Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Kakamega District Mock - Kiswahili Paper 3 Question Paper

Kakamega District Mock - Kiswahili Paper 3 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2007



102/3
KISWAHILI
KARATASI YA TATU
FASIHI
JULY / AUGUST 2007
MUDA: SAA MBILI NA NUSU
JARIBIO LA TATHMINI YA PAMOJA WILAYA YA
KAKAMEGA
HATI YA KUHITIMU KISOMO CHA SEKONDARI
(K.C.S.E) 2007
102/3
KISWAHILI
KARATASI YA TATU
JULAI / AGOSTI 2007
MAAGIZO
 Jibu maswali manne pekee, swali la kwanza ni la lazima.
 Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki. (Tamthilia, riwaya,
hadithi fupi na Fasihi simulizi.
 Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
1. SEHEMU: A
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yote.
KIPIMO NI KIPI?
Nitampa nani, sauti yangu ya dhati
Kwa kipimo gani, ingawa kiwe katiti
Amefanya nini, La kutetea umati
Kipimo ni kipi?
Yupi wa maani, asosita katikati
Alo na maoni, yasojua gatigati
Atazame chini, kwa kile ule wakati
Kipimo ni kipi?
Alo mzalendo, atambuaye shuruti
Asiye mafundo, asojua mangiriti
Anoshika pendo, hata katika mauti
Kipimo ni kipi?
Kipimo ni kipi, changu mimi kudhibiti
Utu uko wapi, ni wapi unapoketi
Nije kwa mkwapi, au ndani kwa buheti
Kipimo ni kipi?
(a) Eleza umbo la shairi hili Alama 4
(b) Taja tamadhaliza usemi na kisha utoe mifano Alama 3
(c) Taja na ueleze namna mshairi alivyotumia uhuru wa ushairi? Alama 2
(d) Eleza maudhui ya shairi hili? Alama 3
(e) Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari Alama 4
(f) Eleza msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa Alama 4
(i) Katiti
(ii) Gatigati
(iii)Shuruti
(iv) Mangiriti
SEHEMU: B
KIFO KISIMANI: KITHAKA WA MBERIA.
2. Uovu wa uongozi katika nchi zinazokua umejikita barabara tamthiliani. Thibitisha Alama 20
3. “Ni kweli Naota. Naota daima. Naota juu ya Butangi….”
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili? Alama 4
(b) Taja mambo ambayo aliyaotea? Alama 7
(c) Ni mambo yapi yanaonyesha kuwa utawala wa mtemi Mrima ulikuwa bora? Alama 6
(d) Maua ya kazi ya wana butangi yalichanua na kupamba mandhari ya Butangi? Toa sababu
Alama 3
MWISHO WA KOSA: Z. BURHANI.
4. Vitafidhina ni dhana ambayo imekithiri mizizi katika uga wa mwandishi. Jadili ukitoa mifano mwafaka kutoka riwayani
5. “Mimi nitasafiri kwa muda mfupi kwa kazi, na nilitaka kukushukuru kwanza kwa msaada
wako………….”
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili Alama 3
(b) Eleza kwa nini kuna kutoa shukrani Alama 1
(c) Taja manufaa ya yule anayezungumza katika riwaya hii kwa nchi na wahusika wengine.
Alama 6
(d) Anayezungumziwa aliadhirika vipi? Alama 3
(e) Taja sifa za anaye zungumziwa Alama 7
SEHEMU:C
FASIHI SIMULIZI
6. Eleza maana ya maneno haya
(a) Soga. Alama 2
(b) Miviga. Alama 2
(c) Eleza umuhimu wa maghani Alama 6
(d) Taja methali zenye maana sawa na hizi Alama 3
(i) Jifya moja haliinjiki chungu.
(ii) Mavi ya kale hayaachi kunuka.
(iii)Ukiona vyaelea vimeundwa.
(e) Eleza sifa za misimu Alama 7
MAYAI WAZIRI WA MARADHI NA HADITHI NYINGINEZO
K.W WAMITILA
7. Wajadili wahusika hawa kama wanavyosawiriwa katika hadithi fupi?
(a) Mayai waziri wa maradhi Alama 6
(b) Daktari Pondamali Alama 4
(c) Hadithi ya Mayai waziri wa maradhi ni kielelezo cha mataifa ya kiafrika jadili. Alama 10






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers