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
k) Bainisha shamirisho tofauti katika sentensi ifuatao: (ala. 4)
Ali alimnunulia simu mpenzi wake.
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
l) Changanua sentensi ifuatayo ukitumia mchoro wa matawi (ala. 4)
Mwanafunzi huyu anaandika vizuri sana.
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
m) Maneno ya fuatayo yanapatikana katika ngeli gani? (ala. 2)
(i) Karakana
…………………………………………………………………………………………………..……
(ii) Diseli
…………………………………………………………………………………………………..……
n) Andika kwa msemo wa taarifa. (ala. 3)
“Lo! Umeweza kuubeba mzigo huu pekeyo?” Mama Alishangaa.
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
o) Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli ulizopewa. (ala. 2)
Kitenzi Kutendea Kutendana
(i) la
(ii) Paka
……………………………………
………………………………..
…………………………………….
……………………………………
p) Tunga sentensi ukitumia alama zifuatazo za kuakifisha.
(ala.2)
(i) Ritifaa
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
(ii) Koloni/nukta pacha
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
4. ISIMU JAMII: (ALAMA 10)
Onyesha njia kumi ambazo kwazo Kiswahili kimeweza kuenea duniani tangu enzi za ukoloni
hadi sasa.
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………..…
..……………………………………………………………………………………………………………

More Question Papers

Popular Exams

Return to Question Papers