Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Got a question or eager to learn? Discover limitless learning on WhatsApp now - Start Now!

Sotik District Mock - Kiswahili Paper 2 Question Paper

Sotik District Mock - Kiswahili Paper 2 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2011

Jina: …………………………………………………………………… Nambari: ………...………
Shule: ………………………………………………………………. Sahihi ....................................
Tarehe: …………….....................................................................……
102/2
KISWAHILI
LUGHA
KARATASI YA 2
JULAI/ AGOSTI 2011
MUDA: SAA 2 ½
Hati ya kuhitimu kisomo cha sekondari Kenya (K.C.S.E)
Kiswahili
Lugha
MAAGIZO
• Andika jina lako na namba yako katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
• Weka sahihi yako na tarehe ya mtihnai katika nafasi ulizoachiwa
• Jibu maswali yote.
• Majibu yaandikwe katika nafasi zilizoachwa wazi katika kijitabu hiki cha maswali.
Karatasi hii ina kurasa 8 zilizopigwa chapa. Watahiniwa ni lazima waangalie kama kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na
kuwa maswali yote yamo.
1. UFAHAMU
Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali yatakayofuata
Uchumi ni mfumo wa mapato, na matumizi ya watu katika nchi fulani. uchumi huu huhusisha
sekta mbalimbali kama vile utalii, kilimo, sanaa miongoni mwa sekta nyingine muhimu. Ukuaji wa kiuchumi hutegemea mambo kadhaa ili kuzaa matunda. Katika nji zote ulimwenguni, sera za kisiasa huamua jinsi uchumi utakavyokua na kunawiri. Kama siasa hazitilii maanani sera za ukuaji wa kiuchumi, basi mapato ya nchi hiyo hugubikwa katika wingu kubwa la uchochole Nchini Kenya, kwa mfano, kuna ulinganifu mkubwa kati ya siasa na ukuaji wa kuichumi.
Ukuaji wa kiuchumi hutegemea uteuzi wa maafisa wanaosimamia asasi muhimu sana. katika
usimamizi wa uchumi. Asasi hizi ni kama vile wizara ya fedha, Wizara ya Mipango ya kitaifa na Ruwaza ya 2030, Mamlaka ya Ukusanyaji wa ushuru ( KRA), Benki kuu ya Kenya (CBK), na tume ya kupambana na ufisadi (KACC). Usimamizi wa asasi hizi huwa muhimu sana katika kuamua
hatima ya uchumi wa nchi hii
Katika mwezi wa Juni kila mwaka, Waziri wa fedha husoma bajeti kwa Wabunge. Katika
maelezo yake yaitwayo. nakisi ya bajeti hujitokeza. Kabla ya bajeti kuandaliwa, Wizara ya Mipango huandaa hati iitwayo Usoroveya wa kiuchumi. Baada ya kusomwa kwa bajeti ni jukumu la Wabunge kupitisha mswada wa kifedha unaohusisha wizara zote au kuutupilia mbali. Jukumu hili linafaa kutekelezwa kufikia tarehe 31 Oktoba ya kila mwaka kulingana na sheria
Wakati huo huo, afisa anayejulikana kama Mhasibu Mkuu wa serikali huwa na jukumu la
kuchunguza na kutathmini matumizi ya fedha ya Wizara mbalimbali na kutoa ripoti yake kwa kamati ya Uhasibu wa Umma bungeni (PAC). Kamati hii hutoa mapendekezo yake kwa mkuu wa sheria na pia kwa Tume ya kupambana na ufisadi ili haki iweze kutekelezwa mahakamani iwapo dosari za kifedha zimefanyika.
Benki kuu ya Kenya kupitia kwa Gavana wake huwa na jukumu la kutoa ushauri kwa serikali
kuhusu usimamizi wa kifedha kuchunguza nguvu za shillingi ya Kenya dhini ya sarafa za kigeni, kutoa sarafu za Kenya kwa umma na usimamizi wa benki zote nchini miongoni mwa majukumu mengine.
Kwa upande mwingine, mamlaka ya Ukusanyaji ushuru Nchini huwa na jukumu la
kuhakikisha kuwa malengo ya ushuru yamefikiwa na pia kuhakikisha kuwa hakuna mtu binafsi au
kampuni yoyote inayokwepa kulipa ushuru Iwapo kuna udanganyifu wowote, basi swala hili linafaa kuangaliwa na mahakama zetu na haki kutekelezwa Kwa ujumla , sisi kama wananchi tunafaa kusaidia asasi hizi zote kufikia malengo. yake ili tupate ukuaji wa kiuchumi utakaofaidi watu wote. Jambo hili litahakikisha kuwa pengo lililo kati ya walalahai na walahoi liniezibwa. Sisi kama wananchi, tunafaa kuonyesha uzalendo wetu kwa nchi yetu kwa kulipa ushuru unavyetakikana , tukifuata mwito kuwa KULIPA USHURU NI
KUJIITEGEMEA. Mwisho, tusaidie viongonzi wetu katika kuendeleza sera mwafaka za kiuchumi ili nchi yetu ipige hatua kubwa katika ukuaji wa kiuchumi. Iwapo afisa yeyote atatuhumiwa kushiriki katika, kashfa yoyote ya kuhujumu nidhamu ya kifedhaa,basi anafaa kukabiliwa vilivyo, kisheria bila kujali hadhi yake ya kijaimi au kisiasa.
Maswali
a) Ipe habari hii kichwa awafaka (al.1)
.………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
b) Uchumi ni nini ? (al.1)
.………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
c) Ukuaji wa kiuchumi nchini Kenya hutegemea nini ? (al.1)
.………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
d) Benki kuu ya Kenya ina majukumu yepi ? (al.2)
.………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
e) Mhasibu Mkuu ana dhima serikalini ? (al. 2)
.………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
f) Pendekeza hatua mbili za kufufua, uchumi. (al. 2)
.………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
g) Ufisadi umehujumu vipi ukuaji wa kiuchumi ? (al. 2)
.………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
h) Ni vipi wakenya wanaweza kuonyesha uzalendo ? (al. 1)
.………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
i) Eleza maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika ufahamu. (a1.3)
i) Hatima
.………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
ii) Walalahai
.………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
iii) Walalahoi
.………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
2. MUHTASARI
Suala la demokrasia na haki ni mambo ambayo yamekuwa yakisisitizwa, nchini kenya tu,
bali katika ulimwengu mzima . Tangu miaka 90 ,nchi imekuwa ikipata sura mpya kila uchao. mfumo mpya wa vyama vingi vya kisiasa uliwatia wananchi hamu ya kudai haki zao na kupinga udhalimu wa kila aina. Hata hivyo, baadhi ya wananchi huvuka mipaka ya kudai haki hii na kuwakosea heshima viongozi , jambo ambalo ni tisho kwa demokrasia yenyewe.
Katiba ya Kenya imeeleza vyema suala la haki za kibinadamu katika mswada wa haki -
Mswada huu umeorodhesha haki za hiari ambazo mwana nchi anapaswa kuwa nazo. Kwa mujibu wa
katiba ya Kenya ,binadamu ana haki ya kuishi hivi ni kusema kwamba, hakuna mtu yeyote
anayepasa kuukatisha uhai wa mtu mwingine , ama kwa kumuua au kwa kusababisba kifo hicho,
kwa njia isiyo, moja kwa moja.
Aidha, kila Mkenya ana haki ya kupata elimu. Elimu humsaidia Mja kuwa mwananchi bora
na kuweza kuyakidhi mahitaji yake na ya familia yake.Ingawa elimu ni muhimu, tunapata kuwa
nchini humu kuna baadhi ya jamii ambazo huwaonjesha tu wana wao elimu. Utapata kwamba katika jamaa nyingi watoto, na hasa wa kike hupewa elimu ya kimsingi tu , yaani kufikia darasa la nane.
Jambo hili lazima likomeshwe kwa vyovyote vile.
Mkenya yeyote yule ana haki ya kumiliki mali ama kwa kununua au hata kurithi kutoka kwa
wazazi. Hata hivyo , utapata kwamba katika jamii nyingine watoto wengi , hasa wa kike , hunyimwa haki hii . Si ajabu kusikia mgogoro kupitia kwa vyombo vya habari baina ya ndugu
wa kiume na wa kike ; wakiume wakidai kuwa wa kike hapaswi kurithi mali ya wazazi. Hata baadhi ya wazazi wanapoena kuwa jua lao linakaibia kuchwa , huuza mali yao bila kujali watoto.
Mwananchi yeyote ambaye amefikisha umri wa miaka kumi na minane ana haki ya kupiga
kura kuchagua, viongozi awatakao.Haifai kwa mtu yeyote kumshurutisha mwingine kumpigia kura
mtu asiyetaka. Hili ni jukumu muhimu mno kwa kila mwananchi.Watu wote wanapoona kuwa
viongozi waliochukuliwa na wengine hawatekelezi wala kutimiza ahadi zao za kabla ya uchaguzi.
Mkenya yeyote yu huru pia kushiriki katika dhehebu analotaka kuabudia. Ana uhuru wa
kuchagua ni marafiki gani atakaoandamana nao mradi tu asiwe anavunja sheria. Hata hivyo , kwa miaka mingi, watu wamekuwa wakikiuka haki za kibinadamu kwa njia mbalimbali . Kwa mfano,utapata kwamba baadhi ya polisi huwashika washukiwa na kuwatesa bila sababu.
Mshukiwa hapaswi kuteswa na kuchukuliwa kuwa. mhalifu hata kabla ya kuhukumiwa . Haupiti muda kabla ya kusikia kamsa mitaani ya mama aliyeibiwa. Badala ya wananchi kumshika mshukiwa huyo na kumpeleka kwa polisi, wao hujichukulia sheria mikononi mwao na kumpiga kitutu Wengine huvishwa magurudumu na kuchomwa kwayo bila huruma Baadhi ya washukiwa hata wanapopelekwa kwenye hifadhi ya polisi hupigwa vibaya ili kukiri makosa yao. Wengi wa polisi hudhani kuwa jukumu lao kubwa ni kuadhibu hata pale ambapo hapana haja ya kuadhibu.
Watoto wengi wamekuwa wakiteseka kwa sababu wazazi wao wamekosa kuwapa malezi.Wazazi wengine , baada ya kutofautiana kidogo, hutalikiana na kuwaacha watoto chini ya ulezi wa mmoja wao. Mara nyingine mzazi anayeachiwa watoto huwa hajimudu na huteseka sana
kuwalea watoto hawa peke yake.Jambo hili huwakosesha raha watoto hawa na baadhi yao huishi
kukimbilia mitaani Binadamu ana haki ya kuishi vyema bila ubaguzi wala dhuluma za aina yoyote. Nijukumu la kila mwananchi kuhakikisha kwamba haki imedumishwa katika eneo lake.
Maswali
a) kwa kurejelea taarifa hii, eleza mambo yanayochukuliwa kuwa haki ya kila mtu .
(maneno 70-80) ( ala 9,mtiririko 2)
Nakala chafu
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
Nakala safi
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………..…
b) Ni vipi haki za kibinadamu zimekiukwa nchini (maneno 50) ( ala 6,mtiririko 2)
Nakala chafu
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
Nakala safi
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
3. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
(a) Taja konsonanti mbili ambazo hujulikana kama nusu irabu. (al. 2)
.………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
(b) Tunga sentensi ukitumia neno “kijana” kama ; (al. 2)
(i) Nomino
..……………………………………………………………………………………………………………
(ii) Kivumishi
..……………………………………………………………………………………………………………
(c) Tunga sentensi ukitumia viwakilishi vifuatavyo: (al.2)
(i) Kiwakilishi nafsi huru
..……………………………………………………………………………………………………………
(ii) Kiwakilishi nafsi kiambata
..……………………………………………………………………………………………………………
(d) Andika sentensi yakinishi kutokana na hii. (al. 1)
Chakula hakipikiki vizuri
..……………………………………………………………………………………………………………
(e) Tumia vitenzi vifuatavyo vya silabi moja kutunga sentensi katika kauli ya kutendewa. (al.2)
(i)-ja-
..……………………………………………………………………………………………………………
(ii)-la-
..……………………………………………………………………………………………………………
(f) Andika sentensi mbili ambazo zaweza kuwa sahihisho la sentensi ifuatayo. (al 2)
Juma ameingia katika chumbani mwake.
.………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
(g) Andika ukubwa wa sentensi hii. (al. 2)
Mwizi aliiba kikapu na ng’ombe.
..……………………………………………………………………………………………………………
(h) Tunga sentensi sahihi kubainisha matumizi ya “KI” kama: (al. 3)
(i) kielezi namna
..……………………………………………………………………………………………………………
(ii) hali ya kuendelea
..……………………………………………………………………………………………………………
(iii) masharti
..……………………………………………………………………………………………………………
(i) Andika kwa msemo wa taarifa (al. 3)
“Mimi nitawakaribisha wageni leo jioni kisha nitaondoka kwenda kwangu kesho” Fatuma
alimwambia Juma.
.………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
(j) Akifisha sentensi hii iletee maana mbili tofauti. (al. 2)
Baba Maria anakuja.
.………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
(k) Changanua sentensi ifuatayo kwa jedwali. (a. 4)
Mtoto mjeuri aliadhibiwa leo asubuhi.
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
(l) Andika sentensi zifuatazo upya kulingana na maagizo. (al. 2)
(i) Ng’ombe walipopotea mchungaji alikuwa na wasiwasi.
(Anza na: Kupotea)
..……………………………………………………………………………………………………………
(ii) Darasa lao halikuwa na milango mikubwa ya kupitia.(Anza: Milango mikubwa)
..……………………………………………………………………………………………………………
(m) “NI” ina matumizi gani katika sentensi hizi; (al.3)
(i) Eliza ni mpenzi wa Otieno.
..……………………………………………………………………………………………………………
(ii) Nitaenda Nairobi kesho.
..……………………………………………………………………………………………………………
(iii) Ameingia chumbani.
..……………………………………………………………………………………………………………
(n) Unda nomino kutokana na viarifa vifuatavyo. (al.2)
(i) Andika
..……………………………………………………………………………………………………………
(ii) Fa
..……………………………………………………………………………………………………………
(o) Tambulisha nyakati au hali za sentensi zifuatazo. (al.2)
(i) Naja
..……………………………………………………………………………………………………………
(ii) Nilikuwa nimeketi alipotembelea
..……………………………………………………………………………………………………………
(p) Ainisha mofimu katika neno “LILILONG’OLEKA” (al.3)
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
..……………………………………………………………………………………………………………
(q) Tunga sentensi ukitumia maneno yafuatayo ili kutofautisha maana .(al.2)
(i) sisi
..……………………………………………………………………………………………………………
(ii) zizi
..……………………………………………………………………………………………………………
(r ) Andika visawe viwili vya neno tabibu. (al.1)
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
4. ISIMU JAMII (ALAMA 10)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata
Kwa mujibu wa sheria kifungu nambari 3 sehemu ya A ya sheria za nchi, umepatikana na
hatia ya kutatiza utulivu wa raia wapenda amani kwa kuwatusi na kutisha kuwapiga. Kiongozi wa mashtaka amethibitisha haya kwa kawaleta mashahidi ambao wametoa ushahidi usiotetereka kuhusu vitendo vyao katika tukio hilo. Korti hii imeonelea una hatia na imeamua ufungwe jela kwa muda wa miaka miwili bila faini ili iwe funzo kwako na kwa wenzako wenye tabia kama zako. Una majuma mawili kukata rufani.
(a) Lugha katika kifungu hiki hutumika katika muktadha upi? (al.1)
…………………………………………………………………………………………………………
(b) Toa ushahidi wa jibu lako. (al.3)
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………………
(c) Zaidi ya sifa zilizo katika kifungu hiki, eleza sifa zingine nne za matumizi ya lugha katika
muktadha huu. (al.4)
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………..……
(d) Eleza maana ya sajili. (al. 2)
…………………………………………………………………………………………………………

More Question Papers

Popular Exams

Return to Question Papers