Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Bondo District Mock - Kiswahili Paper 3 Question Paper

Bondo District Mock - Kiswahili Paper 3 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2007



Jina………………………………………………… Nambari . ……………………………….
Shule ………………………………………………...
102/3
Kiswahili
(FASIHI)
Karatasi 3
JULAI/AGOSTI 2007
Muda: Saa 2 ½
WILAYA YA BONDO MTIHANI WA MWIGO WA K.C.S.E - 2007
Hati ya Kuhitimu Kisomo Cha Sekondari Kenya (K.C.S.E.)
102/3
Kiswahili
(FASIHI)
Karatasi 3
JULAI/AGOSTI 2007
Muda: Saa 2 ½
MAAGIZO
• Jibu maswali manne pekee
• Swali la kwanza ni la lazima
• Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki yaani: Tamthilia,
Riwaya, Hadithi Fupi na Fasihi Simulizi.
• Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
Karatasi hii ina kurasa 4 zilizopigwa chapa
Watahiniwa lazima wahakikishe kurasa zote zimepigwa chapa sawa sawa na kuwa maswali yote yamo.
USHAIRI
1. Soma shairi hili kisha ujibu maswali.
Jicho, tavumiliaje, kwa hayo uyaonayo?
Kicho, utasubirije, maonevu yapitayo
Kwacho, lijalo na lije, nimechoka vumiliyo
Naandika!
Moyo, unao timbuko, maudhi tuyasikiayo
Nayo, visa na mauko, wanyonge wayakutayo
Kwayo, sina zuiliko, natoa niyahisiyo
Naandika!
Hawa, wanotulimiya, dhiki wavumiliayo
Hawa, mamiya mamiya, na mali wazalishayo
Hawa, ndo wanaoumiya, na maafa wakutayo
Naandika!
Hawa, sioni wengine, kwao liko angamiyo
Hawa, uwapa unene, watukufu wenye nayo
Hawa, bado ni wavune, kwa shida waikutayo
Naandika!
Bado, wawapo mabwana, wenye pupa na kamiyo
Bado, tafauti sana, kwa pato na mengineyo
Bado, tuling’owe shina, ulaji pia na choyo
Naandika!
Maswali
(a) Shairi hili laweza kuwekwa katika bahari zipi? (alama 4)
Thibitisha kila jibu lako.
(b) Eleza dhamira ya mshairi. (alama 2)
(c) Onyesha mifano miwili ya uhuru wa kishairi jinsi ulivyotumika katika shairi. (alama 2)
(d) Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari. (alama 4)
(e) Tambulisha kwa mifano mbinu zozote mbili za sanaa katika shairi. (alama2)
(f) Fafanua sifa za kiarudhi zilizotumika katika ubeti wa tano. (alama 3)
(g) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika shairi. (alama 3)
(i) Zuiliko
(ii) Wavune
(iii) Wenye pupa na Kamiyo.
TAMTHILIA: Kithaka Wa Mberia: KIFO KISIMANI
2. a) Kwa kutoa mifano, eleza matumizi matano ya jazanda katika tamthilia ya KIFO
KISIMANI. (alama 10)
b) ‘Tamthilia ya KIFO KISIMANI imetumia mbinu rejeshi katika kuwasilisha ujumbe wake’.
Thibitisha ukweli wa kauli hii. (alama 10)
RIWAYA
Z. Burhani: MWISHO WA KOSA
3. “………. sikukuita kuja kukulaumu, wala kukuhoji kuhusu maisha yako, lakini kama
unavyojua sisi ni wazee, na wajibu wa mzee anapomwona mwanawe anakwenda mwendo sio
lazima amwambie au ajaribu kumwongoza”.
a) Fafanua muktadha wa maneno haya. (alama 4)
b) Ni mwendo gani usio ambao unarejelewa? (alama 4)
c) Fafanua jinsi ambavyo mwanamke ni kama kielelezo bora cha maadili katika jamii
ukirejelea riwaya ya MWISHO WA KOSA. (alama 12)
HADITHI FUPI
K.W Wamitila: MAYAI WAZIRI WA MARADHI NA HADITHI NYINGINE
Jibu swali la 4 au la 5
E. Kezilahabi: Mayai Waziri wa Maradhi
4. “Nyumbani chakula cha mchana hakikukulika vizuri. Alikula kidogo tu akaenda zake kulala.
Akiwa kitandani ndoto za mchana zilianza kumsumbua.
a) Kwa mujibu wa dondoo hili, rejelea ndoto mbili ambazo zinazungumziwa. (alama 4)
b) Hadithi ya MAYAI WAZIRI WA MARADHI ni mfano mzuri wa mwachano uliopo baina
ya watawala na wananchi (raia). Tetea kauli hii. (alama 8)
c) Fafanua dhana ya 10 katika hadithi ya MAYAI WAZIRI WA MARADHI. (alama 4)
d) Taja na ufafanue mifano yoyote minne ya jazanda zilizotumika katika hadithi hii ya
MAYAI WAZIRI WA MARADHI. (alama 4)
Ama
5. Clara Momanyi: NGOME YA NAFSI
“Mamangu eee! Niachilieni! Nishusheni mie sitaki kuolewa jamani eee!”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 2)
b) Kwa kutoa mifano mwafaka katika hadithi hii na nyinginezo, onyesha vile wahusika wa
umri wa mhusika huyu wanavyonyimwa haki zao. (alama 8)
c) Ukirejelea hadithi ya NGOME YA NAFSI thibitisha jinsi ambavyo sifa bainifu za hadithi
fupi zinajitokeza huku ukitoa mifano mwafaka. (alama 10)
FASIHI SIMULIZI
6. a) Eleza maana ya tanzu zifuatazo za Fasihi Simulizi ( alama 4)
(i) Vitanza ndimi
(ii) Vitendawili
(iii) Ngano
(iv) Nyimbo
b) Taja sifa mbili mbili za kila mojawapo wa vipera vya fasihi simulizi vilivyotajwa katika (a)
(alama 8)
c) Eleza umuhimu wa vitanza ndimi. (alama 4)
d) Fafanua uamilifu wa vitendawili katika jamii. (alama 4)






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers