Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Bungoma District Mock- Kiswahili Paper 1 Question Paper

Bungoma District Mock- Kiswahili Paper 1 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2007



102/1
KISWAHILI
KARATASI 1
INSHA
JULAI / AGOSTI 2007
MUDA 1 ¾
MTIHANI WA MWIGO WA WILAYA YA BUNGOMA
HATI YA KUHITIMU KISOMO CHA SEKONDARI KENYA
(K.C.S.E) 2007
102 /1
KISWAHILI
KARATASI 1
INSHA
JULAI /AGOSTI 2007
MAAGIZO
 Andika insha mbili. Swali la kwanza ni la lazima kisha chagua insha nyingine kutoka kwa hizo tatu zilizobakia.
 Kila insha isipungue maneno 400.
 Kila insha ina alama 20.
Karatasi hii ina kurasa mbili zilizopigwa chapa. Mtahiniwa ahakikishe kwamba kurasa zote zimepigwa chapa
sawasawa na kuwa maswali yote yamo.
1. Hivi karibuni ulisafiri kwenda sehemu fulani ya Kenya, katika safari yako ulishuhudia uvunjaji wa
sheria barabarani. Mwandikie barua mkuu wa polisi ukimwarifu kuhusu mambo uliyoyashuhudia,
Kisha upendekeze jinsi ya kukabiliana na hali hiyo.
2. Mwenye Kovu usidhani kapoa.
3. Ukosefu wa usalama ni tatizo sugu katika nchi yetu. Jadili njia mbalimbali za kuweza kukabiliana na tatizo hili.
4. Andika insha itakayokamilika kwa:
…… kulipokucha nilimwangalia kakangu alivyodhoofika, nilikumbuka wosia wa baba kabla
hajaaga dunia. Machozi yalinidondoka njia mbili.






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers