Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Bungoma District Mock- Kiswahili Paper 3 Question Paper

Bungoma District Mock- Kiswahili Paper 3 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2007



102/3
KISWAHILI
KARATASI YA TATU
FASIHI
JULY / AUGUST 2007
MUDA: SAA MBILI NA NUSU
MTIHANI WA MWIGO WILAYA YA BUNGOMA 2007
HATI YA KUHITIMU KISOMO CHA SEKONDARI KENYA
(K.C.S.E)
102/3
KISWAHILI
KARATASI YA TATU
JULAI / AGOSTI 2007
MAAGIZO
 Jibu maswali manne pekee, swali la kwanza ni la lazima.
 Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki. (Tamthilia, riwaya,
hadithi fupi na Fasihi simulizi.
 Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
Karatasi hii ina kurasa nne zilizopigwa chapa. Mtahiniwa ahakikishe kwamba kurasa zote zimepigwa chapa
sawasawa na kuwa maswali yote yamo.
1. Soma shairi hili kisha ujibu mawali yanayofuata.
SABUNI YA ROHO
Ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia?
Ndiwe suluhu la zama, waja wakukimbilia,
Waja wanakutazama, madeni wakalipia,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Ndiwe mafuta ya roho, walisema wa zamani,
Utanunua majoho, majumba na nyumbani,
Umezitakasa roho, umekuwa mhisani,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Matajiri wakujua, wema wako wameonja,
Nguo zao umefua, wakupata kwa ujanja,
Sura Zao ‘mefufua, Wanazuru kila nyanja,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Ndiwe mvunja mlima, onana na masikini
Watazame mayatima, kwao kumekua wa duni
Wabebe waliokwama, wainue walio chini,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Ndiwe mvunja mlima,wapi kapata uwezo?
Umezua uhasama, waja kupata mizozo,
Ndiwe chanzo cha zahama, umewaitia vikwazo,
Ndiwe sabuni ya roho, Ndiwe mvunja mlima.
Umevunja usuhuba, familia zazozana,
Walokuwa mahabuba, kila mara wagombana,
Roho zao umekaba, majumbani wachinjana,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Nakutafuta kwa hamu, sabuni unirehemu,
Sinilipue ja bomu, sije kawa marehemu,
Niondoe jehanamu, ya ufukara wa sumu,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Naondoka wangu moyo, nikuitapo itika
Fulusi wacha uchoyo, tatua yalonifika,
Nichekeshe kibogoyo, nami nipate kuwika,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
(a) Mshairi anaongea na nani katika shairi hili? [alama 1]
(b) Taja majina mengine matatu aliyopewa huyu anayesemeshwa. [alama 3]
(c) Anayezungumziwa katika shairi hili amesababisha balaa gani? [alama 2]
(d) Mshairi anatoa mwito gani kwa mwenziwe? [alama 4]
(e) Fafanua maudhui ya ubeti wa sita. [alama 2]
(f) Mbinu kadha za uandishi zimetumiwa na msanii kuwasilisha ujumbe wake. Taja
mbinu zozote tatu na uzitolee mifano katika shairi. [alama 3]
(g) Fafanua maana ya:
Sura zao “mefufua, wanazuru kila nyanja. [alama 1]
(h) Andika ubeti wa saba katika lugha nathari. [ alama 4]
TAMTHLIA
KITHAKA WA MBERIA: Kifo Kisimani
2. ‘Kazi ya mikono yangu yenyewe: nimechoma mwiba tayari. Kisu kilipata--------------’
(a) Fafanua muktadha wa dondoo hili [alama4]
(b) Ni mambo gani yaliyosababisha kuzuka kwa ‘Mwiba’ Unaotajwa katika dondoo hili.
[alama 4]
(c) Kwa kutumia mifano mitatu, dhihirisha jinsi wanawake walivyochangia katika
ukombozi wa Butangi. [alama5]
(d) Eleza hatima ya msemaji wa maneno haya. [alama 7]
RIWAYA
Z.Burhani: MWISHO WA KOSA:
Jibu swali 3 au 4.
3. “ Mbio za sakafuni huishia ukingoni.” Thibitisha ukweli wa madai haya kwa kurejelea
wahusika watano kutoka katika riwaya ya ‘Mwisho wa kosa.’ [alama 20]
4. “------- Mnavyotaka ni kuwa nifanye kazi kwa akili yangu na nguvu zangu, nikulisheni nyinyi na
watoto wenu! Nikuacheni hata mniendeshee maisha yangu. Hizo ni fikra za kipuuzi na za
kizamani---------”
(a) Fafanua muktadha wa dondoo hili [alama 4]
(b) Kauli hii ilikuwa na athari zipi kwa msemaji na wasemewa? [alama 4]
(c) Dondoo hili linadhihirisha migongano iliyoko kati ya wale wenye fikra za kisasa na
wanaodaiwa kuwa na fikra za kipuuzi na za kizamani. Fafanua visa vine vinavyotoa
ithibati ya madai haya. [alama 12]
HADITHI FUPI
K.W.Wamitula: Mayai waziri wa maradhi.
Jibu swali 5 au la 6
Mayai waziri wa maradhi
5. [-------- Katika ukurasa huu aliona picha ya mama yake. Kifua wazi akinyonyesha kitoto
kimeshika ziwa lililonyauka hali kikitazama kidevu cha mama yake-----]
(a) Ni kweli kuwa picha hizi zinatoa muhtasari wa maisha ya mayai waziri wa maradhi.
Taja picha zingine alizozitazama huku ukieleza sababu za kuzipenda au kuzichukia.
(Alama 10)
(b) Hadithi ya mayai waziri wa maradhi inaangazia matatizo yanayozikabili nchi za
kiafrika. Thibitisha kauli hii kufafanua matatizo yoyote matano.
(Alama 10)
6. Uteuzi wa moyoni
Fafanua changamoto zinazomkabili mwanamke katika hadithi ya ‘uteuzi wa moyoni’
[alama 20]
FASIHI SIMULIZI
7. (a) (i) Ngano ni nini? [alama 1]
(ii) Eleza tofauti iliyoko kati ya visasili na visakale [alama 4]
(iii) Fafanua majukumu yoyote muhimu ya ngano katika jamii. [alama 5]
(b) (i) Eleza umuhimu wa vitendawili katika jamii. [Alama 3]
(ii) Tega na utegue vitendawili vyovyote viwili vilivyo na lugha ya takriri na lugha ya
mlio. [alama 2]
(iii) Taja sifa zozote tatu za methali. [alama 3]
(iv) Taja methali yoyote iliyo na lugha ya balagha kisha ueleze maana yake ya ndani
[alama 2]






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers