Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Butere Mumias District Mock-Kiswahili Paper 2 Question Paper

Butere Mumias District Mock-Kiswahili Paper 2 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2007



Jina………………………………………………… Nambari. …………………….
Shule ………………………………………………...
102/2
KISWAHILI
KARATASI 2
(LUGHA)
JULAI/AGOSTI 2007
MUDA: SAA 2 ½
MTIHANI WA MWIGO. WILAYA YA BUTERE - MUMIAS BARAZA - 2007
Hati ya kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya
102/2
KISWAHILI
KARATASI 2
(LUGHA)
JULAI/AGOSTI 2007
MUDA: SAA 2 ½
Maagizo kwa Watahiniwa
• Jibu maswali yote
• Majibu yako yaandikwe katika nafasi zilizoachwa katika kijitabu hiki.
Karatasi hii ina kurasa 12 zilizopigwa chapa
Watahiniwa lazima wahakikishe kurasa zote zimepigwa chapa sawa sawa na kuwa maswali yote yamo.
1. UFAHAMU.
Soma makala yafuatayo kasha ujibu maswali .
Huku ulimwengu unapoingia katika teknolojia ya tarakilishi na sera ya utandaridhi, ukweli wa mambo ni kuwa akina mama wamezinduka. Suala la usawa wa kijinsia limeanza kushamiri kote duniani na ole wake mwanamume yeyote ambaye hajawa tayari kutembea na majira. Lakini hebu tuchunguze jambo hili kwa makini zaidi.
Usawa wa jinsia ni nini? Usawa wa kijinsia ni usawa wa binadamu wote: wawe wake au waume.
Usawa huu unapaswa kudhihirika katika nafasi za kazi, utoaji wa elimu, nafasi za uongozi na nyanja nyinginezo zozote za maisha. Ubaguzi na aina yoyote ile hasa dhidi ya mwanamke ni jambo linalokabiliwa na vita vikali sana ulimwenguni kote.
Dahari na dahari, hasa katika jamii za kiafrika, kumekuwa na imani isiyotingisika kuwa mwanamke ni kiumbe duni akilinganishwa na mwanamume. Kwa hivyo mwanamke amekuwa akifanyiwa kila aina ya dhuluma ikiwepo kupigwa, kutukanwa, kudharauliwa, kunyimwa haki zake, kunyimwa heshima na mambo kama hayo. Lakini je, ni kweli kuwa mwanamke ni kiumbe duni asiyefaa kutendewa haki?
Tukichunguza jamii kwa makini tunaweza kuona mara moja kuwa hivyo ni imani potofu isiyo na
mashiko yoyote. Ukiimulika familia yoyote ile iliyopiga hatua kimaendeleo, uwezekano mkubwa ni kuwa mume na mke wa familia inayohusika wana ushirikiano mkubwa. . Mume anamthamini mke na hadiriki kufanya maamuzi muhimu yanayoweza kuathiri maendeleo ya familia bila kumhusisha mke. Mume kama huyu huketi na mkewe, wakishauriana na kufikia uamuzi bora.
Tukitoka katika muktadha wa kifamilia na kumulika ulimwengu wa kazi iwe ni katika afisi za
kiserikali au kwenye makampuni binafsi, ukweli ni kwamba kiongozi yeyote yule aliyefaulu katika usimamizi wake mara nyingi huwa na mke nyumbani ambaye wanashauriana kila uchao kuhusu kazi anayofanya hata kama mke hafanyi kazi mahali pale. Hisia na mawaidha anayotoa mke kwa mume wake ni tunu na huenda asiyapate kwingineko kokote hata katika vitabu vya kupigiwa mifano. Hii ni mojawapo ya sababu ambayo huwafanya viongozi wa nchi mbali mbali kupenda sana kuwatambulisha wake na familia zao wazi wazi kwa vile kuwa jamii inathamini sana msingi wa jamii. Kiongozi ambaye hana mke au familia au yule ambaye mke wake hatambulikani, hutiliwa mashaka na jamii hata kama kiongozi huyu ana hulka ya uongozi. Jamii inaamini kuwa mke ni johari kwa mume wake hasa yule aliye na azma ya kushikilia kazi ngumu ya kuongoza umma.
Tukirudi nyuma kidogo na kupiga darubini mataifa ya mbali, tunaweza kuwaona wanawake
mashuhuri waliotoa uongozi ambao hadi waleo unapigiwa mfano. Wanawake hao walisimamia
mojawapo ya mataifa yenye uwezo na ushawishi mkubwa zaidi duniani. Ingawa wengi wao sasa
wameng’atuka, uongozi wao bado unakumbukwa hata baada ya miaka mingi ya wao kuamua
kupumzika. Mifano ni kama; Bi Margaret Thatcher aliyekuwa waziri mkuu wa uingereza. Bi
Bandranaike wa Sri Lanka. Gold a meir wa Israel na wengine katika mataifa kama Indonesia,
ufilipino, Bangladesh, Pakistani na kwingineko.
Katika kufikia tamati, tunapozungumza kuhusu jinsia, hatuna budi kugusia kitafsili masuala nyeti. Kwanza,imani ya kushikilia ki ki ki tamaduni zisizofaa, ni jambo linalofaa kuchunguzwa kwa makini. Kwa mfano, kuna baadhi ya jamii ambazo humlazimu mke kurithiwa baada ya kifo cha mumewe. Vile vile baadhi ya jamii za kiafrika zinashikilia kuwa mwanamke hana haki ya kurithi. Kutokana na imani hii, wanawake wengi huishi maisha ya taabu baada ya kutengana na waume zao kwa vile hawana haki ya kurithi chochote kutoka kwa wazazi wao hata kama wazazi hao wana mali nyingi kupindukia. Mali ya wazazi ni haki ya watoto wa kiume wala si watoto wa kike. Hili ni jambo la kusikitisha mno!
Isitoshe, wanawake hukumbwa na kizingiti kingine wanapojaribu kumiliki mali ya waume zao baada ya waume hao kukata kamba. Sababu ni kuwa, baada ya hao wendani zao kuwekwa kaburini, vita vya umiliki wa mali huanza mara moja na mwishowe yule mke maskini hujikuta hana hata mahali pa kulala sembuse mali waliyochuma na mumewe. Hatimaye mke hujikuta matatizoni anapoamriwa kufunganya virago na mali yake yote kunyakuliwa na aila ya mumewe. Jambo hili linaonyesha namna tulivyoachwa nyuma na uhalisia wa mambo. Ni lazima jamii izinduke na itoke kwenye kiza hiki chenye maki nzito.
MASWALI.
a) Ina maana gani kusema kuwa wanaume hawana budi ‘kutembea na majira’? (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
b) kabla ya uzinduzi huu kuhusu usawa wa kijinsia, wanawake wamekuwa wakitendewa dhuluma za
kila aina. Taja tatu. (alama 3)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………

4
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
c) Je, ni kwa nini viongozi wengi hupenda kujitambulisha na familia zao? (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
d) Je, unaamini kuwa hisia na mawaidha anayotoa mke kwa mume ni tunu na huenda yasipatikane
kwingineko? Fafanua (alama 3)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
e) Je, licha ya kunyimwa haki yake ya kujiamulia, ni matatizo yapi mengine yanayoweza kumkumba
mke anayelazimishwa kurithiwa? (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
f) Eleza maana ya maneno yafuatayo jinsi yalivyotumiwa katika muktadha. (alama 3)
i) kushamiri
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
ii) hulka
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
iii) azma
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
2. UFIPISHO
Soma makala yafuatayo kasha ujibu maswali.
Mwana wa Adamu ni kiumbe cha ajabu! Ni kiumbe kilichopewa uwezo wa kuhodhi na kumiliki kila
kitu, kiumbe kilichopewa akili na maarifa fuvu tele ili kutaratibu shughuli na mambo; kiumbe kilichopewa uwezo wa kuwasiliana na kutumia sauti nasibu ili kuwa na urari na muwala; kiumbe kilichopewa uwezo wa kufaidi viumbe wengine kwa njia mbalimbali na jumla jamala; hiki ndicho kiumbe kilichopewa idhini maalum ya kuzaana na kujaza dunia. Huyu ndiye mwana wa mama Hawa ambaye sasa amegeuka ndovu kumla mwanawe.
Kwa sababu ya bongo alizonazo,binadamu ana uwezo wa kutumia teknolojia kwa manufaa yake na
ithibati zipo tele. Binadamu ametumia nyambizi kuzuru chini ya bahari, amefika mwezini,
amevumbua magala: amevumbua uyoka: amevumbua tarakilishi na sasa shughuli zake ni za
kutandaridhi. Mwenyewe yuasema kuwa dunia yake imekuwa kitongoji katika muumano huu.
Chambilicho wavyele, akili nyingi huondoa maarifa. Binadamu amekuwa dubwana linalojenga
kushoto na kubomoa kulia na tuna sababu ya kulisoza dubwana hili kidole. Rabana ndiye msani asiye mfanowe kwani aliisawiri murua. Rabuka akaona yote yalikuwa mema na mazuri: akamwambia binadamu, “ Haya’ twende kazi!’
Viwanda vya binadamu vinatiririsha maji-taka ovyo hadi mitoni, maziwani na baharini na matokeo yamekuwa ni vifo vya viumbe vya mjini kama samaki ambavyo ni urithi aliopewa na muumba.
Hakuna kiumbe kinachoweza kustahimili maisha bila maji safi. Maji yoye sasa yametiwa sumu na binadamu kwa sababu ya ‘maendeleo’ yake. Joshi kutoa katika viwanda vivyo hivyo nalo limehasiri ukanda wa ozoni ambao sasa umeruhusu jua kutuhasiri kwa joto kali mno. Siku hizi inasemekana kuwa kuna mvua ya asidi inayonyesha katika baadhi ya sehemu za dunia na kuleta madhara makubwa. Labda hata mabahari yamekasirika kwa sababu hivi majuzi katika kile kilichoitwa ‘tsunami’, bahari lilihamia nchi kavu na kusomba maelfu ya binadamu na kuwameza wazima wazima. Vimbunga navyo vimetokea kwa wingi. Wataalamu wanasema kuwa viwango vya miyeyuko vitazidi kwa sababu ya joto na kiwango cha maji kitazidi pia. Binadamu atatorokea wapi?
Idadi ya binadamu imezidi hadi kiasi asichoweza kukishughulikia kwa sababu anaijaza kiholela kwa sababu anadai kuwa aliruhusiwa kuijaza. Hii ni imani potovu. Anasahau kuwa alipewa ubongo wakuwaza na kuwazua kabla ya kufanya chochote. Dhiki, maradhi na ufukara zimehamia kwa binadamu na kumtia kiwewe.
Binadamu amefyeka misitu kwa kutaka makao, mashamba , mbao, makaa, ujenzi wa nyumba na
barabara na mahitaji mengine mengi. Wanyama wamefurushwa na wengi kuangamia kwa sababu ya
ukosefu wa chakula na wengine kushindwa kuhimili mabadiliko katika mazingira. Chemichemi za maji zimekauka nalo jangwa limeanza kutuzuru kwa kasi inayotisha. Kazi ya binadamu imekuwa ya kusukia kamba motoni. Itambidi aanze kujenga kwa matofali ya barafu.
MASWALI
a) Bila kupoteza maana iliyokusudiwa na mwandishi wa taarifa, fupisha aya ya kwanza.
(maneno 40-50) ( alama 5 )
Matayarisho
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
Jibu:
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
b) kwa kuzingatia aya za mwisho, eleza mambo muhimu yanayoshughulikiwa na mwandishi.
( maneno 95 – 105 ) ( alama 8)
Matayarisho;
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………7
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
Jibu:
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
Utiririko ( alama 2)
MATUMIZI YA LUGHA
a) Andika wingi wa ( alama 1)
Jani jembamba
……………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
b) Changanua sentensi ifuatayo ukitumia muundo wa jedwali ( alama 4)
Mwanaume huyu anatembea polepole sana.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
c) Sahihisha sentensi ifuatayo. (alama 1)
Shairi ambalo alilotukariria ni lile ambalo alilotoa katika gazetini.

8
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
d) Tunga sentensi ukitumia vitenzi vifuatavyo katika kauli ya kutendea. (alama
2)
i) –ja
ii) –la
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
e) Andika sentansi ifuatayo katika ukubwa (alama 2)
Moto huu utachoma nyumba.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
f) Bainisha shamirisho kipozi, kitondo na ala katika sentensi hii. (alama 3)
Juma alimlimia mama shamba kwa trekta.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
g) Andika sentensi zifuatazo katika hali yakinifu. ( alama 2)
i) Mgeni hatarudi kwetu tena.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
ii) Kitabu hakisomeki vizuri.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
h) Eleza maana ya ‘ki’ katika sentensi zifuatazo. (alama 3)
i) Ukisoma kwa bidii utafaulu mtihani wako.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
ii) Uji bila sukari haunyweki
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
iii) Hakijapatikana hadi leo.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
I) Tumia neno ‘ vizuri’ katika sentensi kama ( alama 2)
i) Kivumishi
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
ii) kielezi
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
J. Tambulisha vishazi huru na vishazi tegemezi katika sentensi hii (alama 2)
i) Mtu aliyekuja shuleni jana alikaribishwa kwa furaha.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
k. Ainisha aina za vitenzi katika sentensi hizi. (alama 2)
i) Amina atakuja kesho
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
ii) Sanduku lilikuwa limevunjika
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
L. Akifisha (alama 3)
Rehema alimwuliza na wewe unakubali una wazimu twende kwanza nani atajua.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
M. Tunga sentensi kwa kutumia maneno yafuatayo. (alama 2)
i) Laiti
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
ii) Fauka ya
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
N. Andika sentensi zifuatazo upya kulingana na maagizo (alama 2)
i) “ Kuna chai? “ Mtoto aliuliza. (Maliza kwa….. chai)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
ii) Nchi zinazoendelea lazima malighafi yoyote. (Anza malighafi…)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
O. Eleza matumizi ya ‘po’ katika sentensi hii. ( alama 2)
Alipofika alimwona pale alipokuwa amelala
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
P. Eleza maana ya semi ifuatayo. (alama 2)
Piga chenga
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
Q. Tunga sentensi kuthibitisha maana ya vitate hivi (alama 2)
i) Chali
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
ii) Shali
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
R. Badilisha katika hali timilifu. (alama 2)
i) Wazee wa kijiji watakata kesi hii
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
ii) Wafanyakazi hulipwa mishahara yao wakati ufaao.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
S. Kanusha sentensi ifuatayo.
Ukilala sana utapona haraka. (alama 1)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
4. ISIMU JAMII
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali.
A: Ohh, dada Naomi
B: Dada Ruth ( anamsogea kwa bashasha wanakumbatiana) Ahh mungu asifiwe!
A: Asifiwe sana.
B; Ehh dadangu, miezi .. mingi ….sijakuona
A: Dada wee…Nilitumwa huko kusini…. Kuwahubiria watu injili.
(mtuo mdogo) singeweza kukata..
B: Ehh, usiwe kama Yona…
A: Habari ya siku nyingi?
B: Nzuri Mungu bado ameendelea kunibariki
A: Amen!
B: Nimeendelea kuiona neema yake.
A: Amen! Asifiwe Bwana
B: Halleluya.
A: Ni Mungu wa miujiza!
B: Amen. Hata nami nimeona neema yake.
Bado niko imara katika wokovu katika siku hizi za mwisho.
A: Amen!
B: Ni Mungu wa ajabu kweli!
A: Nilikumbana na matatizo lakini nikategemea sala
Kama Paulo na sila…. Na nikashinda(anatua). Sikuweza kumpa shetani nafasi… maana
ameshindwa
B: Ameshindwa kabisa
i) Hii ni sajili ya wapi? Fafanua. (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
ii) Taja na ueleze sifa za sajili hii (alama 4)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
iii) Taja masharti manne yanayoathiri matumizi ya lugha (alama 4)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
Mwisho






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers