-
a)Eleza tofauti kati ya sauti /z/ na /d/
b)Toa kigezo chochote kimoja cha kuainisha konsonanti
c)sentensi ifuatayo ina maana mbili tofauti. Zieleze.
Huyu amekuja kutuliza.
Date posted:
June 9, 2018
-
Eleza maana ya maneno yafuatayo
i)Kujizatiti
ii)Kichwa kuwa chepesi
iii)Vigae
Date posted:
June 9, 2018
-
a)Unda nomino kutokana na vivumishi vifuatavyo
i)Zuri
ii)Hodari
b)Yakinisha sentensi hii,
Asipotoka nje hataona cha mtema kuni
Date posted:
June 9, 2018
-
Eleza athari za lugha ya kwanza.
Date posted:
June 4, 2018
-
Onyesha jinsi majazi yametumika katika tamthilia ya Kigogo.
Date posted:
May 14, 2018
-
Kiswahili ni lugha ya kibantu kulingana na ushahidi wa ki-isimu. Thibitisha kauli hii.
Date posted:
May 14, 2018
-
Hatua ya serikali kuu kumpa kila mwanafunzi wa darasa la kwanza tarakilishi ni ya manufaa sana. Jadili.
Date posted:
May 14, 2018
-
Maenezi ya Kiswahili Afrika Mashariki punde baada ya uhuru yalikuwa na chagamoto tele. Fafanua zozote tano.
Date posted:
May 14, 2018
-
“We bwana unafikiri natumia petroli nini?”
(a) Uweke usemi huu katika muktadha wake. (al 4)
(b) Huku ukitoa mifano, eleza mbinu mbili za lugha zilizotumiwa na mwandishi katika dondoo hili. (al 4)
(c) Eleza migogoro yoyote sita inayojitokeza katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea. (al 12)
Date posted:
May 14, 2018
-
Kidagaa Kimemwozea
“....usiniweke pembeni kama tanbihi, mimi na wanawake wenzangu kama wanaume wengine wafanyavyo waandikapo...”
a) Fafanua muktadha wa dondoo hili (alama 4)
b) Fafanua mbinu mbili za uandishi zilizotumika hapa (alama 2)
c) Hakiki usawiri wa wahusika wa kike katika riwaya hii (alama 14)
Date posted:
May 14, 2018
-
Thibitisha jinsi mwandishi wa Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea alivyo fanikisha maudhui ya uwajibikaji.
Date posted:
May 14, 2018
-
Jadili mbinu ya sadfa katika Kidagaa Kimemwozea.
Date posted:
May 14, 2018
-
(i) Eleza maana ya Lingua Franka
(ii) Tambua sifa zozote tatu za Lingua Franka
Date posted:
May 14, 2018
-
Fafanua dhima tano za michezo ya chekechea
Date posted:
May 14, 2018
-
Taja miundo yoyote mitano ya nomino katika ngeli ya A-WA
Date posted:
May 14, 2018
-
Eleza umuhimu wa fasihi.
Date posted:
May 9, 2018
-
1.Taja aina nne za ngomezi za kisasa.
2. Eleza sifa nne za maapizo.
3. Eleza kikwazo vitatu vinavyokumba Fasihi simulizi.
Date posted:
May 4, 2018
-
Taja tanzu tano za fasihi simulizi
Date posted:
May 1, 2018
-
Taja maudhui yoyote sita ambayo hujitokeza Katika kazi yako fasihi andishi
Date posted:
May 1, 2018
-
“Hatimaye Tarishi alikuja na barua moja ya Mtemi na nakala ya siku hiyo ya gazeti la Tomoko Leo: Mtemi Nasaba Bora akapokea barua hiyo na gazeti toka kwa tarishi aliyekuwa kanywea si haba.”
(a) Jadili mambo yaliyomshtua Mtemi Nasaba Bora kuhusiana na barua na gazeti alizopokea siku hiyo.
(b) Onyesha jinsi madhubuti alivyoendeleza uasi dhidi ya babake.
Date posted:
April 30, 2018
-
“Lowela tunapendana mno na ni msiri wangu wala hakuogopa kuniambia yaliyojiri.
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Fafanua ‘yaliyojiri’ kwa mujibu wa msemaji.
(c) Lowela ni kielelezo kibaya cha msichana wa kisasa.
Thibitisha.
Date posted:
April 30, 2018
-
Ujenzi wa jamii mpya ni wajibu wa vijana. Thibitisha ukweli wa kauli hii ukirejelea riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.
Date posted:
April 30, 2018
-
Onyesha jinsi mbinu ya Taharuki imetumiwa katika Tamthilia ya kigogo
Date posted:
April 30, 2018
-
Jadili maudhui ya siasa katika Tamthilia ya kigogo
Date posted:
April 30, 2018
-
Jadili kwa kina sifa zozote tano zinazokitambulisha Kiswahili kama lugha ya kibantu.
Date posted:
April 30, 2018
-
Jadili juhudi za TUKI katika kuendeleza na kustawisha Kiswahili katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Date posted:
April 30, 2018
-
Eleza nafasi ya makundi yafuatayo katika ama kukua au kudhoofika kwa Kiswahili nchini Kenya kabla ya uhuru.
a) Watawala
b) Wamisheni
c) Walowezi
(alama 15)
Date posted:
April 30, 2018
-
Jadili aina tatu za ‘maana’ huku ukizitolea mifano kutoka Kiswahili.
Date posted:
April 30, 2018
-
Upepo unapovuma, kaskazi kwenda kusi ,
Kwa ngurumu kututuma, ukivisomba vifusi,
Ukasukua milima, nakuyang' oa manyasi,
IIi kukwepa mikosi, miti mikuu hwinama.
Miti mile iloimia , ikaijaza nafasi,
Kwa matawi yake mema, kusheheneza utosi,
Haiwi iko salama, upepo ukenda kasi,
IIi kukwepa mikosi , miti mikuu hwinama.
Upepo ukiivuma , miti haitaanasi,
Huchezeshwa lelemama, ikachezeshwa na dansi,
Matawi yake hunema , yakakatika rahisi,
IIi kukwepa mikosi, miti mikuu hwinama.
Upepo ukitetema, hukata kama makasi,
Miti hwingia ulema, uzima ukawa basi,
Hilivunja tawi zima, kama eawi halinesi,
IIi kukwepa mikosi, miti mikuu hwinama.
Upepo una zahama , hasa ule wa chunusi,
Hata misitu hwandama, ikabaki mufilisi,
Matawi mani huhama, ikapoteza nemsi,
IIi kukwepa mikosi, miti mikuu hwinama.
Upepo unasukuma, miti hula sarakasi,
Matawi yakachutama, mengi chini hujilisi,
Watu ukiwatazama, wanavuja makamasi,
IIi kukwepa mikosi, miti mikuu hwinama.
Ndege wachimachima, viota wameviasi,
Wakajiweka wanyama, kwenye vichaka yabisi,
Majahazi yaparama, yakenda mwemdo wa ngisi,
IIi kukwepa mikosi, miti mikuu hwinama .
.
Miti mile yenye kima , yenye tambo mahsusi,
Mtawi kakikingama, ili upepo kuuasi,
Billahi yaja nakama, kubwa tena kwa wepesi,
IIi kuwepa mikosi, miti mikuu hwinama.
Miti mile hungama, na kujidhili nafusi,
Upepo ukishavuma, ndipo inatanafusi,
Vinginevyo ni kiyama, hapana wa kuramisi,
Ili Kukwepa mikosi, miti mikuu hwinama.
Maswali
(h) Andika kichwa mwafaka cha shairi hili. (alama 2)
(i) Eleza ujumbe uliomo katika shairi hili. (alama 3)
(j) Taja na utoe mifano ya tamathali za usemi zilizotumiwa katika shairi. (alama 4)
(k) Eleza muundo wa shairi hili. (alama 4)
(l) Andika ubeti wa sita kwa lugha nathari. (alama 4)
(m) Eleza maana ya misamiati ifuatayo kama ilivyotumiwa katika shairi.(alama 3)
(i) Kututuma
(ii) Haitaanasi
(iii) Zahama
Date posted:
April 30, 2018
-
1. Na ujenge nyumba yako, jingi jasho likuoshe,
Ufyeke, upime na uweke nguzo,
Kisha paa uweke na ukandike,
Siku nyingi bila kuingiliwa na mgeni hutakaa.
Wataanza kutalii mpaka mende usiku,
Nje na ndani ya nyumba watazunguka,
Bila woga, bila ruhusa ulichonacho watakula,
Masalia yatakuwa yako, ijara ya kaziyo.
Na nyingi dawa uweke, nyumba nzima uihame,
Ukae nje nzima siku usubiri,
Wazima wamelala ukirudi usiku,
Vichwa vigumu hawafi mende rahisi.
Kifo cha mende sharti miguu juu
Kichwa ukikanyage kipasuke usikie,
Na kisha wengine usiku mchana uwasake.
Mpaka watakapokwisha. Usiseme nao.
Maswali
(a) (i) Hili ni shairi la aina gani? (alama 1)
(ii) Tetea jibu lako. (alama 3)
(b) Eleza jinsi mshairi alivyoutumia uhuru wake katika utunzi wa shairi hili. (alama 4)
(c) Taja mbinu mbili za lugha alizotumia mshairi na uzitolee mifano. (alama 4)
(d) Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari. (alama 4)
(e) Eleza ujumbe wa mshairi. (alama 2)
(f) Toa mfano mmoja wa mshata. (alama 1)
(g) Kichwa gani kinaliafiki shairi hili? (alama 1)
Date posted:
April 30, 2018