Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Thika District Mock - Kiswahili Paper 2 Question Paper

Thika District Mock - Kiswahili Paper 2 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2011



JINA………………………………………………………….NAMBA YAKO……………………….
SAHIHI YA MTAHINIWA…………….
TAREHE…………………………………
102/2
KISWAHILI
KARATASI YA 2
LUGHA
JULAI/AGOSTI 2011
SAA: 2 ½
MTIHANI WA PAMOJA WA SHULE ZA MKOA WILAYANI THIKA – 2011
HATI YA KUHITIMU ELIMU YA SEKONDARI KENYA (K C S E)
KISWAHILI
KARATASI YA 2
LUGHA
SAA 2 ½
MAAGIZO
(a) Andika jina lako na namba yako katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
(b) Weka sahihi yako na tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
(c) Jibu maswali yote.
(d) Andika majibu yako katika nafasi ulizoachiwa katika kijitabu hiki cha maswali.
(e) Karatasi hii ina kurasa 9 zilizopigwa chapa.
(f) Watahiniwa ni lazima waangalie kama kurasa zote zimepigwa chapa sawawa na kuwa
maswali yote yamo.
(a) UFAHAMU
Soma makala yafuatayo kasha ukubu maswali.
Ingawa wenye hekima walisema kuwa macho hayana pazia, ni muhimu kuyatumia macho ulivyojaaliwa
na muumba wako. Ndio maana ninaamini pia kuwa macho hayafilisi duka!
Mimi hupenda kuyafumbua macho pima kila nitembeapo barabarani au hata ninapokaa nyumbani
kusakura yaliyo karibu nami. Lakini kuna matukio ambayo hunisumbua na kunisikitisha. Hunisumbua kwa sababu sipati majibu kwayo; hunisikitisha kwa sababu ya athari zake na mihemko yanayoleta katika hisia zangu za ndani. Kila mara hujiuliza: “Kwa nini watu wengi huteseka namna hii duniani? Kwa nini mtu adamke mafungulia ng’ombe akielekea kibaruani kila siku bila kusita huku wachache wakistarehe?
Kwa nini ugonjwa unaweza kumvamia mtu ghafla bin vuu na kumlemaza ama kumtaabisha kwa muda
mrefu kabla ya kumuua? Kwa nini? Mbona kila mara mtu anapokuwa akisikitika, kuna mwenzake huwa anacheka? Ama maisha ni kitendawili tu?
Hata hivyo, linalonishangaza sana wakati mwingine ni jinsi wale ninaowafikiria kuwa wanataabika wanavyochukulia hali zao. Utawaona akina yakhe wakitabasamu kila mara na kucheka hata matumbo yakiwaguruma. Utawasikia wakiulizana: “Umeshindaje”? Kana kwamba wamejishindia chochote kwani unapoangalia vizuri unakuta kwamba wameshindwa karibu kwa kila hali. Mbona wasiulizane :
Umeshindwaje?
Hii ndio sababu wakati mwingi moyo wangu huanza kuhisi kuwa labda siku ya kiyama inakaribia zaidi.
Wewe hebu fikiria, wanasayansi wanapotuambia kila mara kuwa wamevumbua hiki ama kile ambacho kitafanya maisha ya mwanadamu kuwa rahisi zaidi, ndivyo tunavyojitumbukiza katika majanga na matatizo zaidi maishani. Hii ndio sababu hata ile dhana iliyokuwepo miaka ya nyuma kuwa maradhi ya Ukimwi ambayo yamekosa tiba hadi sasa kando na kuwaua mamilioni ya watu yalitokana na ajali ya kisayansi huko Marekani inaweza kupata mashiko.
Swali la kujiuliza ni: “ Ni kwa nini maisha yanaposemekana kuwa yamebadilika na kuwa mazuri siku hizi ikilinganishwa na zamani mimi naona kinyume? Au wewe waonaje? Mbona zamani kabla ya majilio ya kile siku hizi kinaitwa ‘maendeleo’ watu walikuwa wakitembea tu na kula matunda na mimea, watoto wakicheza na kucheka kwa furaha bila bughudha yoyote? Au hata mbona watu hawakuwa na ubinafsi niunao siku hizi?”
Maendeleo hayo tunayoyataja kila siku nayaona kama ongezeko la chuki, uhasama, magonjwa, ubinafsi,vita, ufisadi na hujuma dhidi ya mazingira ambamo mwanadamu anafaa kufurahia maisha. Ukweli ni kwamba maendeleo hayo yamepelekea watu wengi zaidi ulimwenguni kuishi katika mitaa ya mabanda, kuwa na nyuso za “sitaki mchezo” na “karibu lakini usidowee”.
Ninapozama zaidi katika bahari ya luja kuhusu hali hii duniani ndivyo ninavyochanganyikiwa zaidi kuhusu ukweli halisi. Maajuzi nimeishitakia hali hii kwa Mola ingawa sijajaaliwa jibu. Hata hivyo, ninavyoendelea kulingoja jibu ndivyo ninavyoendelea kuelewa ile dhana kuwa ulimwengu ni kokwa ya fuu huishi utamu, anayekwisha ni binadamu.
UFAHAMU
(a) Tolea makala haya kichwa mwafaka. (alama 1)
…………………………………………………………………………………………………….
(b) Kwa nini mwandishi anadai kuwa labda siku ya kiyama imefika? (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(c) Unafikiri ni kwa nini mwandishi anayaona madai kuhusu maendeleo duniani kuwa ni kinaya (alama 3)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(d) Mwandishi wa taarifa anamaanisha nini kwa kusema.
(i) Sitaki mchezo
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(ii) Karibu lakini usidowee. (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(e) Yalinganishe maisha ya kabla ya maendeleo na ya sasa ambayo mwandishi anadai ni duni kuliko ya
zamani. (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(f) Je, unakubaliana na msimamo wa mwandishi kuwa madai kuhusu maendeleo ni kinaya?
Eleza. (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(g) Eleza maana ya vifungu vya maneno kama vilivyotumika katika taarifa. (alama3)
(i) Kusakura
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(ii) Bahari ya hija
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(iii) Ulimwengu ni kokwa ya fuu huishi utamu, anayekwisha ni binadamu.
……………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………….
MUHTASARI
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
Mwana wa Adamu ni kiumbe cha ajabu! Ni kiumbe kilichopewa uwezo wa kuhodhi na kumiliki
kila kitu; kiumbe kilichopewa akili na maarifa fuvu tele ili kuratibu shughuli na mambo; kiumbe kilichopewa uwezo wa kuwasiliana na kutumia sauti nasibu ili kuwa na urari na muwala; kiumbe kilichopewa uwezo wa kufaidi viumbe wengine kwa njia mbalimbali na jumla jamala; hichi ndicho kiumbe kilichopewa idhini maalumu ya kuzaana na kujaza dunia. Huyu ndiye mwana wa mama Hawa ambaye sasa amegeuka ndovu kumla mwanawe.
Kwa sababu ya bongo alizonazo, binadamu ana uwezo wa kutumia teknolojia kwa manufaa yake
na ithibati zipo tele. Binadamu ametumia nyambizi kuzuru chini ya bahari; amefika mwezini; amevumbua mangala; amevumbua uyoka; amevumbua tarakilishi na sasa shughuli zake ni za kutandaridhi. Mwenyewe yuasema kuwa dunia yake imekuwa kitongoji katika muumano huu.
Chambacho wavyele, akili nyingi huondoa maarifa.Binadamu amekuwa dubwana linalojenga
kushoto na kubomoa kulia na tuna sababu ya kulisoza dubwana hili kidole. Rabana ndiye msanii asiye mfanowe kwani aliisawiri dunia kwa kila lililo jema kwa siku sita mtawalia na kumpa binadamu mazingira murua. Rabuka akaona yote yalikuwa mema na mazuri; akamwambia binadamu, “Haya, twende kazi!”
Viwanda vya binadamu vinatiririsha maji-taka ovyo hadi mitoni, maziwani na baharini na matokeo yamekuwa ni vifo vya viumbe vya majini kama samaki ambavyo ni urithi aliopewa na Muumba. Hakuna kiumbe kinachoweza kustahimili maisha bila maji safi. Maji yote sasa yametiwa sumu na binadamu kwa sababu ya ‘maendeleo’ yake. Joshi kutoka katika viwanda vivyo hivyo nalo limehasiri ukanda wa ozoni ambao sasa umeruhusu jua kutuhasiri kwa joto kali mno. Siku hizi inasemekana kuwa kuna mvua ya asidi inayonyensha katika baadhi ya sehemu za dunia na kuleta madhara makubwa. Labda hata mabahari yamekasirika kwa sababu hivi majuzi katika kile kilichoitwa ‘tsunami’ bahari lilihamia nchi kavu na kusomba maelfu ya binadamu na kuwameza wazima wazima. Vimbunga navyo vimetokea kwa wingi.
Wataalamu wanasema kuwa viwango vya miyeyuko vitazidi kwa sababu ya joto na kiwango cha maji kitazidi pia. Binadamu atatorokea wapi?
Idadi ya binadamu imezidi hadi kiasi asichoweza kukishughulikia kwa sababu anaijaza kiholela kwa sababu anadai kuwa aliruhusiwa kuijaza. Hii ni imani potovu. Anasahau kuwa alipewa ubongowa kuwaza na kuwazua kabla ya kufanya chochote. Dhiki, maradhi na ufukara zimehamia kwa binadamu na kumtia kiwewe.
Binadamu amefyeka misitu kwa kutaka makao, mashamba, mbao, makaa, ujenzi wa nyumba na
barabara na mahitaji mengine mengi. Wanyama wamefurushwa na wengi kuangamia kwa sababu ya
ukosefu wa chakula na wengine kushindwa kuhimili mabadiliko katika mazingira. Chemichemi za maji zimekauka nalo jangwa limeanza kutuzuru kwa kasi inayotisha. Kazi ya binadamu imekuwa ya kusukia kamba motoni. Itambidi aanze kujenga kwa matofali ya barafu!
Maswali
(a) Bila kupoteza maana iliyokusudiwa na mwandishi wa taarifa, fupisha aya ya kwanza. (Maneno 40-
50) (alama 5)
Matayarisho
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
Jibu
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(b) Kwa kuzingatia aya nne za mwisho, eleza mambo muhimu yanayoshughulikiwa na mwandishi.
(Maneno 95 – 105) (alama8)
Matayarisho:
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
Jibu:
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
MATUMIZI YA LUGHA(ALAMA 40)
(a) Kwa nini sauti ng’ ni king’ong’o? (alama 1)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(b) Taja aina mbili za mizizi na utolee mifano. (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(c) Tumia kihisishi kifuatacho katika sentensi kudhihirisha hisia yake. Labeka. (alama 1)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(d) Tunga sentensi ukitumia neno ghushi katika kauli ya kutendesha. (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(e) Weka nomino hizi katika ngeli zake. (alama 2)
(i) golegole
……………………………………………………………………………………………………
(ii) Mwiku
……………………………………………………………………………………………………
(f). Yakinisha sentensi hii katika hali ya udogo. (alama2)
Kono lake halijapona baada ya kuumwa na joka.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(g) Unda vitenzi kutokana na nomino zifuatazo. (alama2)
(i) Pete
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(ii) Muflisi
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(h) Tumia neno sura kudhihirisha mwingiliano wa nomino na kitenzi. (alama2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(i) Nukta pacha hutumiwa kutanguliza orodha na katika maandishi ya kitamthilia. Tunga sentensi
mbili kubainisha matumizi mengine mawili ya alama hii. (alama2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(j) Andika katika usemi wa taarifa. (alama3)
“Ahh! Unadhani atakupenda nani ikiwa mawazo uliyo nayo ni haya ya karne nyingi zilizopita”, alisema
samiji.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(k) Kwa kutoa mifano onyesha uamilifu wa chagizo katika sentensi. (alama2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(l) Changanua kwa kutumia mishale. (alama5)
Wananchi hawa ni wazalendo ingawa viongozi wao wangali wanafuja mali yao.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(m) Tumia kitenzi kishirikishi ‘ndi-‘ na nafsi huru ya tatu wingi. (alama1)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(n) Ainisha virai na vishazi katika sentensi hii. (alama3)
Mvuvi aliingia katika mto uliokuwa na mamba wengi.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(o) Bainisha matumizi ya ‘kwa’ katika sentensi ifuatayo. (alama2)
Aliishi Ujerumani kwa miaka mingi na kurudi nyumbani kwa ndege.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(p) Kanusha katika hali ya umoja. (alama2)
Mngaliwaendea walimu kwa mashauri mngalifaidika maishani.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(q) Tunga sentensi kubainisha maana mbili za neno luja. (alama2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(r) Eleza maana ya msemo huu. (alama2)
Kata choo.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(s) Andika upya sentensi ifuatayo ukitumia vinyume vya maneno yaliyopigiwa mstari. (alama2)
Msichana aliyevaa nguo tawili, alitwezwa na wenzake.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
D. ISUMU JAMII (alama 10)
1(a) Eleza sababu za lugha kufa. (alama5)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(b) Huku ukitoa mifano onyesha vile lugha inavyojiendeleza kimsamiati. (alama5)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers