Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Laikipia District Mock- Kiswahili Paper 3 Question Paper

Laikipia District Mock- Kiswahili Paper 3 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2007



102/3
KISWAHILI
KARATASI YA TATU
FASIHI
JULAI / AGOSTI 2007
MUDA: SAA MBILI NA NUSU
JARIBIO LA TATHMINI YA PAMOJA WILAYA YA
LAIKIPIA
HATI YA KUHITIMU KISOMO CHA SEKONDARI
102/3
KISWAHILI
KARATASI YA TATU
JULAI / AGOSTI 2007
MAAGIZO
 Jibu maswali manne pekee.
 Swali la kwanza ni la lazima.
 Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki yaani;
(Tamthilia, riwaya, na fasihi simulizi.
 Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
HADITHI FUPI: MAYAI WAZIRI WA MARADHI.
1. “Nyumbani chakula cha mchana hakikulika vizuri, Alikula kidogo tu akaenda kulala. Akiwa kitandani ndoto za mchana zilianza kumsumbua. Katika ndoto ya kwanza aliota yeye na mawaziri wengine pamoja
na wabunge kadha……….”
(a) Ni mambo gani yalikuwa yametendeka kabla ya ndoto hii? (alama 10)
(b) Eleza tabia za mayai waziri wa maradhi kama inavyojitokeza katika hadithi hii
(alama 4)
(c) Taja ndoto zingine mbili alizoziota waziri wa mayai (alama 2)
(d) Mayai waziri alikuwa amefanya kazi nyingi baada ya kumaliza masomo yake. zitaje.
(alama 4)
TAMTHILIA KIFO KISIMANI: KITHAKA WA MBERIA
2. (a) Askari katika tamthilia ya kifo kisimani ni kioo cha askari katika jamii ya kisasa. Jadili
(alama 10)
(b) Wanawake ni kiini cha ukombozi wa Butangi katika tamthilia ya kifo kisimani. Thibitisha
(alama 10)
3. RIWAYA : MWISHO WA KOSA: Z. BURHANI.
“Juu ya masomo yako, makaratasi yako, na kizungu chako wewe ndiye mjinga mbele ya watu wote”
(a) Eleza asili ya ugomvi unaoendelea (alama 10)
(b) Hatima ya ugomvi huu ilikuwaje? (alama 5)
(c) Kwa kuzingatia tabia ya aliyezusha ugomvi huu thibitisha ukweli kuwa angali ujingani licha
ya kuwa amesoma. (alama 5)
4. Jadili jinsi swala la ndoa lilivyo sawiriwa katika jamii ya Mwisho wa kosa (alama 20)
5. FASIHI SIMULIZI
(a) Taja vipengele vyovyote vitano vya kipera cha hadithi (alama 5)
(b) Tofautisha kati ya mighani na maghani (alama 4)
(c) Ngomezi ni sanaa ya aina gani? (alama 2)
(d) Bainisha sifa na udhaifu wa ngomezi (alama 8)
(e) Ni utanga upi wa fasihi ulio na historia ndefu? (alama 1)
SEHEMU YA E: USHAIRI
Soma shairi lifuatalo kisha uiibu maswali
Duniani husifiki;
Wala hupati thamani,
Yalisemwa hukumbuki?
Na wazee wa zamani,
"Mkono haurambiki,
Bila kitu kiganjani"
Wangapi watu azizi,
Fulani bin Fulani,
Waliokichinja mbuzi,
Kukirimu mitaani,
Sasa kama wapuuzi,
Kwa hali kuwa ta'bani
Walifanya makubeli.
Wakaapa hadharani,
La uongo huwa kweli,
" Kubishika kitaani,
Na tangu kukosa mali,
Wakawa kama nyani!
Walifanya mahashumu.
Kuwaliko masultani,
Ushekhe na Ualimu,
Kufasiri vitabuni,
Na leo wana wazimu,
Kama si wanachuoni.
Maswali
(a) Kwa maneno yako mwenyewe eleza ujumbe wa shairi hili. (Alama 3)
(b) Eleza jinsi mshairi anavyosisitiza huo ujumbe katika shairi lote. (Alama 4)
(c) Eleza kwa tafsili umbo la shairi hili. (Alama 5)
(d) Andika ubeti wa kwanza katika lugha nathari. (Alama 3)
(e) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyo tumika katika shairi;
(i) Kiganjani.
(ii) Kukirimu.
(iii) Makubeli.
(iv) Mahashumu.
(v) Wanachuoni (Alama 5)
USHAIR1:
Soma shairi lifuatalo kisfea ujibu saaswali vanavofuata:
1.
Niliusiwa zamani, babu aliniusia, N
ili bado utotoni, hapo aliponambia,
Babu yaweke kitwani, yasije yakapotea,
Penye nia ipo njia, usikate tumaini.
2. Wewe bado ni mgeni, katika hii dunia,
Mimi ndiye wa zamani, mengi nimejionea,
Sasa niko uzeeni, uzee umewadia,
penye nia ipo njia, usikate tumaini.
3. Mtima ndio sukani, waongoza'kila ndia,
Weka mkazo moyoni, kila unalofwatia,
Moyoni mwako amini, kuwa utalifikia,
Penye nia ipo njia, usikate tumaini.
4. Kama uko safarini , waongoza kila ndia,
Bahari kuu kinani, mawimbi yakuchachia,
Usikate tumaini. hapo ndipo penye ndia,
Penye nia ipo njia, usikate tumaini.
5. Hapo hapo mawimbini, wewe hapo
pigania,
Hapo ndipo milangoni, mawimbi yakuzuia,
Mtima utie kani, bandarini utangia,
Penye nia ipo njia, usikate tumaini.
6. Na iwapo ni shuleni, masomo yakutatia,
Usiasi masomoni, kusoma ukakimbia,
Kidogodogo bongoni, elimu itakungia,
Penye nia ipo njia, usikate tumaini.
7. Kama wenda uchumini, biashara waania.
Usihofu asilani, hasara ikitukia,
Leo ukipata duni, na kesbo litazidia,
Penye nia ipo njia, usikate tumaini.
(a) Andika methaii ambayo ingetumiwa kujumuisha ujumbe katika ubeti wa pili. (Alama 1)
(b) Kutokana na shairi hili, ni katika nyanja zipi za maisha tunapopaswa kujikakamua? Tujikakamue vipi?
(alama 6)
(c) Taja arudhi ambazo zimetumiwa kuusarifu ubeti wa kwanza. (Alama 4)
(d) Huku ukitoa mfano mmoja bainisha uhuru wa kishairi ambao umetumiwa katika ubeti wa 3.
(alama 1)
(e) Andika ubeti pili kwa lugha ya nathari. (Alama 4)
(f) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi.
(i) Aliniusia.
(ii) Mtima.
(iii) Sukani
(iv) Waania. (Alama 4)






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers